MKUU WA MKOA WA TANGA AWAONYA MAFATAKI

January 09, 2024











Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kinamba akiwa amekaa kwenye dawati na wanafunzi wa shule ya msingi Bombo mara baada ya kutembelea shuleni hapo leo january 8,2024.




Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akiwa amekaa na wanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Bombo iliyopo jijini hapa mara baada ya kutembelea shuleni hapo kukagua kuwasili kwa wanafunzi hao kwa mwaka mpya wa masomo 2024.








Na Mwandishi Wetu,TANGA

SERIKALI mkoani Tanga imetoa onyo kali kwa wanaume ambao wamekuwa wakijihusisha kimapenzi na wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari kuacha tabia hiyo huku ikiwaagiza wakuu wa wilaya  za mkoa huo kusimamia na kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote ambaye atabainika kujihusisha na vitendo hivyo.

Kauli hiyo ilitolewa Januari 8 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba wakati wa ziara yake ya kuzitembelea shule za Msingi Bombo na Sekondari Old Tanga kukagua hali ya kuripoti kwa wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo pia amatoa onyo kwa wazazi na walezi ambao wamekuwa wakimaliza kesi kifamiliya na wahusika mara baada ya watoto wao kupata ujawazito.

Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara hiyo Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba vipi vitendo  kwa baadhi ya wananchi wasiokuwa na tabia nzuri wanaoitwa "Mafataki"ambao wamekuwa wakitembea na  wanafunzi hii sio sawa na haikubaliki.

"Niwaambie kwamba wakati wangu mimi kama mkuu wa mkoa wa Tanga sitavumilia , sitastahamili walasitakuwa na simile na mtu yeyote anayeharibu maisha ya mwanafunzi , ukitaka kufanya hivyo chukua umri wako jumlisha na miaka 30 ya gerezani uone utatoka ukiwa na umri gani" Alisisitiza RC Kindamba

Katika kusisitiza jambo hilo Mkuu huyo wa Mkoa aliwataka  wakuu wa wilaya za mkoa huo kusimamia watoto hao na watakaobainika kujihusisha na vitendo vya mapenzi na watoto wa shule wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

"Nimeanza  kupata kesi kutoka kwa baadhi ya wazazi kesi zikishaenda mahakamani baadaye wanawaficha watoto au wanakaa kikao kifamilia mtu yeyote atakayecheza na watoto wa shule ajue anacheza na watoto wa serikali" Alisema 

Hata hivyo aliwataka  wazazi na walezi kuwapeleka watoto shule baadala ya kubaki nao nyumbani huku akisisitiza michango yote itakayokuwa wakichangishwa wazazi na walezi kwaajili ya wanafunzi lazima iwe imepata kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa.


"Mhe Rais Dkt Samia Suluhu ameshatoa fedha kwaajili ya watoto wote wawe wanasoma bila ya ada kwahiyo kusiwe na kisingizio cha wazazi kutoleta wanafunzi kwenye mashule sitaki kusikia michango ambayo haina kichwa wala miguu michango yote inayochangwa kwenye mashule ni lazima iwe na kibali kutoka kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa"Alisema 

Katika hatua nyengine Mkuu huyo wa Mkoa alizipongeza shule za Msingi Bombo na sekondari Old Tanga kwa kuvuka lengo la kusajili wanafunzi kwa mwaka mpya wa masomo 2024 ambapo shule ya msingi Bombo ilitarajia kusajili wanafunzi 70 na imefika 71 huku Old Tanga ambayo ilitarajia kusajili wanafunzi 114 ambapo amesema wataendelea kutembelea na kukagua kuona wanafunzi ambao wamesharipoti .


Akitoa taarifa kuhusu wanafunzi ambao wamesharipoti mkuu wa shule ya Old Tanga Juma Mgunya amesema kuwa shule hiyo awali ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini ikaongezewa wengine 86 wa uhamisho hivyo kufikisha jumala ya wanafunzi 200 ambao wote watapata viti pamoja na madawati pindi wawapo darasani.


"Shule ya Old Tanga ilipangiwa kupokea wanafunzi 114 lakini nmeongezewa wanafunzi wengine wa uhamisho na sasa jumla tuna wanafunzi 200 na mpaka sasa ambao wameshafika ni wanafunzi 109 kati ya wanafunzi 200 ambao nimepangiwa , wanafunzi wote walipangiwa shule ya Old Tanga watakuwa na viti pamoja na meza ambazo zitatosha kutokana na wanafunzi wa kidato cha nne ambao walimaliza mwaka jana" alisema Mwalimu Mgunya.


Kwa upande wake mkuu wa shule ya msingi Bombo Denis Mushi amesema kuwa shule hiyo ilitarajia kusajili wanafuzi 70 ambao wamefanikiwa na kufika 71 kwa upande wa darasa la awali huku darasa la kwanza wakitarajia wanafunzi 120 mpaka sasa wamesajili wanafuzi 121 na hivyo kufikisha wanafuzi 1002 kwa shule nzima kwa mwaka huu wa masomo.


"Shule ya Msingi Bombo iliweka maoteo ya kusajili wanafunzi 70 kwa darasa la awali na mpaka hivi sasa tumesajili wanafunzi 71 na kwa darasa la kwanza tuliweka malengo ya kusajili wanafunzi 120 na mpaka leo tumeshasajoli wanafunzi 121 na hivyo kufikia asilimia 100 ya malengo kwa darasa laawali na la kwanza hivyo baafa ya usajili huu shule itakuwa na jumla ya wanafunzi 1002 wavulana 492 na wasichana 510" alisema Mwalimu Denis


Alisema shule ya msingi Bombo ilipokea kiasi cha shilingi Milion 81, 300, 000 kwaajili ya kutekeleza mradi wa BOOST kujenga vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo ambapo ujenzi huo umekamilika na tayari madarasa yanatumika na hivyo kuondoa changamoto ya msongamano wa wanafunzi katik vyumba vya madarasa.


"Tulipata mradi wa BOOST ambao ulitekelezwa hapa shuleni kwa mwaka 2023 ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa pamoja na matundu ya matatu ya vyoo ujenzi huu ulighalimu kiasi cha fedha Milion 81, 300, 000 kutoka serikali kuu na ujenzi huu umekamilika kwa aailimia 100 tunaishukuru serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na serikali ya mkoa wa Tanga kwani mradi wa BOOST uliotekelezwa umepunguza msongamano mkubwa wa wanagunzi katika vyumba vya madarasa" aliongeza


Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akifundisha baadhi ya wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Bombo alipotembelea shuleni hapo kukagua wanafunzi walisajiliwa tayari kwa kuanza masomo kwa mwaka 2024.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »