Na Oscar Assenga, TANGA.
MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala watakatiwa huduma hiyo.
Kindamba aliyasema hayo wakati wa ziara yake ya kutembelea Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira (Tanga Uwasa) kukagua vyanzo vya maji na kuona upanuzi wa eneo Mowe ambalo maji yanasafirishwa kwa ajili ya matumizi katika Mkoa na Jiji la Tanga
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba pamoja na kwamba Tanga Uwasa wamekuwa wakishirikiana na vyombo hivyo lazima wahakikishe wanalipa haraka madeni hayo kwa wale ambao ni wadaiwa sugu ambao hawaonyeshi jitihada za kuyalipa.
“Niwapongeze Tanga Uwasa kwa kufanya kazi nzuri ya kutoa huduma lakini nivitake amevitaka vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma wanaodaiwa madeni na Tanga Uwasa kulipa madeni hayo haraka kwa sababu itafikia mahala mtasitishiwa huduma hii”Alisema RC Kindamba.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa namna anavyoendelea kugusa maisha ya wananchi wa kawaida kwa maana ukienda kwenye maji,afya na elimu utamkuta walichokwenda kushuhudia ni kitu kikubwa sana ambapo Tanga Uwasa wameweza kuongeza uwezo wa kusambaza maji kutoka lita Milioni 30,000,000 mpaka lita milioni 45,000,000.
Hata hivyo alisema mpango wa muda ujao na muda wa kati ni kupanua uwezo wa kuzalisha lita milioni 60 na hilo litawezekana kutokana na mipango waliojiwekea watakuja kutangaza kwenye masuala la hati fungani ambazo zitasaidia kupatikana mtaji wa kuweza kupanua zaidi mradi wa maji kwenye mkoa na Jiji la Tanga.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly alisema wanashirikiana vizuri na taasisi za ulinzi na usalama kutoa huduma zao kwani wao wanatoa huduma kwao.
Mhandisi Hilly alisema wakati mwengine kutokana na sababu mbalimbali kuna kukwama kwenye malipo na kwa sasa wanazidai taasisi hizo takribani Bilioni 1.8 wanashuruku wameanza kupunguza kidogo.
“Kama mlisikiliza Bunge mara ya mwisho tulikuwa tunadai Bilioni 2.4 hivyo wamejitahidi kupunguza Milioni 400 karibia 500 hivyo tunaomba wapunguze deni hilo kutokana na deni ni kubwa na linatukwamisha mambo mengi ya utoaji huduma,ununuaji madawa na ulipaji umeme”Alisema Mkurugenzi huyo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiit wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tanga Uwasa Dkt Ally Fungo alisema kwamba madeni yamekuwa yakiwasumbua sana hususani vyombo vya Serikali na Taasisi za Umma.
“Kwa kweli ni wateja wetu wazuri lakini madeni yamekaa muda mrefu na tuliona tukushirikishe ili uweze kutusaidia Mkuu wa Mkoa na uwasaidia wenzetu wanadai wanapodai walipwe ili waweze kutulipa”Alisema Dkt Fungo..
EmoticonEmoticon