Wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu na Wizara ya Fedha, wakiangalia dagaa walioanikwa katika kichanja cha kienyeji, katika kata ya KILWA Kivinje,wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maeneo yatakayoteleza programu ya KILIMO na UVUVI (AFDP) mkoani Lindi Leo.
Picha ikionesha washiriki wa Kikao cha ugeni kutoka programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) wataalam na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya KILWA,wakati Ujumbe huo ulipotembelea maeneo yatakayoteleza programu hiyo mkoani Lindi
Mtaalamu wa masuala ya Lishe na Jinsia Bi. Irene Mbando, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu akizingumzia namna ambavyo Programu Hiyo itakavyohusisha masuala ya Lishe na jinsia.
Picha ikionesha Dagaa walioanikwa chini, katika kata ya KILWA Kivinje mkoani Lindi.Kulia Bw. Robert Lee mtaalam wa Uvuvi kutoka Mfuko wa Kimataifa wa maendeleo ya Kilimo Duniani (IFAD) akijadili jambo na Bw. Richard Abila mtaalamu wa Ufugaji wa viumbemaji kutoka IFAD.
Mfanya biashara wa dagaa,katika kata ya KILWA kivinje Wilayani KILWA, Mkoani Lindi akianika dagaa katika chanja ya kienyeji, ambapo programu ya kuendeleza Kilimo na uvuvi (AFDP) Itaenda kuwajengea chanja za kisasa.
Na; Mwandishi Wetu - KILWA
IMEELEZWA kuwa, Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi AFDP inategemea kwenda KUBORESHA MAZINGIRA na maisha ya wavuvi wilayani Kilwa Mkoani Lindi.
Hayo yamesemwa mapema Leo tahehe 15 Mei 2023, Mkoani Lindi na Mtaalamu wa masuala ya mazingira wa mradi huo, Mhandisi Erick Isack kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu wakati Ujumbe wa Programu hiyo ulipokuwa katika Ziara ya kikazi Mkoani hapo.
Mhandisi Isack amesema programu hiyo itasaidia kujenga kiwanda Cha kuchakata samaki katika maeneo ya bandari ya uvuvi KILWA Masoko na ghala la kutunzia samaki. Sambamba na hilo programu hiyo pia itaenda kujenga vichanja vya kisasa vya kukaushia dagaa katika kata ya KILWA Kivinje.
Kwa Upande wake mtaalam wa masuala ya Lishe na jinsia Bi. Irene Mmbando alisema, programu itazingatia ushiriki wa jinsia zote ikiwa wanawake watashiriki Kwa asilimia sitini (60%) na Asilimia arobaini (40%) vijana.
Aliongeza Kwa kusema kuwa Mradi huo unalenga kufika kaya laki mbili na sitini ambazo zitahusika katika kilimo, uvuvi na ufugaji wa viumbemaji.
Akizingumzia masuala ya Lishe, mtaalamu huyo Alisema programu hiyo inakwenda kuzingatia maswala ya Lishe katika kaya husika.
Awali akiongea katika mazungumzo hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya KILWA Bw. Eston Mngilangwa alisema, programu hii imezingatia mazingira halisi ya maeneo husika "Kwa upande wangu naona kama Lindi tumependelewa, tumeletewa miradi sita, programu hii tunaipokea Kwa mikono miwili, Tunashukuru sana, tunawahakikishia kuwa Mradi huu utaenda kuleta matokeo chanya, tumeshafanya maandalizi kwenye kila eneo,kama itatokea Kuna mahala tumekosea itakuwa ni suala la uelewa tuu." Alibainisha Mkurugenzi Huyo.
Ujumbe huo kutoka Programu ya kuendeleza Kilimo na Uvuvi, inayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, uliohusisha wataalam kutoka IFAD, Wizara MIFUGO NA UVUVI, FEDHA na Wizara ya Kilimo itaendelea na ziara yake ya kikazi kisiwani Zanzibar wiki hii.
= MWISHO =
EmoticonEmoticon