PSSSF YAPITA "BANDA KWA BANDA" KUWAFIKIA WANACHAMA WAKE KWENYE MAOENSHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

April 27, 2023

 

 

NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID, MOROGORO.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) pamoja na kutoa elimu kwa wanachama na wananchi wanaotembelea banda la Mfuko huo kwenye Maonesho ya Siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, viwanja vya Tumbaku mjini Morogoro, pia unapita “Banda kwa Banda” ili kuwafikia wanachama wake, Afisa Uhusiano Mkuu wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi amesema.

Bw. Njaidi amesema Mfuko unashiriki Maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu na kuwahudumia wanachama wake ambao ni wastaafu lakini pia watumishi wa Umma na Mashirika ambayo Serikali inamiliki hisa asilimia 30.

“Lakini tukumbuke kuwa watumishi walio kwenye viwanja hivi nao pia wanawahudumia wananchi kwenye mabanda yao, hivyo tumeona tugawane majukumu, baadhi yetu wako bandani kutoa elimu na huduma kwa watakaofika na sisi tunapita banda kwa banda kuwahudumia." Alifafanua Bw. Njaidi ambaye alifuatana na Afisa Matekelezo Mwadamizi wa Mfuko huo Bw. Charles Mahanga.

Akifafanua alisema kwakuwa huduma nyingi za Mfuko zinapatikana kiganjani (PSSSF Kiganjani) hivyo ni rahisi kuwapatia elimu kwenye mabanda yao ya jinsi ya kutumia huduma hiyo.

Kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Usalama na Afya mahali pa kazi hufanyika Aprili 28 kila mwaka ambapo Tanzania huungana na mataifa mengine duniani kuiadhimisha siku hii, lengo kubwa ni kuendeleza kampeni za kuhamasisha uwepo wa mazingira salama na yenye kulinda afya za watu katika sehemu za kazi ambapo kauli mbiu ya maadhimisho kwa mwakam huu ni “Mazingira salama na afya ni kanuni na haki ya msingi mahali pa kazi.”.

Afisa Uhusiano Mkuu wa PSSSF Bw. Abdul Njaidi akiwa na Afisa Matekelezo Mwandamizi PSSSF, Charles Mahanga akimkabidhi kipeperushi cha PSSSF Msimamizi Mkuu wa banda la Jeshi la Polisi, Mkaguzi Msaidizi Zuwena Mwita.
Meneja wa PSSSF Kanda ya Masahariki, Bi. Zaida Mahava (kulia) akimuhudumia mwanachama

Bw. Njaidi (kushoto), akitoa elimu kwa maafisa wa polisi.

Banda la NMB
Banda la NSSF
Banda la CRDB
Banda la CRDB
Banda la WCF

Banda la OSHA

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »