TANZANIA MWENYEJI WA MKUTANO WA JUKWAA LA MAJAJI WAKUU UKANDA WA NCHI ZA KUSINI NA MASHARIKI MWA AFRIKA

October 20, 2023

 Pamela Mollel, Arusha


Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano mkuu wa jukwaa la majaji wakuu ukanda wa nchi za kusini na Mashariki mwa Afrika(SEAJAA) utakaofanyika oktoba 23 hadi 27 jijini Arusha

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mwenyekiti wa Chama cha hicho, Profesa Elisante ole Gabriel ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, amesema maandalizi ya kikao cha watendaji hao yanaendelea vizur  na kuwa Mkutano huo utakaofunguliwa na Rais Dkt Samia Hassan Suluhu.

Profesa Gabriel amesema katika  kikao hicho tayari nchi 13 zimejiunga na chama hicho huku jitihada za nchi nyingine tatu  kujiunga na chama hicho zikiendelea na badae idadi ya wanachama wengine itaongezeka kufika Afrika nzima

Aliongeza kuwa malengo ya chama hicho ni kubadilishana uzoefu katika nchi wanachama ikiwemo jinsi gani wakuu wa mahakama wanavyoendesha shughuli za mahakama

Amesema kikao kazi hicho kitajadili mambo mbalimbali kwani watendaji wakuu wanawashauri majaji wakuu katika masuala ya miundombinu, rasilimali za watu na masuala ya fedha

Pia kitakuwa na ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho, mikakati ya masuala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »