NA VICTOR MASANGU KIBAHA
KATIBU
wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Bernard Elias Ghati
amewahimiza wana ccm pamoja na wananchi kwa pamoja kumchagua kwa
kishindo mgombea wa udiwani kata ya Msangani Gunze Yohana ili aweze
kuwaletea wananchi maendeleo.
Katibu huyo ameyasema hayo wakati
wa mkutano wa kampeni wa hadhara kwa ajili ya kuweza kumnadi mgombea wa
udiwani uliofanyika katika mtaa Garagaza.
Katika mkutano huo wa
kampeni ambao ulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ngazi ya Wilaya
pamoja na ngazi ya Mkoa sambamba na wananchi wengine kutoka Jimbo la
Kibaha mjini.
Katibu huyo aliwaomba katika kuelekea katika
uchaguzi huo wananchama wa ccm wanapaswa kuwa kitu kimoja katika
kuhakikisha kwamba wanashinda kwa kishindo kwa asilimia kubwa katika
uchaguzi huo.
"Kikubwa tunakuja katika mikutano hii kwa ajili ya
kuzungumza mambo mbali mbali ambayo chama cha mapinduzi mambo ambayo
yamefanyika katika utekelezaji wa Ilani hivyo wananchi wa Msangani
inabidi kumchagua mgombea wetu Gunze '"alisema katika huyo.
Aidha
katibu huyo alisema kuwa wana ccm wanatakiwa kuungana kwa pamoja na
wananchi wote wa kata ya Msangani kwa lengo la kuwaeleza mambo mbali
mbali yaliyofanyika ya kimaendeleo.
"Inatakiwa wana msangani wote
muelewe shughuli mbali mbali za kimaendeleo ambazo zimefanywa na hivyo
ninawaomba wananchi kumchagua Gunze awe diwani wa kata ya
Msangani,"alisema Katibu huyo.
Katika hatua nyingine aliongeza
kuwa endapo wananchi wa kata ya Msangani wakimchagua Gunze kuwa diwani
wa Kata ya Msangani ataweza kuwaletea maendeleo wananchi katika nyanja
mbali mbali ikiwemo maji,afya,elimu pamoja na maeneo mengine.
Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani amnayo ilikuwa wazi unatarajiwa kufanyika machi 20 mwaka huu.
EmoticonEmoticon