NAIBU WAZIRI DAVID KIHENZILE ATEMBELEA BANDA LA TASAC MAONESHO YA MIAKA 60 YA MAPINDUZI

January 15, 2024

 

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile  akizungumza na watumishi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) alipofika kwenye banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Sheria Mkuu kutoka TASAC Devotha Mandanda alipotembelea banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Mwandamizi Ukaguzi wa Meli kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Kapt. Ghadaf  Chambo kuhusu namna ya kusajiliwa kuwa kapteni wa meli alipotembelea banda la TASAC kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akisaini kitabu mara baada ya kupata maelezo kweye banda la Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar
Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Afisa Sheria Mkuu kutoka TASAC Devotha Mandanda pamoja na kupiga picha ya pamoja mara baada ya kutembelea Banda la Shirika hilo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba, Zanzibar.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »