Shirika la Afya Duniani (WHO) limebainisha kelele kuwa ni mojawapo ya
kisababishi cha madhara katika maisha ya binadamu. Aidha, kwa mujibu wa “European Environmental Agency” (EEA, 2018) kelele zimeainishwa kuwa mojawapo ya visababishi vya vifo vya mapema vya watoto “Pre-mature death” ambapo takwimu zinaonyesha takribani watoto 12,000 hufariki kila Mwaka katika Bara la Ulaya”. Katika nchi yetu changamoto ya kelele zinazozidi viwango vilivyoainishwa na TBS zinatokana na kukua kwa shughuli za kiuchumi na kijamii ikiwemo matumizi yasiyo sahihi ya teknolojia. Kwa siku za hivi karibuni, kelele zimeongezeka kwenye maeneo ya kazi na hivyo kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo kupoteza uwezo wa kusikia, matatizo ya uzazi, kupunguza umakini katika mafunzo, ajali na kupungua uwezo wa kusikilizana. Vyanzo vikuu vya kelele hizi ni kumbi za starehe hasa biashara za vileo (baa), vyombo ya usafiri na usafirishaji (kama magari, ndege na treni), matumizi ya teknolojia zilizopitwa na wakati kwenye viwanda vikubwa na vidogo (Karakana za kuchomelea, ufyatuaji matofali, mashine za kusaga na kukoboa nafaka), majenereta, matangazo ya biashara mitaani, shughuli za ujenzi, nyumba za ibada n.k. |
SHERIA NA SERA ZINAZOONGOZA UDHIBITI WA
KELELE NA MITETEMO
Udhibiti wa kelele na mitetemo nchini unasimamiwa na Sheria mbalimbali
zikiwemo Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya Mwaka 2004 pamoja na
Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Udhibiti wa Kelele na Mitetemo) za
Mwaka 2015; Sheria ya Usalama Kazini ya Mwaka 2003; Sheria ya Afya ya
Jamii ya Mwaka 2009; Sheria ya Jumuiya [Sura ya 337 Marejeo ya 2002];
Sheria ya Baraza la Sanaa la Taifa [Sura 204 Marejeo ya 2002] na Kanuni za
Baraza la Sanaa la Taifa za Mwaka 2018; Sheria ya Ardhi [sura 113 Marejeo ya
Mwaka 2019] na Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 pamoja na Kanuni
zake za Mwaka 2018.
Sheria na Kanuni hizi zimeelekeza shughuli zote zenye madhara zifanyike
mbali na makazi ya watu na hivyo shughuli zenye kelele kufanyika mbali na
makazi ya watu ili kupunguza madhara kwa afya ya binadamu na mazingira.
BARAZA LA HIFADHI NA USIMAMIZI WA MAZINGIRA (NEMC)
Katika kuhakikisha kelele na mitetemo zitokanazo na shughuli mbalimbali
zinadhibitiwa, Baraza litafanya yafuatayo:
a. Kuendelea na ukaguzi wa maeneo ya biashara na kutoa
maelekezo mbalimbali ikiwemo Amri na Ilani za kudhibiti kelele.
b. Kuanisha na kutangaza maeneo ambayo kelele haziruhusiwi
(Noise Control Zone).
c. Kusimamia uanishaji wa ramani za maeneo yenye kelele
zilizopitiliza na kuandaa Mkakati wa udhibiti.
Mwongozo wa Kitaifa wa Udhibiti Kelele na Mitetemo
d. Kufanya tafiti za mara kwa mara kubaini hali ya uchafuzi wa
mazingira utokanao na kelele na mitetemo.
e. Kutoa elimu kwa jamii na maafisa mazingira kuhusu majukumu
yao katika udhibiti wa kelele na mitetemo.
f. Kupokea taarifa za malalamiko yanayohusu kelele na mitetemo.
EmoticonEmoticon