Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhamani kulia akionyeshwa maeneo mbalimbali ya Hospitali ya wilaya ya Pangani na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo wakati apofanya ziara ya kushtukiza
MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rajab Abdurhamani amekerwa
na wizi wa misumari katika Hospitali ya wilaya aya Pangani Mkoani Tanga huku
akiliagiza Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi na watakaowabaini walihusika
kwenye tukio hilo hatua kali za kisheria zichukuliwe.
Hayo yalibainika wakati wa ziara yake wilayani hapa ya
kushtukiza iliyokuwa na lengo la kufuatilia maagizo yake aliyoyatoa wakati wa
ziara yake hivi karibuni ambapo alisema pamoja na hayo wachukuliwe hatua za
kinidhamu na sionewe mtu huku akisisitiza aliyetia mkono wake kuiba vifaa hivyo
ashughulikiwe.
Akiwa Hospitalini hapo baada ya kukagua ukarabati wa Hospitali
hiyo ambao unagharimu milioni 900 ndipo alipoelezwa wizi huo na Mkuu wa wilaya
ya Pangani Zainabu Abdallah wakati akipopata nafasi ya kuzungumza.
Mwenyekiti huyo alisema lazima washughulikiwe kwa kuchukuliwa
hatua kali ili iweze fundishwa kwa watu wengine wenye tabia za namna hivyo
maanaa zikivumiliwa vitakwamisha juhudi za kimaendeleo ambazo zinafanywa na
Serikali.
“Kwa maana tutawapa lawama ndugu zetu waliopewa nafasi ya
kusimamia miradi ikiwemo Mkurugenzi na Mkuu wa wilaya na katika hili nikutake Mkuu
wa wilaya usicheke na mtu na ukiacha hilo ninazo taarifa nyegine nimeweka watu
wangu nitakapozithibitisha nitachukua hatua kuna vifaa viliibwa hapa hospitali
lakini jana usiku baada ya kusikia ninakuja vimerudishwa watu hawaogopi wala
hawana haya hilo halikubaliki”Alisema
Mwenyekiti huyo pia aliwapongeza uongozi wa Hospitali hiyo kwa kusimamia
mradi huo wa ujenzi wa Hospitali huku akionyesha kuridhika nao kwa kiasi
kikubwa kwa sababu thamani ya fedhana kinachoonekana kinaendana.
“Niwaombe wananchi wenzangu lazima tumhurumie Rais Wetu Dkt
Samia Suluhu kwa maana anahangaika usiku na mchana muda wowote siku zote halali
kwa sababu ya kuwasaidia Watanzania kuwaondolea adha zinazowakabili pia mbunge
wetu anapambana sana kujenga hoja kwamba hospitali yetu na hapa Hospitalini
ameleta Milioni 900 kwa ajili ya ukarabati hivyo tusiwakatishe tamaa viongozi
wetu”Alisema
Aidha alisema kwa maana wakati miradi inapotekelezwa zinatumika
fedha nyingi ambazo zimeletwa kwenye wilaya yenu katika utekelezaji wa miradi
hiyo lazima wananchi wawe waaminifu ili lengo liweze kutimia lakini inapojitokeza
watu wanaiba misumari inakwamisha juhudi hizo.
Hata hivyo aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kuendelea kuwa
wabunifu katika maeneo yao ikiwemo kuendelea kumuunga mkono Rais Dkt Samia Suluhu
anayejali matatizo ya wananchi anaowaongoza.
Mwenyekiti huyo aliwataka wananachi hao kuhakikisha mwaka 2025 hawana
Rais mwengine zaidi ya Dkt Samia Suluhu mambo anayoyafanya ni makubwa ya
kimaendeleo watapata muda kwenda kuyaelezea.
Awali akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Pangani
Zainabu Abdallah alimueleza Mwenyekiti huyo kwamba Serikali ya Rais Dkt Samia
Suluhu aliwapelekea million 900 kwa ajili ya ukarabati wa Hospitali ya wilaya
hiyo huku akieleza wakati anapofanya ziara na kamati ya usalama kukagua ujenzi
huo ndipo walipobaini uwepo wa wizi huo.
Alisema baada ya kulibaini hilo alimuelekeza Mganga Mfawidhi wa
Hospitali ya wilaya hiyo (DMO) aweze kuchukua hatua kutokana na kupotea magunia
mawili ya misumari lakini hawakuripoti katika Jeshi la Polisi ili uchunguzi
ufanyie na hatua zichukuliwe.
“Lakini nilitoe maelekezo kwa DMO achukua hatua ili sheria
ichukue mkono wake lakini niliwataka lega ya vifaa vyote vinavyongia na kutoka
vya zamani na vipya na hali yake ipoje bahati nzuri DMO aliniandikia taarifa na
nilimueleza aende kufungua kesi na kesi tayari imeshafunguliwa kituo cha Polisi
na uchunguzi unaendelea na hivi vilipotea wakati wanahamisha vifaa kutoka
sehemu waliokuwa wamehifadhi kwenye stoo mpya”Alisema
Mwisho.
EmoticonEmoticon