NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WANUFAIKA
wa fidia inayotolewa na WCF, wametoa ya ‘moyoni’ mbele ya wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari, kwa kile walichokiita Mfuko huo umewafuta machozi.
Wakitoa
ushuhuda Novemba 2, 2023, katika kikao kazi baina ya Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) na Wahariri wa vyombo vya habari, kuelezea utekelezaji wa
majukumu na mafanikio ya Mfuko huo, miaka 8 tangu kuanzishwa kwake.
Beauty
Jackson Letema, ni mnufaika wa WCF, yeye ni mama mjane ambaye alifiwa na mumewe
katika ajali wakati akitekeleza majukumu ya mwajiri wake.
“Namshukuru
sana Mwenyezi Mungu, lakini pia naishukuru WCF, mume wangu alipofariki
aliniacha na watoto watatu na ujauzito, WCF walianza kunihudumia
mimi na watoto wangu hao watatu na kisha huyu mwingine, Mimi sikuwa na kazi yoyote ya kufanya, WCF wanatuhudumia
mimi na watoto, tunavaa, tunakula na pia watoto wangu wanasoma bila shaka
yoyote, kwakweli wamenifuta machozi.” Alisema
Kutokana
na manufaa anayoyapata kutoka WCF, Mnufaika huyo aliwahimiza waajiri kujisajili
na mfuko ili wafanyakazi wanapopatwa na madhila wakiwa kazini, basi Mfuko
utakuwa mfariji wao.
“Wito
wangu kwa waajiri, WCF ni mfuko wenye faida sana, kama mimi mume wangu
alivyofariki na mwajiri wake angekuwa hajajisajili WCF, maisha yangekuaje? Natoa wito kwa waajiri
wajiunge na WCF.” Alisisitiza Beauty.
Mnufaika
mwingine ni Halima Sheikh, wakati akitekelza jukumu lake kama dereva wa bus la
abiria, Super Feo, alikatika mkono baada ya bus alilokuwa akiliendesha
kupinduka.
“Baada
ya kupoteza mkono na kupata ulemavu wa kudumu, WCF imekuwa ikinilipa fidia kila
mwezi, malipo yananisaidia mimi na familia yangu, nimeambiwa nitalipwa maisha
yangu yote, hakika nafarijika sana.” Alisema.
“Kwa
kifupi naishukuru sana Serikali kwa kuanzisha WCF, Mfuko una manufaa makubwa
sana, ninajitegeema asilimia 100, namshukuru Mkurugenzi Mkuu wa WCF na timu yake, Mfuko umenipatia matibabu vizuri sana hadi kupona, maisha yangu
yanaendelea.” Alisema Mnufaika mwingine, Bw. Hassan Sima Jambau, aliyekuwa
mtumishi wa Televisheni ya Taifa, TBC.
Beauty Jackson Letema, mnufaika wa WCF, akitoa ushuhuda mbele ya Waandishi wa habari
Bi. Halima Sheikh
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma (kushoto), akiteta bjambo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Bw. Thobia Makoba.
Mwandishi wa habari mwandamizi na Mhariri, Bw. Joe Nakajumo akiwa mwenye hisia wakati akisikilzia ushuhuda wa wanufaika wa fuidia.
Baadhi ya washiriki
EmoticonEmoticon