KESI ZA DAWA ZA KULEVYA, ULAWITI ZATAJWA KUSHAMIRI TANGA

January 26, 2023
WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi Jijini Tanga wakiwa mmoja ya mabanda yaliyopo katika eneo la Urithi kunakofanyika maadhimisho ya wiki ya Sheria kimkoa 
Wanafunzi kutoka shule za Msingi Jijini Tanga wakipata elimu kwenye Banda la Jeshi la Zimamoto na 
Uokoaji Tanga 

Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi za Jijini
Tanga waliotembelea Banda lao kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa.
Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo akitoa elimu 
AFISA Uchunguzi wa Takukuru Mkoa wa Tanga Khadija Luwongo akitoa elimu kwa mmoja wa wananchi waliofika kwenye banda lao
Mtendaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga Humphrey Paja akipatiwa elimu na Afisa  Uchunguzi wa Takukuru Frank Mapunda   kuhusu namna wanavyofanya shughuli zao kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya rushwa wakati alipotembelea banda lao

Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili wa Kujitegemea Mkoa wa Tanga (TLS) Tumaini Bakari akitoa elimu kwa wanafunzi wa chuo cha Utalii cha Masai kilichopo Jijini Tanga kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa wanapokumbana na vitendo vya ukatili
Mwanasheria wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) mkoa wa Tanga Mwanaidi Kombo akisisitiza jambo


Na Oscar Assenga,TANGA

OFISI ya Taifa Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga imesema kwamba kesi zinazopokelewa kwa wingi mkoani humo ni za biashara ya dawa za kulevya,ukatili wa kijinsia ikiwemo ulawiti na ubakaji.

Hayo yalisemwa leo na Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Taifa ya Mwendesha Mashtaka ya Serikali Mkoani Tanga Lucky Titus Kaguo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule za Sekondari na Msingi za Jijini Tanga waliotembelea Banda lao kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa.

Banda hilo lipo kwenye viwanja vya Urithi Jijini humo ambako kunaendelea maonyesho ya wiki ya Sheria Tanzania huku akieleza mkakati ambao wameupanga kuweza kukabiliana na vitendo hivyo.

Alisema mkakati wa kwanza ni kwamba wanakusudia kuandaa mpango wa kutoa elimu kwa wananchi na wanafunzi juu ya athari ya vitendo hivyo ili kuweza kuibadilisha jamii iondokana navyo.

“Kwa mkoa huu tunapata shida kwenye makosa ya jinai aina mbili madawa ya kulevya na unyanyasaji wa kijinsia ubakaji na ulawiti makosa ambayo yameshamiri sana kwa mkoa wa Tanga “Alisema

Aidha alisema kutokana na uwepo wa hali hiyo wanaandaa mpango wa kuzunguka kwenye shule za msingi na sekondari ikiwemo kukutana na wanafunzi ikiwemo wananchi kuwaeleza iumuhimu wa kutoa taarifa za unyanyasaji unapotokea na wanapoona watu wanauza dawa na wanapata marejesho chanya suala hilo na bado linaendelea kufanyiwa kazi

Hata hivyo alisema kwamba wameshiriki kwenye maonyesho hayo ya wiki ya sheria kutoa elimu kwa wanafunzi na wananchi kwa kutatua matatizo yao na kuwaleta wananchi kuhusu ofisi hizo na kueleza majukumu yao na kutatua matatizo yao.

Alisema pia kuwaeleza ofisi hizo na umuhimu wake katika mashauri wanayopalekwa na wananchi huku wakieleza jitihada za serikali katika kutatua mashauri yake kwa nia ya usuluhihi badala ya njia ya mahakama

Mwisho.

DIWANI AWATAKA KIMAYA AWATAKA WAZAZI,WALEZI KUWAPELEKA WATOTO WAO KITUO CHA SAYANSI STEM PARK CHA JIJINI TANGA

January 21, 2023


Na Oscar Assenga.Tanga

DIWANI wa Kata ya Chumbageni (CCM) Ernest Kimaya amewataka Wazazi na Walezi Jijini Tanga kukitumia kituo hicho cha Sayansi STEM PARK kwa kuwapeleka watoto wao ili waweze kujifunza na kupata Ubunifu wa mambo ya Kisayansi ili baadae waweze kuwa wabunifu wazuri na wenye vipaji kwenye maisha yao.

Aliyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kambi hiyo  Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA wakati wa ufunguzi wa kambi maalumu ya kuwamejengewa Uwezo juu ya Sayansi ya Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo "Janja

Kambi hiyo  maalumu ambayo iliyofadhiliwa na Mashirika ya Club Rotary clubs Tanga , Robotech Labs na Tanzania Open Innovation(TOIO) kwa Ushirikiano wa Jenga Hub chini ya usimamizi wa Project Inspire ambao ndio wasimamizi wa Kituo Cha Sayansi Nchini STEM PARK kilichopo mkoani Tanga.
Alisema uwepo wa kituo hicho katika eneo lake umekuwa na tija kubwa kwani kimekuwa kikitumiwa na wanafunzi na Walimu kujifunza kwa vitendo masomo ya sayansi hivyo kusaidia wanafunzi wanapokuwa wakisoma kwa nadharia shuleni baadae wanapokwenda kwenye kituo hicho wanasoma kwa vitendo na hivyo kuwasaidia kuwa na uelewa mzuri wa mambo wanayofundishwa wakiwa darasani.

“Kwa kweli kituo hiki kinafanya kazi kubwa na nzuri sana hivyo niwapongeze kwani mafunzo mnayotoa vijana wetu ni mazuri na yanawasaidia namna ya kutumia ujuzi walioupata na hivyo kuepukana na kukaa vijiweni ambako wengine wanajikuta wakitumia dawa za kulevya “Alisema

Aidha alisema kwamba kazi inayofanywa na kituo hicho ni kubwa kwa sababu mafunzo waliyoyapata yanakwenda kuwasaidia kuwa wabunifu wazuri zaidi huku akiwataka pia kuyatumia vizuri kwa ajili ya tija zaidi.

Alisema kwamba mazoezi ambayo wamewafundishwa vijana hao watengeneze utaratibu mzuri baada ya wa kutoka hapo baadae waende kwenye uhalisi wakiondoka wanaondoka watakuwa kitu ambacho wanacho baada ya hapo vijana watakuwa na ujuzi mkubwa wa kuwatoa kwenye fikra.

Alieleza kwamba itawatoa kwenye fikra ambazo sio nzuri na badala yake watakuwa wabunifu na kuondokana na vijana wavuta bangi, madawa ya kulevya maana watakuwa wamejitambua na wanaamini wanafunzi wanashika sana wakiwa na umri mdogo.

Awali akielezea kambi hiyo Meneja wa Kituo cha Meneja wa Kituo Cha Sayansi STEM PARK TANGA  Max George alisema  Kituo hicho kimekuwa na utaratibu wa kuweka Kambi kwaajili ya kupata Mafunzo juu ya namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwakutumia Sayansi,

Alisema kituo hicho kimekuwa na  utaratibu maalumu wa kuweka kambi kwaajili ya kupata mafunzo ya mada husika, kwa mfano Kambi hii tumeifanya kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi Jijini Tanga kwaajili ya kujifunza Kilimo cha Kisasa changamoto mbalimbali za Kilimo Cha Kisasa Maarufu kama Kilimo Janja.

Aidha alisema lakini pia changamoto za kilimo kwa nyakati hizi sote tunafahamu kuwa ni mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo yameperekea upungufu wa Mvua maeneo mengi, hivyo kwakupitia Kambi hii Wanafunzi wameweza kujifunza namna ya kulima Kilimo ambacho hakitahitaji maji mengi, wamejifunza jinsi ya kumwagilia mbegu lakini jinsi ya Kutumia mfumo wa mbolea na Umeme katika Kilimo" Alisema George

Alisema Kituo hicho kitaendelea kuwafundisha Wanafunzi masuala mbalimbali kisayansi nakuwataka Wazazi kuwaruhusu Watoto Wanapokuwa wanahitajika kituoni hapo,

"Kituo chetu kinafundisha Sayansi kwa ujumla na tutaendelea kuandaa Kambi kama hizi, Niwaombe Wazazi muwaruhusu Watoto wenu pale wanapohitajika lakini pia hata pale hatuwahiji ni vizuri Watoto mkawapatia utaratibu maalumu wa kumwezesha kufika kituoni kwaajili ya kujifunza Sayansi, hapa mwanafunzi anaruhusiwa kuja muda wote kujifunza na Walimu wapo muda wote " Alisisitiza George




CCM TANGA KUIRUDISHA TANGA YA VIWANDA

January 20, 2023
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga
Sehemu ya Wazee wa Mkoa wa Tanga wakifuatilia matukio mbalimbali



Na Oscar Assenga, TANGA.

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman amesema wamejipanga ndani ya miaka mitano ya uongozi wao kuhakikisha wanaurudisha mkoa huu kwenye hadhi yake ya viwanda kwa kuvutia wawekezaji wapya.

Mkakati huo ulitangazwa na Mwenyekiti huyo wakati wa kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Tanga ambapo alisema watakachofanya ni kuanisha viwanda vilivyopo kuona changamoto zao na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Rajabu alisema pamoja na hayo ni kuona namna bora ya kuwavutia wawekezaji wapya kwenda kuwekeza kwenye mkoa Tanga ambao una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitawawezesha kuendesha shughuli zao bila vikwazo.

“Kama Mkoa wa Pwani wameweza kufanya vizuri kwenye viwanda kwanini Tanga ambako ndio kwenye asili ya viwanda nyie wazee wetu ndio mnaijua hii vizuri tuiteni mtueeleza kwamba tunakosea wapi moja mbili tatu wazee wetu mnafahamu ”Alisema

“Bandari ya Tanga ilifanya kazi ipasavyo,Reli na tukawa na viwanda vya kutosha ajira za kumwaga na tukachangia kwa kiasi kikubwa pato la uchumi wa Taifa letu lakini niwaambie kwamba kwa sasa tumedhamiria kuirudisha Tanga kwenye hadhi yake tena kwa haraka sana ”Alisema Mwenyekiti huyo

Hata hivyo alisema kwamba uchumi wa Tanga ukiinuka hata vilabu vya Coastal Union na African Sports navyo vitainuka kwa sababu watu wataweze kuvichangia vilabu vyao.

Kuhusu Migogoro ya Ardhi

Mwenyekiti huyo alisema kwamba wamejipanga vema kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kukaa chini kutafutaka namna bora na nzuri ya kuweza kuondoa migogoro ya ardhi kwenye mkoa huo.

Rajabu alisema unaweza usione athari ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji mpaka pale utakapopigiwa simu kwamba ndugu yao ameuwawa kutokana na migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.

“Tumeenda wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hatukutaka kusimuliwa watu imefika wakati wakulima na wafujaji wanauana wanachomea mali zao ukikaa mjini yanayoendelea vijijini huwezi kuyajua na mimi niliomba Uenyekiti kuja kusaidia chama changu,wananchi wa Tanga tumeenda kujioneka na baadhi ya maeneo hali sio shwari lakini kwa kufika CCM katika maeneo hayo hali nzuri imerejea na shwari watu wanaishi kwa Amani hivyo tuitake jamii iendelee kuienzi Amani iliyopo”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanajua serikali inadhamira njema na mkoa wa Tanga na Rais Samia kwa hatua kubwa anayoendelea kuichukua kuimarisha Tanga kiasiasa na kiuchumi hivyo aliwataka waendelee kumpa muda Rais ikiwemo kumuombea na kumuunga mkono yeye na Makamu wa Rais Philip Mpango,Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.

Kauli yake kwa viongozi wa dini.

Mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa dini na wazee wa mkoa huu waisaidie Serikali katika suala la mmomonyoko wa maadili ambalo limekuwa ni tatizo .

