SERIKALI INATAMBUA NISHATI NI MUHIMU KATIKA KUCHOCHEA MAENDELEO YA KIUCHUMI

April 10, 2024

 Na Janeth Raphael  -Dodoma


Tanzania imendelea kushirikiana na wataalum sambamba na michango ya wadau wa nje na ndani ya nchi katika kuhimiza matumizi ya nishati Mbadala katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dodoma katika Ukumbi wa Afrika Dream na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt James Mataragio wakati wa ufunguzi wa warsha iliyolenga kuhamasisha wananchi juu ya kutumia Nishati Jadilifu.

Dkt Mataragio amesemae Serikali inatambua kwamba nishati ni muhimu katika kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya 2025 ambayo Serikali imejipangia.

“zaidi sera yetu ya nishati ya 2015 inatambua umuhimu wa wadau na katika kufikia malengo ya kuwa na nishati jadilifu, kulingana na mahitaji ya upatikanaji nishati nchi nzima na kwa bei himilivu ambayo ni hitaji la msingi katika kukuza uchumi, na kuboresha maisha,” albainisha.

Aidha Matarajio ya Taifa ni kuweka Misingi thabiti na kuchochea matumizi ya nishati jadilifu, katika kukuza maendeleo ya nchi na ustawi wa watu.

Pia katika kutizama mabadiliko ya hali ya hewa na kuondoa umasikini, Serikali imeendelea kuweka mkazo katika upunnguzaji wa hewa ya kaboni kupitia sera zake ikiwemo ya Mwaka 2021 ambayo inaainisha malengo ya 30-35% ya kupunguza matumizi ya hewa ya ukaa.

Ameongeza kusema kuwa mashirika ya Climate Action Network Tanzania na Power Afrika na taasisi ya suistainable Futures wanaanda taarifa yenye mchanganuo wa njia ya mbalimbali zinaweza kusaidia kujikita katika matumizi ya nishati jadilifu.

“Tunahitaji michango ya mawazo katika taarifa hii kusaidia kufikia malengo ya matumizi endelevu ya nishati yakayosaidia wizara kutumia taarifa katika mipango yake iliyoainisha,” alisema.







 

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »