SERIKALI YAAHIDI KUKUZA SEKTA YA UTALII KUPITIA NaPA

September 15, 2024

 

Na Mwandishi Wetu, WHMTH, Arusha.

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema miongoni mwa maeneo ya vipaumbele vya Wizara chini ya Mfumo wa Anwani za Makazi ni kushiriki kikamilifu katika kukuza Sekta ya Utalii nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 15 Septemba, 2024 na Bw. Mulembwa Munaku, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara hiyo, wakati akizungumza na washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Jijini Arusha.
Washiriki wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano Bw. Mulembwa Munaku (mwenye koti la Buluu Katikati) na Wataalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi tarehe 15 Septemba, 2024. 
Mafunzo hayo yamefanyika Katika jengo la Kituo cha Utalii Ofisi za Hifadhi ya Ngorongoro, Jijini Arusha.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari yameanza tarehe 12 Septemba, 2024 yakitarajiwa kuhitimishwa tarehe 16 Septemba, 2024, yana lengo la kuwawezesha wataalamu hao kuwa na ujuzi wa kutoa Anwani za Vivutio vya Utalii vilivyopo kwenye Hifadhi ya Ngorongoro.

“Maendeleo ya aina yeyote yanategemea sana utaalamu, hivyo wataalamu mnaopata mafunzo haya mnao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa, adhma ya Serikali ya kukuza utalii inachochewa kupitia matumizi ya Mfumo wa NaPA”, amesema Bw. Munaku na kuongeza kuwa;
“Kupitia zoezi hili, wataalamu mfikirie namna bora ya kuimarisha, kuchochea na kuvutia watalii wa ndani (wananchi) na watalii wa nje kwa ujumla wake”.

Kwa upande wake Mratibu wa Mfumo wa Anwani za Makazi Kitaifa, Mhandisi Jampyon Mbugi, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza wigo wa kutangaza huduma na vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ili kuvutia watalii kutembelea maeneo hayo na hivyo kuongeza pato la Taifa.

SERIKALI YATAKA WANANCHI KUITAMBUA NA KUITUAMINI MIRADI YA MAENDELEO KATIKA MAENEO YAO

September 15, 2024

 


Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imewataka wananchi kuitambua na kuthamini uwekezaji mkubwa wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao na kuacha imani potofu katika utekelezaji wa miradi hiyo, hususani ujenzi wa Skimu za umwagilliaji na barabara kwa madai kuwa maeneo ya miradi ni ya matambiko hivyo isitishwe.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe katika muendelezo wa ziara yake ya kikazi akiwa Mkoani Tabora ambapo alitembelea eneo la mradi wa Umwagiliaji Mwasimbo Igunga, Mwampuli, Mwanzugi na Makomero.

Akiwa katika ziara hiyo ameahidi kurudisha ushirika katika eneo la mradi wa umwagiliaji Mwampuli, kujengwa fensi kuzunguka maeneo ya shamba kwa ajili ya usalama na kukarabati maghala ya mpunga.

Pia, kuanzisha kituo cha zana za kilimo ambacho kitakua na trekta na pawatila za serikali kwa ajili ya wakulima hao.

Waziri Bashe, ameelekeza kujengwa kwa bwawa upya, kujenga mashine za kukoboa mpunga na kukarabati za awali na kuweka mipaka katika eneo la umwagiliaji.

Waziri Bashe, amesema ameshangazwa na hatua ya wananchi wa Nzega vijijini kupinga utekelezaji wa miradi ya skimu za umwagiliaji unaohusisha ujenzi wa miundombinu ya bwawa la Nsembo, ujenzi wa barabara, madaraja madogo na mitaro ya kupitisha maji pembezoni mwa barabara.

Amesema, wananchi hao wanapinga miradi hiyo kwa imani potofu kuwa inapingana na mila na sehemu inapopita miradi hiyo ni maeneo ya matambiko hivyo iondolewe.

“Hii inashangaza sana ndugu zangu wa Nzega vijijini ipo haja sisi serikali kuongeza utoaji elimu, haiwezekani wananchi wanasimama na kudai hawataki barabara, hawataki miundombinu, wanachotaka ni ngoma za asili na matambiko, hivyo hatua zinazochukuliwa na serikali ni kuharibu mila,”amesema waziri Bashe

Akiwa wilayani Igunga Waziri Bashe, ameahidi kutuma timu ya wataalamu kufanya utafiti katika ujenzi wa bwawa la kukusanya maji, kutokana na maji mengi wakati wa mvua katika maeneo hayo, huku akiwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam wa Wizara hiyo watakapo fika kufanya utafiti.


"Ninawaomba ndugu zangu wataalam watakapofika muwape ushirikiano," aliomba.

Ameeleza kuwa bwawa litakapojengwa watawekewa maeneo ya kunyweshea mifugo lengo ni kuhakikisha mifugo haingii mashambani.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Umwagiliaji Raymond Mndolwa,amesema Tume ipo katika hatua za mwisho kuanza utekelezaji wa mradi wa skimu ya Mwamapuli iliyopo katika Kijiji cha Mwanzugi, kata ya Igunga wilaya ya Igunga -Mkoa wa Tabora.

Amesema skimu hiyo ilijengwa kwa mara ya kwanza mwaka 1968 hadi mwaka 1970 lakini bwawa lilikamilika mnamo mwaka 1986 hadi mwaka 1994, mifereji na miundombinu ya shambani ilijengwa na jumla ya hekta 630 zilianza kumwagiliwa Katika mwaka wa fedha 2024/2025.

“Serikali kupitia Tume imedhamiria kuboresha na kuendeleza skimu ya Mwampuli ambapo jumla ya hekta 1,557 zitajengewa miundombinu ya umwagiliaji na kufanya skimu kuwa na jumla ya hekta 2,187,”amesema Mndolwa

Mndolwa ameongeza kuwa mradi huo umeshatangazwa kwa ajili ya kumpata Mkandarasi atakaye fanya shughuli ya ujenzi.

Kwa upande wa mkazi wa eneo hilo, Jilala Shomba, amesema kuwa wapo tayari kwa miradi inayoletwa na serikali katika maeneo yao.



UBALOZI WA TANZANIA NCHINI UHOLANZI WATIA FORA TAMASHA LA MABALOZI MJINI THE HAGUE

September 15, 2024

 

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi  Mhe. Caroline Kitana Chipeta akipongezwa na Meya wa Mji wa The Hague kwa Tanzania kuwa kivutio kikubwa  kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 mjini The Hague.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi  Mhe. Caroline Kitana Chipeta akiwa kavalia mavazi ya asili ya mwanamke wa kimwambao kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 mjini The Hague.

Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi  Mhe. Caroline Kitana Chipeta akipongezwa na Mstahiki Meya wa Mji wa The Hague Mhe. ~Jan Van Hanen kwa Tanzania kuwa kivutio kikubwa  kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 mjini The Hague.


Na Mwandishi Maalumu

UBALOZI  wa Tanzania umetia fora kwenye Tamasha la Mabalozi 2024 (Embassy Festival) nchini Uholanzi lililovutia watazamaji zaidi ya 50,000 wikiendi iliyopita mjini The Hague.

 

Idadi hiyo ya wahudhuriaji nkatika Tamasha hilo ni pamoja na makumi ya wana Diaspora wa Tanzania waishio nchini humo pamoja na wawekezaji wakubwa kutoka Tanzania kama vile PetroBas NL.

 

“Tamasha hilo ni fursa ya kipekee kuonyesha utajiri wa utamaduni wa Tanzania, nasi nafasi hiyo hatukuipoteza hata kidogo,” Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi Mhe.Caroline Kitana Chipeta amesema.

 

Balozi Chipeta amesema fursa zilizojitokeza kwenya tamasha hilo ni kuanzia kukuza utalii na lugha ya Kiswahili hadi mchanganyiko wa mitindo ya zamani na ya kisasa, ambapo Tanzania iliibuka kuwa kivutia kikubwa.

 

Amesema Banda la Tanzania, likiwa na vyakula vya kuvutia na vifaa vya kitamaduni, lilikuwa kivutio kikubwa kiasi ya kwamba  Mstahiki Meya wa The Hague, Jan Van Zanen, alifika na kulisifia huku akiongeza heshima zaidi ya Tanzania kwenye tukio hilo.

 

“Ujio wa Meya Zanen  bandani kwetu kunaonyesha jinsi uwepo wa kitamaduni wa Tanzania ulivyothaminiwa sana huko The Hague”, amesema Balozi Chipeta

 

Katika tamasha hilo Tanzania ilifanya onyesho la mitindo na mbunifu wa Kitanzania la kuvutia sana, hasa kwa kuchanganya mavazi ya zamani na ya sasa ambako kulileta athari kubwa.

 

Balozi Chipets, ambaye yeye mwenyewe alishiriki akiwa kavalia vazi la mwanamke wa kimwambao la khanga na baibui na kushangiliwa sana, anasema, onesho hilo pia lilikuwa ni njia bora ya kuendeleza tamaduni za jadi huku zikifanywa ziwe za kisasa.

 

 

Banda la Tanzania pia lilikuwa kivutio cha pekee hasa kwa kucheza muziki pendwa wa Bongo Fleva ambapo kila aliyepita alifurahia, hasa hasa ilipopigwa ngoma ya Coma Cava ya Diamond Platinumz ambaye Septemba 30, 2024 atafanya onesho jijini Amtserdam.

TUVUMILIANE NA KUHESHIMIANA KAMA WATANZANIA - DKT. BITEKO

September 15, 2024

 







📌 Mamia ya Wakatoliki Wamiminika Uwanja wa Uhuru Kongamano la Ekaristi Takatifu

📌 Watanzania Wahimizwa Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa


Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amewaasa Watanzania kuishi kwa kuvumiliana, kuheshimiana na kupendana kama ilivyoagizwa na vitabu vya Mungu.

Dkt. Biteko amesema hayo leo Septemba 15, 2024 katika Kongamano la Tano la Ekaristi Takatifu Kitaifa lililofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaaam.

“ Wote tuliokuja hapa tumesikia mahubiri mazuri, tumehubiriwa kuwa wamoja zaidi tukavimiliane zaidi na kuheshimiana kama Watanzania wamoja. Kuwa na mawazo tofauti kusitufanye tugawanyike Ekaristi Takatifu hii itufanye tuwe wamoja,” amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza “ Tuwafundishe jamii tuliyonayo kuwa na huruma kwa watu wote wanaohitaji na muhimu zaidi kuwa na huruma na taifa letu la Tanzania.”

Akizungumzia kaulimbiu ya Kongamano hilo inayosema “Udugu Kuponya Ulimwengu, Ninyi Nyote ni Ndugu”, Dkt. Biteko amesema kuwa kauli mbiu hiyo ni muhimu na inawaunganisha watu pamoja.

Dkt. Biteko ameongeza “Tunapotoka hapa tuwafundishe watu, tuwe wapya Ekaristi Takatifu imetuagiza tuishi upya.

Aidha, Dkt. Biteko amewahimiza Watanzania kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Serikali za Mitaa utakofanyika Novemba 27, 2024 kwa kuchagua viongozi kulinga na sifa zao watakaosaidia kuleta maendeleo nchini.

Akihubiri katika misa takatifu wakati wa Kongamano hilo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Wolfgang Pisa, amesema kuwa siku hiyo ni ya kuhitimisha Jubilei ya miaka 50 ya Jumuiya Ndogondogo katika majimbo yote nchini.

Askofu Pisa amesema kuwa kwa miaka mingi nchini Jumuiya Ndogondogo zimetumika kama chombo cha kuwafikia waumini wote na kuwa Ekaristi Takatifu tu ndio kiunganisho cha wakristo.

“ Hii ni sakramenti ya upendo hivyo tusibaguane kwa itikadi, rangi wala sababu zingine kwa kuwa sote tuna Mungu mmoja. Ndugu zangu twende katika sakramenti hii katika hali isiyo na dhambi, tumuombe Mungu sakramenti hii itubadilishe tuwe wapya.” Amesisitiza Askofu Pisa.

Aidha, Askofu Pisa amewashukuru waamini wa kanisa hilo kutoka majimbo mbalimbali nchini kwa kushiriki Kongamano hilo la Ekaristi Takatifu na kusema kuwa baada ya kulihitimisha Kongamano hilo la tano lilifofanyika kwa siku nne litakutana tena miaka minne ijayo katika Jimbo Kuu la Arusha.

Akitoa salama za Baba Mtakatifu, Balozi wa Vatican nchini Tanzania Askofu Mkuu Angelo Accattino amesema kuwa Kongamano hilo limeeleza umuhimu wa Ekaristi Takatifu kama kiini cha imani yao.

“Ekaristi inatuunganisha na kristo na ndugu zetu katika imani Ekaristi ina imarisha upendo wetu kwa Mungu. Naipongeza Serikali kwa kufanya matukio kama haya kwa uhuru na amani” Amesema Askofu Accattino.

Kongamano hilo limekonga nyoyo za maelfu ya waumini wa Kanisa Katoliki kutoka maeneno mbalimbali nchi nzima limehudhuriwa na mamia ya viongozi wa dini wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa.

Ambalo limehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent Bashungwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe. Albert Chalamila.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Makinda, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emannuel Nchimbi na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Tundu Lissu, Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.

MSIGWA AIPONGEZA TBS KWA KUHAMASISHA MICHEZO MAENEO YA KAZI

September 15, 2024

 



NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KATIBU Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amezitaka taasisi mbalimbali za serikali kushiriki na kufanya mabonanza ya michezo ambapo itasaidia kuimarisha afya za wafanyakazi na kuleta manufaa kwa taifa kwa kuongeza idadi ya wachezaji na wawakilishi katika mashindano ya kimataifa.


Rai hiyo imetolewa Septemba14,2024 Jijini Dar es salaam alipokuwa katika Bonanza la michezo la watumishi lililoandaliwa na Shirika la viwango Tanzania (TBS).


Msigwa ameipongeza TBS kwa kuunga juhudi za Serikali ya awamu ya sita kwa kuhamasisha michezo maeneo ya kazi kwa kutengeneza bajeti na kuruhusu wafanya kazi kushiriki katika michezo ili kuimarisha afya na kujenga mahusiano mazuri kazini jambo ambalo huoongeza ubunifu na ufanisi maeneo ya kazi.


Ameongeza kwa kuiasa Menejimenti ya TBS kutenga bajeti ya kujenga viwanja bora maeneo ya kazi ili kuwawekea wafanyakazi mazingira bora wakati wa kushiriki michezo mbali mbali.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi TBS Prof. Othman Chande amesema walianzisha Bonanza hilo miaka mitano iliyopita ambapo limelenga kuimarisha afya za wafanyakazi pamoja na kujenga umoja.


"Wachezaji wanacheza kama timu mbili tofauti lakini ni walewale wakishamaliza mchezo wanaenda pamoja inaongeza urafiki". Amesema


Aidha Prof.Chande ameeleza kuwa mashindano hayo ya mabonanza yatachangia kuwa na machaguo mengi ya wachezaji watakao wakilisha katika mashindano ya kimataifa.


Nae Mwenyekiti wa Michezo Shirika la viwango Tanzania (TBS) Nyabutwenza Methusela ameeleza faida za bonanza hilo ambapo amesema kuwa linasaidia watumishi kuondokana na changamoto ya afya ya akili kwa kujikita zaidi katika michezo ambayo inawaondolea msongo wa mawazo na kuongeza ufanisi wanaporudi kufanya kazi.


"Kupitia michezo afya ya akili na mwili inaboreshwa, wafanyakazi wanakuwa wachapakazi kwasababu wameboresha afya zao za akili pamoja na mwili". Nyabutwenza ameeleza.



WAZIRI MAVUNDE AIPONGEZA TUME YA MADINI KWA KUVUNJA REKODI YA UKUSANYAJI WA MAPATO

September 15, 2024
Waziri wa Madini Anthony Mavunde akizungumza leo wakati akifungua kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Madini Jijini Tanga 

Naibu Waziri wa Madini Dkt Steven Kiruswa akizungumza wakati wa kikao hiho
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini Mhandisi Yahaya Samamba akizungumza wakati wa kikao kazi hicho
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Balozi Batilda Burian akizungumza



Na Oscar Assenga,TANGA

WAZIRI wa Madini Anthony Mavunde ameipongeza Tume ya Madini kwa kuvunja rekodi kukusanya kiasi cha Sh Bilioni 196 kwa kipindi cha siku 75 huku akieleza jambo hilo ni kubwa na inaonyesha wamedhamiria kuifanya sekta ya madini inachangia kwenye uchumi wa nchini.

Mavunde aliyasema hayo leo Jijini Tanga wakati akifungua kikao kazi na Menejimenti ya Tume ya Madini Jijini Tanga ambapo alisema kiwango hicho kimepokelewa mpaka leo 15 Septemba ndani ya miezi miwili ya mwaka huu na hilo linatokana na .

Alisema kiwango hicho kimeifanya kuvunja rekodi ya makusanyo ilihali mwaka 2015/2016 ilichukua mwaka mzima kukusanya Bilioni 161 lakini leo ndani ya siku 75 tume hiyo imeshakusanya kiasi hicho na hivyo kuvunja rekodi kwani waliojiwekea makusanyo ya Bilioni 60 mpaka Bilioni 65 kwa kila miezi na mwili iliyopita mmekusanya Bilioni 83 kila mwezi mmevuka malengo yao.

“Niwatie moyo na wakikaza buti na kuendelea na usimamizi huo mzuri na makusanyo wakifika mwakani mwezi wa saba watakuwa mmeandika historia kubwa”Alisema

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde amewataka maafisa madini wakazi wa mikoa kuhakikisha wanashughulikia migogoro kwenye maeneo yao kwa haraka inapojitokeza badala ya kusubiri mpaka wafike viongozi wakubwa ikiwemo Waziri.

Alisema haiwezekani wao wapo kwenye mikoa na wanashindwa kutatua migogoro iliyopo hivyo wabadilike wahakikishe wanaishughulia na utatuzi wake unapatikana haraka bila kumuonea mtu.

Alisema anajisikia vibaya kuona mgogoro inapotokea mpaka aende waziri au Naibu Waziri wakati wapo maafisa madini wakazi mpaka umshinde ndio uvuke uende ngazi lakini kazi yenu hya kwanza ni utatuzi wa migogoro labda mniembie nyie ni sehemu ya migogoro lakini kama sio sehemu ya migogoro tatueni migogoro,

“Niwaambieni kipimo chenu cha kazi kitakuwa ni namna mnavyotatua migogoro tatueni na sio mpaka msubiri ufike hatua ya juu anzeni nao lakini mtatue migogoro katika haki asionewe mtu simamieni haki ndugu zangu”Alisema Waziri Mavunde

Udhibiti wa Utoroshwaji wa Madini

WAZIRI Mavunde aliwataka maafisa hao kuhakikisha wanadhibiti utoroshwaji wa madini katika maeneo yao hususani ile ya mipakani

“Mmeona hivi karibuni kuna kesi nyingi sana zinapelekwa mahakamani na juzi tumewakamata watu Bandari Dar na kilo 15 za dhahabu na tumezitaifisha ela dhahabu na wanakwenda mahakamani,huko kwenye maeneo yenu hakikisheni mnashirikiana kwenye task force kudhibiti hili lisitokee”Alisema Waziri Mavunde

Aidha Waziri Mavunde aliutaja Mkoa wa Madini wa Kahama ndio unaongoza kwa shughuli za za utoroshaji wa madini na mbinu hivi sasa zimebadilika wanasikie wale ambao wanakwenda kuuziana kwenye mashine za Mpunga ambapo alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo kuhakikisha anaimarisha eneo hilo.

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde amewataka maafisa madini wakazi wa mikoa kuhakikisha wanashughulikia migogoro kwenye maeneo yao kwa haraka inapojitokeza badala ya kusubiri mpaka wafike viongozi wakubwa ikiwemo Waziri.

Mavunde alitoa agizo hilo leo Jijini Tanga ambapo alisema haiwezekani wao wapo kwenye mikoa na wanashindwa kutatua migogoro iliyopo hivyo wabadilike wahakikishe wanaishughulia na utatuzi wake unapatikana haraka bila kumuonea mtu.

Alisema anajisikia vibaya kuona mgogoro inapotokea mpaka aende waziri au Naibu Waziri wakati wapo maafisa madini wakazi mpaka umshinde ndio uvuke uende ngazi lakini kazi yenu hya kwanza ni utatuzi wa migogoro labda mniembie nyie ni sehemu ya migogoro lakini kama sio sehemu ya migogoro tatueni migogoro,

“Niwaambieni kipimo chenu cha kazi kitakuwa ni namna mnavyotatua migogoro tatueni na sio mpaka msubiri ufike hatua ya juu anzeni nao lakini mtatue migogoro katika haki asionewe mtu simamieni haki ndugu zangu”Alisema Waziri Mavunde

Udhibiti wa Utoroshwaji wa Madini

WAZIRI Mavunde aliwataka maafisa hao kuhakikisha wanadhibiti utoroshwaji wa madini katika maeneo yao hususani ile ya mipakani

“Mmeona hivi karibuni kuna kesi nyingi sana zinapelekwa mahakamani na juzi tumewakamata watu Bandari Dar na kilo 15 za dhahabu na tumezitaifisha ela dhahabu na wanakwenda mahakamani,huko kwenye maeneo yenu hakikisheni mnashirikiana kwenye task force kudhibiti hili lisitokee”Alisema Waziri Mavunde

Aidha Waziri Mavunde aliutaja Mkoa wa Madini wa Kahama ndio unaongoza kwa shughuli za za utoroshaji wa madini na mbinu hivi sasa zimebadilika wanasikie wale ambao wanakwenda kuuziana kwenye mashine za Mpunga ambapo alimtaka Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo kuhakikisha anaimarisha eneo hilo.



“Lakini pia nimemwambia Katibu Mkuu waifanye Kahama kama Kanda Maalumu kwa maana dhahabu nyingi inatoroshewa kupitia Kahama nimekuona RMO mara mbili mara tatu mnatoka mnakamata endeleee na mikoa mingine hasa mikoa ya Mipakani”Alisema Waziri huyo.

Waziri huyo aliwataka maafisa hao kila mmoja katika eneo lake ahakikishe anakuwa sehemu ya udhibti wa utoroshaji wa madini kwa maana utoroshwaji huo unasababisha kupoteza mapato mengi.

Hata hivyo Waziri huyo aliitaka Ofisi ya Kamishna wa Madini kushirikiana na RMO kuwalea wachimbaji wadogo na kuwaendeleza katibu mkuu pale wizara wawekezaji wakubwa wana meneja wake ndani ya wizara wa kuyasimamia katibu mkuu kupitia Ofisi ya Kamishna natoa maelekezo tengenezeni utaratibu kushirikiana na RMO kuwaibua watanzania wawekezaji wa sekta ya madini kupitia ofisi ya Kamishna wawelee nao wagraduate kutokana na kwamba hivi sasa wenyewe hawana muangalizi.

Alisema ili siku moja waweze kutengeneza mabilioni wengi kupitia wachimbaji wadogo hivyo wakikaa nao na kuwasaidia kama wanavikwazo waone namna ya kuyatatua ili kuweza kuongeza mapato.

Katika hatua nyengine Waziri Mavunde aliwataka kuhakikisha wanadhibiti upotevu wa mapato waende wakazibe mianya na makusanyo yaweze kuongezeke huku akieleza hiyo ni sehemu ya kazi yako ya msingi.

“RMOs kila mtu amewekewa malengo ya kuwafikia kwa mwaka wa fedha huu kama unahisi kwako unashindwa kufikia malengo kwa jambo ambalo halihusiani na wewe ni tatizo la kimfumo,kimundo lipo nje ya uwezwa

WAZIRI MAVUNDE AZINDUA UMOJA WA WASAMBAZAJI WA SEKTA YA MADINI

September 14, 2024

 

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akizungumza wakati akizindua chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA) jiji Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), Peter Kumalilwa akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa chama chao.
Meneja wa Barrick Tanzania, Melkiory Ngido akizungumza machache.
Mjumbe wa Bodi ya TPSF, Octavian Mshiu.
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akifuatilia jambo.
Mwakilishi wa Kituo cha Uwekezaji akizungumza machache.
Wadau mbalimbali sekta ya Madini wakifuatilia uzinduzi huo.
Viongozi wa TAMISA wakizungumza Mhe. Mavunde.
Wadau wa Sekta ya madini wakizungumza na Mhe. Mavunde.

Na Mwandishi Wetu 

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amezindua chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), shirika jipya lililoanzishwa ili kusaidia wasambazaji wa sekta hiyo.

TAMISA imeanzishwa ili kutetea maslahi ya wasambazaji katika sekta ya madini, kuboresha maudhui ya ndani, kuimarisha mazingira ya biashara, kukuza utamaduni wa uvumbuzi, ushirikiano kati ya wadau na uendelevu wa biashara ndani ya mfumo wa maudhui ya ndani.

Dhamira ya TAMISA ni kuimarisha sekta ya ugavi na huduma za madini kwa kuwapatia wanachama wake fursa muhimu, kutetea maslahi yao, na kukuza utamaduni wa ubunifu na uendelevu.

Akizindua TAMISA, Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ambaye alikuwa mgeni rasmi, amepongeza dhamira ya TAMISA na kuzingatia sera za maudhui ya ndani. “Kuunganisha Watanzania katika sekta ya madini kupitia maudhui ya ndani ni muhimu kwa ukuaji endelevu na kutaiwezesha serikali kutatua changamoto za mahudhui ya ndani kupitia umoja huo ambao ndio sauti rasmi ya pamoja ya wasambazaji wa sekta madini.

Uwepo wa TAMISA utachagiza azma ya serikali katika kuhakikisha kuwa utajiri wetu wa madini unawanufaisha wananchi wetu moja kwa moja na kukuza maendeleo ya kiuchumi,” alisema Mhe. Mavunde.

Pia ameiangazia maono mapana ya serikali: “Serikali inataka kuona makampuni ya Tanzania yakijitosa katika kuanzisha viwanda na kutengeneza bidhaa muhimu katika kuchimba madini. Serikali inatoa kipaumbele kipaumbele katika uwekezaji wenye tija kupitia ajira za ndani na matumizi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini, kwani tunalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kupunguza utegemezi wa pembejeo za nje. Juhudi hizi zitachangia sana katika kuleta ajira, ukuzaji wa ujuzi, na ukuaji wa tasnia zinazohusiana, na hivyo kuunganisha sekta ya madini kwa undani zaidi katika uchumi wa ndani.

Aidha Waziri Mavunde amefurahishwa na uzinduzi wa taasisi hiyo iliyoko chini ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania akisema kwamba sasa wasambazaji wa sekta ya madini wana sauti rasmi katika masuala muhimu jambo litakalohakikisha kwamba haki zao zinalindwa na kuimarishwa kupitia uboreshaji wa mazingira ya biashara na utatuzi wa chan

Aidha Waziri Mavunde amefurahishwa na uzinduzi wa taasisi hiyo iliyoko chini ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania akisema kwamba sasa wasambazaji wa sekta ya madini wana sauti rasmi katika masuala muhimu jambo litakalohakikisha kwamba haki zao zinalindwa na kuimarishwa kupitia uboreshaji wa mazingira ya biashara na utatuzi wa changamoto zao.

Awali Mwenyekiti wa TAMISA, Peter Kumalilwa alifafanua kwamba TAMISA imeanzishwa ili kuwawezesha na kuwaleta pamoja wasambazaji wa sekta ya madini, kutetea maslahi yao na kuimarisha mazingira ya biashara. Malengo yetu makuu ni pamoja na kutetea wasambazaji wa sekta ya madini, kuboresha uwezeshaji wa biashara, kutetea haki za wasambazaji, na kuendeleza utafiti na ukuaji wa teknolojia. Tunalenga kuendesha uvumbuzi na uendelevu ili kuweka wanachama wetu kama viongozi katika tasnia.

“Sekta ya madini nchini Tanzania kwa muda mrefu imekuwa nguzo ya uchumi wetu. Hata hivyo, ili kutumia kweli uwezo wa sekta hii, ni lazima tupite zaidi ya uchimbaji; ni lazima tuhakikishe kuwa manufaa ya uchimbaji madini yanaenea hadi kwenye uchumi mpana kupitia uendelezaji na uwezeshaji wa mnyororo wa ugavi wa ndani. Ndio maana TAMISA ilizaliwa: ili kutetea ukuaji na mafanikio ya wasambazaji wa sekta ya madini," amesema Kumalilwa.