MARY CHATANDA APIGA MARUFUKU WABUNGE NA MADIWANI VITI MAALUM KUFANYA VIKAO NA WAJUMBE TU

January 18, 2023




Na Mwandishi Wetu,Dar, 


Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzana (UWT) Mary Chatanda amewaonya amepiga pia marufuku Wabunge na Madiwani wa Viti Maalum kuandaa na kufanya vikao na Wajumbe wa Baraza huku akiwaonya atakayekiuka marufuku hiyo atahukuliwaa hatua kali



Amesema miongoni mwa hatua atakazochukuliwa Mbunge au Diwani wa Viti Maalum akibainika kukiuka marufuku hiyo ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kufikishwa kwenye vikao kuonywa na akikaidi zaidi atafikishwa Kamati ya Maadili kwa ajili ya hatua zaidi.


Chatanda aliyasema hayo wakati akizungumza na Viongozi na Wanachama wa UWT katika Mkutano wa Mapokezi uliofanyika katika Ukumbi wa Kiramuu, Mbezi Beach, Kata ya Kawe,ikiwa ni sehemu ya mapokezi rasmi yaliyofanywa na UWT mkoa wa Dar es Salaam, kufuatia kuwasili kwake mkoani hapa kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo. 


Hata hiyo Mwenyekiti huyo aliwaasa madiwani na wabunge kuacha utaratibu wa kupita kuwatafuta wagombea na kuzungumza nao sio wakati muafaka badala yake wazungumze na wanawake wote na sio wale ambao wamewapigia kura.


Alisema maana kuna utamaduni umejengeka kwamba wanaporudi wilayani au mkoani wanawachukua mjumbe wa baraza tu huyo sio sawa na haipo badala yake waende kukutana na wanawake wote kwenye maeneo yao.


"Na ni marufuku kufanya vitendo hivyo wale watakaobainika wataitwa kwenye vikao na wakionekana wamekaidi watapelekwa kwenye vikao vya maadili lengo ni kukomesha vitendo vya namna hii ndani ya umoja huu"Alisema Mwenyekiti Chatanda. 


Mwisho

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »