MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman akizungumza na wazee wa Mkoa wa Tanga |
Na Oscar Assenga, TANGA.
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Tanga Rajabu Abdurhaman amesema wamejipanga ndani ya miaka mitano ya uongozi wao kuhakikisha wanaurudisha mkoa huu kwenye hadhi yake ya viwanda kwa kuvutia wawekezaji wapya.
Mkakati huo ulitangazwa na Mwenyekiti huyo wakati wa kikao chake na Wazee wa Mkoa wa Tanga kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM Mkoa wa Tanga ambapo alisema watakachofanya ni kuanisha viwanda vilivyopo kuona changamoto zao na kuona namna ya kuzipatia ufumbuzi.
Rajabu alisema pamoja na hayo ni kuona namna bora ya kuwavutia wawekezaji wapya kwenda kuwekeza kwenye mkoa Tanga ambao una fursa nyingi za kiuchumi ambazo zitawawezesha kuendesha shughuli zao bila vikwazo.
“Kama Mkoa wa Pwani wameweza kufanya vizuri kwenye viwanda kwanini Tanga ambako ndio kwenye asili ya viwanda nyie wazee wetu ndio mnaijua hii vizuri tuiteni mtueeleza kwamba tunakosea wapi moja mbili tatu wazee wetu mnafahamu ”Alisema
“Bandari ya Tanga ilifanya kazi ipasavyo,Reli na tukawa na viwanda vya kutosha ajira za kumwaga na tukachangia kwa kiasi kikubwa pato la uchumi wa Taifa letu lakini niwaambie kwamba kwa sasa tumedhamiria kuirudisha Tanga kwenye hadhi yake tena kwa haraka sana ”Alisema Mwenyekiti huyo
Hata hivyo alisema kwamba uchumi wa Tanga ukiinuka hata vilabu vya Coastal Union na African Sports navyo vitainuka kwa sababu watu wataweze kuvichangia vilabu vyao.
Kuhusu Migogoro ya Ardhi
Mwenyekiti huyo alisema kwamba wamejipanga vema kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kukaa chini kutafutaka namna bora na nzuri ya kuweza kuondoa migogoro ya ardhi kwenye mkoa huo.
Rajabu alisema unaweza usione athari ya migogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji mpaka pale utakapopigiwa simu kwamba ndugu yao ameuwawa kutokana na migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
“Tumeenda wenyewe kwenye baadhi ya maeneo hatukutaka kusimuliwa watu imefika wakati wakulima na wafujaji wanauana wanachomea mali zao ukikaa mjini yanayoendelea vijijini huwezi kuyajua na mimi niliomba Uenyekiti kuja kusaidia chama changu,wananchi wa Tanga tumeenda kujioneka na baadhi ya maeneo hali sio shwari lakini kwa kufika CCM katika maeneo hayo hali nzuri imerejea na shwari watu wanaishi kwa Amani hivyo tuitake jamii iendelee kuienzi Amani iliyopo”Alisema
Hata hivyo alisema kwamba wanajua serikali inadhamira njema na mkoa wa Tanga na Rais Samia kwa hatua kubwa anayoendelea kuichukua kuimarisha Tanga kiasiasa na kiuchumi hivyo aliwataka waendelee kumpa muda Rais ikiwemo kumuombea na kumuunga mkono yeye na Makamu wa Rais Philip Mpango,Waziri Mkuu Kasim Majaliwa.
Kauli yake kwa viongozi wa dini.
Mwenyekiti huyo aliwataka viongozi wa dini na wazee wa mkoa huu waisaidie Serikali katika suala la mmomonyoko wa maadili ambalo limekuwa ni tatizo .
“Hivyo tukirudi kwenye maadili mazuri nchi yetu itaendelea kuwa salama na lawama kwa serikali itaondoka na kupungua kwa asilimia kubwa hivyo suala hilo ni muhimu mkubwa kwenu kuhimiza maadili mema “Alisema
Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga Suleiman Mzee alisema Mwenyekti baada ya kuchaguliwa alianza kazi za dharura ikiwemo ya maeneo yalikuwa migogoro ya ardhi mikubwa baina ya wakulima na wafugaji nako kumeanza kutulia. Alisema sasa wanataka kuanza rasmi kazi za Chama wakaona sio vema kuanza bila kukutana na wazee wa mkoa huo wafanye kikao hicho kwa ajili ya Baraka kwa ajili ya ratiba zao mbalimbali za kichama.
EmoticonEmoticon