“Hivyo tukirudi kwenye maadili mazuri nchi yetu itaendelea kuwa salama na lawama kwa serikali itaondoka na kupungua kwa asilimia kubwa hivyo suala hilo ni muhimu mkubwa kwenu kuhimiza maadili mema “Alisema

Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee alisema Mwenyekti baada ya kuchaguliwa alianza kazi za dharura ikiwemo ya maeneo yalikuwa migogoro ya ardhi mikubwa baina ya wakulima na wafugaji nako kumeanza kutulia. Alisema sasa wanataka kuanza rasmi kazi za Chama wakaona sio vema kuanza bila kukutana na wazee wa mkoa huo wafanye kikao hicho kwa ajili ya Baraka kwa ajili ya ratiba zao mbalimbali za kichama.

MARY CHATANDA APIGA MARUFUKU WABUNGE NA MADIWANI VITI MAALUM KUFANYA VIKAO NA WAJUMBE TU

January 18, 2023




Na Mwandishi Wetu,Dar, 


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzana (UWT) Mary Chatanda amewaonya amepiga pia marufuku Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum kuandaa na kufanya vikao na Wajumbe wa Baraza huku akiwaonya atakayekiuka marufuku hiyo atahukuliwaa hatua kali



Amesema miongoni mwa hatua atakazochukuliwa Mbunge au Diwani wa Viti Maalum akibainika kukiuka marufuku hiyo ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kufikishwa kwenye vikao kuonywa na akikaidi zaidi atafikishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.


Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT katika Mkutano wa Mapokezi uliofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Beach, Kata ya Kawe,ikiwa ni sehemu ya mapokezi rasmi yaliyofanywa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, kufuatia kuwasili kwake mkoani hapa kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo. 


Hata hiyo Mwenyekiti huyo aliwaasa madiwani na wabunge kuacha utaratibu wa kupita kuwatafuta wagombea na kuzungumza nao sio wakati muafaka badala yake wazungumze na wanawake wote na sio wale ambao wamewapigia kura.


Alisema maana kuna utamaduni umejengeka kwamba wanaporudi wilayani au mkoani wanawachukua mjumbe wa baraza tu huyo sio sawa na haipo badala yake waende kukutana na wanawake wote kwenye maeneo yao.


"Na ni marufuku kufanya vitendo hivyo wale watakaobainika wataitwa kwenye vikao na wakionekana wamekaidi watapelekwa kwenye vikao vya maadili lengo ni kukomesha vitendo vya namna hii ndani ya umoja huu"Alisema Mwenyekiti Chatanda. 


Mwisho

MBUNGE SALIM AWAPA TAHADHARI WANAOZIMEZEA MATE FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

January 17, 2023
















“Hamtazila kizembe”


Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe Salim Alaudin Hasham amesema hatamfumbia macho mtu yoyote atakekuwa kikwazo cha kukwamisha mradi wowote unaosimamiwa kupitia fedha za mfuko wa Jimbo.


Mbunge salim ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa shule ya sekondari mwaya kata ya Ruaha kwa lengo la kuwaomba wananchi kujitolea kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ili iweze kukamilika kwa wakati na ianze kutoa huduma.


Mbunge Salim pia amesema kwa mwaka 2022/2023 Serikali kupitia Rais Dkt.Samia Sulluhu Hassan jimbo la Ulanga limepata kiasi cha shilingi Milioni themanini na tisa laki moja na arobaini elfu kama fedha za mfuko wa jimbo (89,140,000/=) ikiwa ni fedha nyingi kupatiwa tangu aingie madarakani.


Mbunge salim amesema kiasi cha Mil 50 amekielekeza kukamilisha bweni la wasichana  Shule ya sekondari mwaya kata ya ruaha kwa lengo la kupunguza mimba za utotoni na kuinua kiwango cha elimu katika jimbo la Ulanga.


Aidha Mbunge Salim amemtaka mhandisi wa halmashauri hiyo ndugu Amir Athumani kuhakikisha wanazitumia vyema fedha hizo na zinakamilisha mradi huo wa bweni kwa wakati bila kikwazo chochote ili watoto wa kike waanze kulitumia.


Mbali na mkutano huo mbuge salim pia amefanya ziara ya kukagua miradi yote iliyopata fedha za mfuko wa jimbo kwa mwaka 2021/22 ili kujiridhisha kama fedha hizo zimefanya kazi vyema kama ilivyoelekezwa na kamati ya mfuko wa jimbo katika vikao vyao.


Mbunge salim amemshukru Rais Dkt Samia sulluhu Hassan kwa kuendelea kuikumbuka wilaya ya Ulanga katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya,elimu,miundombinu na miradi mbalimbali ya maendeleo.

MABONDIA ZAIDI YA 20 KUPANDA ULINGONI JANUARI 18 NA 28 JIJINI TANGA KUONYESHANA UMWAMBA

January 17, 2023

 



MASHABIKI wa ngumi mkoa wa Tanga wanatarajiwa kushuhudia pambano la ngumi la kufungua mwaka 2023 wakati w mabondia Mustafa Doto kutoka Dar es Salaam atakapopambana na Said Mundi kutoka Tanga katika mnyukano wa round 10 kesho Januari 18, 2023. 


Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa leo, Promota maarufu  nchini, Ali Mwazoa na ambaye pia mtayarishaji wa pambano hilo alieleza kutakuwa na mengine ya utangulizi  9.


Mapambano hayo yatakuwa kati ya Jay Jay atakayepambana na Peter Julius wakati Jonas Mtafya atapigana na Patrick Kimweri.  Wengne ni Hamis Mwambashi dhdi ya Haji Juma, wote kutoka Tanga.


Mtoto wa bondia mkongwe nchini, Rashid Matumla, Snake Junior atapambana na Ali Reli wote kutoka  Tanga..


Haya ni mapambano ya utangulizi kwa ajili ya mabondia chipukizi kuelekea pambano kubwa la aina yake mkoani na nchini Tanzania kati ya mabondia wawili wanaogopwa, Ibrahim Classic atakayemkabili bondia mwenye mikwara na ngumi nzito, Ndondande Harmer, wa nchini Zimbabwe. Pambano hilo litakuwa la round 10.


Promota Mwazoa alitoa wito kwa mashabiki wa jijini Tanga na nje ya  mkoa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mabambano hayo mawili yatakayofanyika 18 na 28 Januari ambayo yatautangaza mkoa katika fursa za biashara na ajira.


Pia Mwazoa aliahidi kuandaa mapambano mengine ya ngumi ambayo yatatoa zaidi fursa kwa vijana wanaochipukia katika ulingo wa michezo ya ngumi nchini.

DKT MWINYI ATETA NA VIONGOZI WA UWT TAIFA LEO WAMPONGEZA

January 16, 2023






Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg Mary Chatanda akikabidhi Tuzo ya Pongezi kwa Mhe Dkt Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Uchaguzi 2020-2025. #UWTImara #JeshiLaMama #KaziIendelee

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiteta jambo na ujumbe waViongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leo


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiteta jambo na ujumbe waViongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leo
Ndg Mary Chatanda, Mwenyekiti wa UWT Taifa akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi mara baada ya mazungumzo


Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar Dkt Hussein Ali Mwinyi akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Zainab Shomari mara baada ya kuteta na Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Ikulu Zanzibar mapema leoujumbe ambao uliongozwa na Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda.
Ndg Riziki Kingwande, Naibu Katibu Mkuu UWT - Bara





Mbunge Neema Lugangira: Mbunge Neema Lugangira akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu   






Na Mwandishi WetuZanzibar.

 

Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi leo Jumatatu Januari 16,2023 amekutana na Viongozi wa Umoja  wa Wanawake Tanzania (UWT) Ikulu Zanzibar.

Uongozi wa Jumuiya hiyo uliongozwa  na Mwenyekiti wa  UWT Taifa Ndugu Mary Chatanda ,Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa aliyeambatana na  Makamu Mwenyekiti UWT Zanzibar Ndugu Zainab Shomari ,viongozi mbalimbali wa  kitaifa wa Jumuiya hiyo kwa nia ya kujitambulisha baada ya kuchaguliwa .

 Pia wamempongeza Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa kuchaguliwa  kuwa Makamu Mwenyekiti CCM Zanzibar na Kutekeleza Ilani ya CCM ya Utekelezaji 2020-2025 .

WAZIRI AWESO ATUA TANGA KUFUATILIA TATIZO LA MAJI,ATOA MAELEKEZO KWA TANGA UWASA

January 14, 2023

 



Waziri wa maji Jumaa Aweso  akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi 
Waziri wa maji Jumaa Aweso  akizungumza wakati wa ziara yake Jijini Tanga ya kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi kwa wananchi 
Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule  akizungumza wakati wa ziara hiyo
KATIBU wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee akizungumza wakati wa ziara hiyo
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly akieleza hatua walizochukua kuondosha changamoto hiyo


Waziri wa Maji Jumaa Aweso katika mwenye kofia akikagua maji katika mtambo wa kusafishia maji wa Mowe Jijini Tanga wakati wa ziara yake 
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akiwa kwenye mtaa wa Chumbageni Jijini Tanga akikagua upatikanaji wa maji kwa wananchi wakati wa ziara yake 






Na Oscar Assenga,Tanga

Waziri wa maji Jumaa Aweso amelazimika kutua Mkoani Tanga kwa ajili ya kufuatilia uwepo wa changamoto ya kukosekana kwa huduma ya maji huku akiitaka Mamlaka ya Maji Safi na Usafiri wa Mazingira (Tanga Uwasa) kuhakikisha taarifa zinatolewa kwa wakati kwa wananchi inapojitokeza hitilafu ya ukosefu wa huduma hiyo muhimu ili kuondoka malalamiko kwao.

Sambamba na hayo aliagiza Bonde la Maji la Mto Pangani kufanya ufuatiliaji kwa wote wanaofanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji na hatua kali kuchukuliwa dhidi yao ili kuhakikisha wanakomesha vitendo vya watu kufanya shughuli zao

Akizungumza wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga kuangalia hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wananchi kufuatia changamoto ya ukosefu wake kwa baadhi ya wananchi kwa siku nne mfufulizo chanzo kikitajwa ni uchafuzi wa mazingira uliofanywa na wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji vya Mto Zigi hali iliyopelekea maji kuwa katika hali ya uchafu usio kawaida na hivyo kuifanya mamalaka hiyo kusitisha huduma kwa wananchi ili kutatua changamoto hiyo.

Waziri Aweso alisema jukumu la utoaji wa huduma ya maji safi na salama kwa jiji la Tanga ni la Tanga Uwasa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji hivyo ni kwa nini wananchi walipata huduma ya maji isiyo ya kawaida baada ya kuona maji katika hali ile waliamua kuzima mitambo kwahiyo kelele za watu kukosa maji yaliyokuwa yanapatikana zilileta taharuki pamoja na changamoto iliyojitokeza watu wa maabara na wataalamu wameweza kuyatibu na sasa hivi yapo katika hali yake na tumepita kwa wananchi baadhi ya nyumba maji yapo.

Alisema kubwa ambalo alitaka kusisisitiza kwao ni kwamba inapotokea changamoto kukosekana kwa maji sio jambo baya lazima watoe taarifa kwa wakati na hivyo kutokuitoa kunapelekea tahatuki kwa wananchi hivyo jambo hilo waangalie na lisiitokeze tena .

“Lakini Tanga Uwasa utoaji wa huduma ya majisafi na salama ni wajibu na majukumu ya mamlaka yenu kwahiyo lazima mjipange kuhakikisha mnatoa huduma ya maji safi na salama wakati wote “Alisema Waziri Aweso

“Ndugu zangu maji hayana mbadala lakini pamoja na kurejea huduma hii lazima iundwe timu maalum ya kupita kila mtaa kuona huduma ya maji inarejea kama kawaida yake nina imani hili jambo haliwezi kutokea tena"


Aidha waziri Aweso ameitaka bodi ya mamlaka hiyo kukaa na kujadili namna watakavyoweza kupambana na kutatua changamoto zinazopelekea kukosekana kwa maji akiitaka pia kufanya kikao cha pamoja na madiwani na wenyeviti wa mitaa kuwaeleza hali halisi ya utekelezaji wake hii ikilenga hasa kuweka wazi taarifa za kiutendaji zitakazosaidia kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

Akieleza changamoto iliyopelekea kukosekana kwa huduma ya maji kwa siku kadhaa mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Tanga uwasa Geofrey Hilly alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kufanya shughuli zao ikiwemo uchimbaji wa madini katika chanzo kibwa cha Mto Zigi kinachotegemewa na mamlaka hiyo hali iliyopelekea kuchafuka kwa maji.

"Tumekuwa na changamoto ya upungufu wa maji tangu mwezi wa 10 mwaka 2022 changamoto kubwa ilikuwa ni upungufu wa umeme katika maeneo yetu ya kuzalisha maji lakini hivi karibuni ikatokea changamoto ya kuchafuka sana kwa maji na imetokana na hali ya uchafuzi wa mazingira katika chanzo chetu kikubwa cha mto Zigi na hata usafishaji wake ulikuwa ni wa hali ngumu kwahiyo tukazima kwanza maji yasije tuyatibu na tumefanikiwa na hivyo tayari maji yameshaanza kutoka kwa baadhi ya maeneo"


Hilly alisema kuwa Mamlaka hiyo ipo mbioni kupambana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza mara kwa mara ambapo wamejipanga kununua mitambo maalumu ya kudhibiti changamoto ya kupungua kwa umeme , kupatikana kwa mradi mkubwa wa kujenga tanki la kuhifadhia maji ambapo hata itakapotokea changamoto ya umeme bado maji yatakuwa yanapatikana kwa uhakika.

Hata hivyo kwa upande wake Mkurugenzi wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule amekiri uwepo wa baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na vyanzo vya maji licha ya jitihada wananzozifanya akiahidi kupokea na kwenda kutekeleza maagizo ya waziri wa Maji Jumaa Aweso.



Alisema bonde hilo ndio lenye dhamana ya kuhakikisha kuwa wenzao wanaochukuwa maji kwenye vyanzo yana kuwa kwenye ubora stahiki hivyo wamezingatia maelekezo ya viongozi na wameshajipanga kutekeleza na wamekuwa wakichukua hatua mbalimbali kwa kushirikiana na madiwani serikali za wilaya na mikoa.



Akizungumza Katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Suleiman Mzee ameipongeza Tanga Uwasa kwa jitihada za haraka ilizozifanya kutatua changamoto ya kuchafuka kwa maji hali iliyoleta taharuki kwa wakazi wa jiji la Tanga kwa siku nne mfululizo huku akiwataka wananchi kuendelea kutunza na kuvilinda vyanzo vya maji vilivyopo.



Akizungumza mmoja wa madiwani wa Jiji la Tanga Salimu Perembo ameishauri mamlaka hiyo kupanua huduma zake kwa upande wa majitaka hii ikienda sambamba na ongezeko la wananchi na makazi ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza.



Mamlaka ya maji safi na usafi wa Mazingira inazihudumia wilaya za Tanga Pangani pamoja na Muheza ikiwa inazalisha lita zaidi ya 30 za maji kwa siku ambapo sasa inatekeleza mradi unaogharimu shilingi Billion 9.18 ambao mara baada ya kukamilika utaiwezesha Tanga uwasa kuwa na uhakika maji ya kutosha kwa mahitaji ya wananchi.

MWENYEKITI WA CCM TANGA AMPONGEZA RAIS DKT SAMIA SULUHU KWA KUIMARISHA DEMOKRASIA NCHINI

January 09, 2023

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Jijini Tanga wakati akitoa tamko la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dkt Samia Suluhu

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza 

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo




Na Oscar Assenga, TANGA



CHAMA cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (CCM) kimetoa wito kwa wana CCM Mkoa huo kujielekeza katika kufanya siasa zenye hoja,tija na majawabu kwa watanzania wa rika zote na ambaye atakwenda kinyume chake chama kitahangaika naye ili kupata heshima anayostahili kupata Rais Dkt Samia Suluhu

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga Rajab Abdurhaman wakati akizungumza na waandishi wa habari akitoa tamko la wana CCM Mkoa wa Tanga la kumpongeza na kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha na kuishaurisha demokrasi Nchini.

Ambapo alisema kufuatia Rais Samia kuridhia kufanyika kwa mikutano ya hadhara ni vyema kila chama cha siasa kuheshimu taratibu na sheria zilizopo ili kufanya siasa zenye utashi na ustawi wa maendeleo huku akitaka vyama vya siasa kutumia nafasi walioipata kuheshimu taratibu zilizopo ili kufanya siasa za kistaarabu.

"Ndugu zangu waandishi nimewaita leo hii ili kuongea na wana CCM na watanzania kwa ujumla kuongea juu ya mambo makubwa mawili ambayo mwenyekiti wa ccm Taifa na Rais dkt Samia Suluhu Hassan kayapanga kwa upendo mkubwa kwa watanzania na vyama vyote nchini moja kukubali maridhiano ya mazungumzo baina ya serikali ya ccm chama cha mapinduzi na vyama vingine vya siasa vipavyo 18,"

Alisema kwamba baada ya kuruhusiwa kufanyika kwa mikutano ya siasa hawata mvumilia au kuona mwanasiasa yeyote ambaye atakuwa na nia ovu ndani ya ccm na nje ya ccm ya kuvuruga mikutano ya vyama vya siasa ambalo ni tamko lililoruhusiwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

"Kuridhia na kukubali yeye binafsi na chama cha mapinduzi juu ya kuruhusu kazi ya kuimarisha siasa ya vyama vyote nchini kuendelea kufanya siasa bila upendeleo kwa kuruhusu mikitano ya hadhara hivi karibuni alipokutana na vyama vyote hivyo kama Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga na kwaniaba ya wana CCM na wananchi wote wa Mkoa wa Tanga tunatoa pongezi nyingi kwa hatua hii ambayo imeonyesha kuwa Rais ni mtu mwenye hofu ya Mungu na amejua na kuelewa kwa busara za hali ya juu kuliongoza Taifa letu na wananchi wake, "Alisema Mwenyekiti Rajab.


Mwenyekiti Rajab alisema mchakato huo ulianza kwa mazugumzo ambayo yalipelekea kuunda kikosi kazi kitakachofanya kazi kwa weledi na ustadi zaidi ili kutoa maoni na ushauri namna ya kufanya siasa baina ya vyama vyote nchini ambapo kazi hiyo haikuwa rahisi kama wanavyofikiria.

Alisema jambo hilo lilihitaji uongozi makini na wenye busara za kiungozi ili kupokea na kufanya maamuzi juu ya kuridhia kuanza siasa kwa usawa wa vyama vyote hivyo kutokana na hilo wamempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

"Maono ya Mwenyekiti wetu wa ccm na Rais yamejikita katika mawazo ya (4R) maridhiano na ustahamilivu katika mabadiliko ya kujenga umoja na mshikamano baina yetu sisi kama watanzania na wanaccm tunapaswa kumpa ushirikiano mkubwa kufanya jambo hili kuwa na ukweli wa wazi ili kila mmoja wetu afaidi matunda ya mawazo yake, "alisisitiza Rajab.

"Kwa muktaza huo wanaccm na wananchi wa Mkoa mzima wa Tanga nimesimama mbele yenu kuelezea furafa yetu katika jambo hili muhimu lenye tija kwa maendeleo ya watanzania wote wapenda amani pia tunaelekeza mawazo yetu na nguvu zetu katika kulisimamia na kuliishi tanko hili ambalo ni dira maendeleo ya siasa, "

Aidha amewataka viongozi na watendaji wa serikali kusimamia maelekezo ya Rais kwa vitemdo bila kusahau kuimarisha ulinzi na usalama kwa kila mtanzania.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Mohamed Ratco wakati huu serikali imefungua pazia la mikutano ya hadhara ni vyema vyama vyote vizingatie sheria na kanuni zinavyoeleza wakati wakitekeleza wajibu wao.

"Kila kitu kina mipaka yake ukikengeuka ukasema mambo yasiyofaa sheria itachukua mkondo wake ni vyema kila mwanasiasa akafuata taratibu sheria na kanuni za mikutano zinavyotaka, "alisema Ratco.

Alisema jambo la Rais Dkt Samia Suluhu Hassan la kuruhusu mikutano ya hadhara lengo ni kupana wigo wa siasa nchini ikiwemo kurekebishana, kutoa maoni na kushauriana ili isaidie kuchochea maendeleo.