TANGA PRESS CLUB WAFANYA BONANZA LA KUHAMASISHA SENSA NA KUTAMBUA JUHUDI ZA RAIS SAMIA SULUHU KATIKA MAENDELEO

August 29, 2022

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa bonanza hilo kushoto ni Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akifuatiiwa na Bondia Mwakinyo na Afisa Michezo Mkoa wa Tanga Digna Tesha
MKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba akizungumza wakati wa bonanza hilo kushoto ni Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George akifuatiiwa na Bondia Mwakinyo na Afisa Michezo Mkoa wa Tanga Digna TeshaMKUU wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba kulia akiwa na Mwenyekiti wa Tanga Press Club Lulu George na Bondia Hassani Mwakinyo wakifuatilia bonanza hilo
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandiliwa akizungyumza wakati wa bonanza hilo

 Na Mwandishi Wetu,TANGA.

Bonanza la Mama Tumeikita lenye lengo la kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Mkoani Tanga ikiwemo kutambua jitihaza za Rais Samia Suluhu katika maendeleo ya Taifa hapa .

Bonanza hilo ambalo liliandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga *TPC*limefanyika mwishoni mwa wiki Jijini Tanga kwenye viwanja vya Disuza kwa kushirikisha viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omari Mgumba.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Bonanza hilo Mkuu wa Mkoa Mgumba alisema aliupongeza uongozi wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoani Tanga chini ya Mwenyekiti wake Lulu George kwa kuanza na kuratibu bonanza hilo ambalo lilikuwa la aina yake.

Alisema ubunifu ambao umefanywa na uongozi wa klabu hiyo unapaswa kuungwa mkono huku akisema bonanza hilo limefanikiwa sana  huku akiwataka viongozi hao kuhakikisha linakuwa endelevu mara kwa mara na kuwahaidi ushirikiano.

“Niwapongeze Tanga Press Club kwa ubunifu huu mkubwa mlioufanya kwa kuhamasisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi na kutambua juhudi za Rais kuwaletea maendeleo wa Tanga limefanikiwa sana nimpongeza Mwenyekiti wa TPC na viongozi wengine kwa kufanikisha bonanza hilo ambalo limewakutanisha pamoja wanajamii wote wa Tanga,viongozi wa mkoa wilaya mpaka vitongoji na waandishi wa habari”Alisema

Alisema kwamba amefurahishwa kwamba na kupendwa na ujumbe uliobebwa kwenye bonanza hilo mama huku akisisitiza umuhimu wa jamii ya wana Tanga kuhakikisha wanaendelea kushiriki zoezi la Sensa ya watu na Makazi ikiwemo kuendelea kuwahabarisha wana Tanga.

Awali akizungumza wakati wa Bonanza hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa aliushukuru uongozi wa Tanga Press Club kuweza kuliandaa bonanza hilo ambalo limewakutanisha wadau mbalimbali kuishiriki katika michezo ambayo ni muhimu kiafya.

Mkuu huyo wa wilaya aliwataka waandishi wa habari mkoani humo waendelee kuboresha mahusiano baina yao kwa wao na taasisi mbalimbali za serikali na kupitia wao wanaweza kuwa na mabonanza mbalimbali huku akiwaomba waone umuhimu wa kufanya hivyo.

DC KISSA AWAHAMASISHA WANANCHI KUCHANJA UVIKO 19

August 15, 2022

 



Mkuu wa Wilaya ya Njombe mkoani Njombe Kissa Kasongwa (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Etv na Efm Redio, Majizzo (wa pili kushoto) kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Agosti 13, 2022 Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Njombe Filoteus Mligo (wa pili kulia), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. Zabron Masatu (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Njombe Kuruthum Sadick (kushoto). (Picha na Yusuph Mussa)


Wananchi wakiwa wamefurika kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Agosti 13, 2022 Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19. (Picha na Yusuph Mussa).
 Wananchi wakiwa wamefurika kwenye Tamasha la Mziki Mnene lililofanyika Agosti 13, 2022  Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19. (Picha na Yusuph Mussa).



Na Yusuph Mussa, Njombe

MKUU wa Wilaya ya Njombe mkoani Njombe Kissa Kasongwa amesema wapo kwenye jitihada za kuongeza idadi ya watu wanaochanja chanjo ya UVIKO 19 kwenye wilaya hiyo, na ndiyo maana wanafanya jitihada mbalimbali ikiwemo kuandaa matamasha.

Aliyasema hayo Agosti 13, 2022 kwenye tamasha la Mziki Mnene lililoratibiwa na Efm Redio kutoka Dar es Salaam na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe na kufadhiliwa na Epic/ FHI 360 kwa ajili kuhamasisha wananchi wachanje chanjo ya UVIKO 19, ambalo tamasha hilo lilifanyika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

"Tupo kwenye jitihada za kuongeza idadi ya wananchi wanaochanja chanjo ya UVIKO 19. Nia yetu ni kuona asilimia 70 ya wananchi wa Wilaya ya Njombe wanakuwa wamechanja. Wataalamu wanasema, kama asilimia 70 wataweza kuchanja, itakuwa ni kinga kwa wengine" alisema Kasongwa wakati anazungumza na wanahabari pembeni ya tamasha hilo.

Akizungumza na wananchi kwenye tamasha hilo, Kasongwa aliwaasa wananchi kujitokeza kwa hiari yao na kuchanja chanjo ya UVIKO 19 ili waendelee kuwa salama, na kuendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani.

'Ujanja ni kuchanja. Kuchanja sio suala la mzaha. Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan ametutaka tuchanje kwa hiari yetu ili tuwe salama. Hata Shirika la Afya Duniani (WHO) linatutaka tuchanje. Tukichanja tutaushi, ila tukiacha kuchanja tutakufa. Tuhakikishe tunachanja na kuepukana na ugonjwa huu wa hatari" alisema Kasongwa akiwa amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka kwenye tamasha hilo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya zoezi hilo la uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 kukamilika, Mratibu wa Chanjo Halmashauri ya Mji Njombe Simon Ngassa, alisema watu waliojitokeza kuchanja kwenye tamasha hilo ni 4,563, ambapo wanaume ni 1,954 na wanawake 2,609.

"Lengo ni kuchanja watu 98,396, ambao Ni asilimia 70 ya watu wenye umri wa miaka zaidi ya 18.. Tulianza kuchanja Agosti 3, 2021, na hadi Agosti 13, 2022 tumechanja jumla ya watu  92,422 sawa na asilimia  93.

"Dira yetu ni kufikia lengo la asilimia 100 ifikapo Septemba 30 mwaka huu 2022. Kwa kushirikiana na wadau wetu FHI360,  na wadau mbalimbali kwa pamoja na mikakati ya hamasa ya matamasha makubwa, na ushirikiano wa  DC (Kasongwa) na Mbunge (Deo Mwanyika- Njombe Mjini) katika ziara ya kijiji kwa kijiji kuhamasisha chanjo kwa wananchi" alisema Ngassa.

MWISHO.

LUHAGA MPINA ACHUKUA FOMU YA KUWANIA NAFASI YA HALMASHAURI KUU YA CCM TAIFA VITI 15 TANZANIA BARA

August 10, 2022

 


Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akikabidhiwa fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara na Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10, 2022


Mbunge wa Kisesa, Luhaga Joelson Mpina (kushoto) akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika Ofisi ya CCM Mkoa wa Dodoma kabla ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara kulia ni Ndg. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma leo Agosti 10,2022.

MBUNGE wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Joelson Mpina amechukua na kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi kuwania nafasi ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC) kupitia kundi la Viti 15 Tanzania Bara.

Mpina amechukua na kurejesha fomu hiyo leo Agosti 10, 2022 ikiwa ni siku ya mwisho ya zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa chama hicho kwa mwaka 2022.

Mbunge huyo wa Kisesa amechukulia fomu hizo katika Ofisi ya Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma na kukabidhiwa fomu hizo na Ndugu. Matilda Mgeni, Karani wa Masijala ya CCM Mkoa wa Dodoma.

Mpina amechukua fomu hizo leo Dodoma ikiwa ni siku chache tangu kuhitimu Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Operesheni Venance Mabeyo katika Kambi ya Kikosi cha Jeshi Makutupora Dodoma mafunzo yaliyomalizika Agosti 5, 2022.

WATUMISHI WA SERIKALI TANGA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA NYONGEZA YA MSHAHARA,WASEMA AMEUPIGA MWINGI

August 05, 2022

 



Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja

 Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja



Mtumushi wa Jiji la Tanaga Mwanaidi Mashaka






Na Oscar Assenga,Tanga.

WATUMISHI wa Serikali Mkoani Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara ya asilimia 23 ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo ambalo miaka ya nyuma halikufanyika na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu yao ipasavyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari Jijini Tanga jambo ambalo amelifanya kwao ni kubwa mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.

Akizungumza mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka alisema wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo limefanyika.

“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii”Alisema

Naye kwa upande wake mtumishi mwengine Waziri Ally ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Elimu ya Msingi alisema wana mpongeza Rais kwa mengi aliyoyafanya kwa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23 imewagusa moja kwa moja wao kama watumishi.

Alisema asilimia 23 sio ndogo wanaweza kufanya jambo kubwa kama watumishi na wana morali wa kufanya kazi kwa bidii ili kuweza malengo yaliyotarajiwa yanafikiwa.

“Kwa kweli ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara na ongezeko la watumishi sasa tumekuwa wengi na tunafanya kazi bila kuwepo kwa mzigo mkubwa”Alisema

Hata hivyo kwa upande wake Stella Siang’a ambaye ni mtumishi wa Jiji Kada ya Elimu alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewafanyia mengi mno jambo la kwanza ni kuongeza wafanyakazi miaka mingi watu walikuwa hawajaajiriwa walikuwa mitaani iliyokwenda sambamba na ongezeko la mishahara ambalo litawawezesha kufanikisha majukumu yao.

Halikadhalika mtumishi mwengine Kasim Bashiru Lyimo kutoka Idara ya Elimu Sekondari alisema kwamba wanampongeza Rais Samia ameupiga mwingi kwa mambo mazuri aliyoyafanya kwa kuweza kuwaongezea asilimia 23 ya mshahara.

“Hili jambo sisi tumelifurahia sana na tupo pamoja na Rais na tuna hari ya kufanya kazi na atakapokuwepo mama na sisi tutakuwepo kuhakikisha tunamuunga mkono”Alisema

Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkwakwani Joshua Kiula alisema wana mpongeza Rais Samia kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuifungua nchi na inakwenda na imetulia .

Alisema pia amefanikiwa kufungua biashara zilikuwa zimefungwa na kurudisha na kuhuisha mahusiani na mataifa mengine ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha madaraja.

“Kwa kweli Rais Samia ameupiga mwingi kubwa ni kupandisha madaraja ambayo ni haki ya Msingi ya wafanyakazi na nyongeza ya mishahara jambo hilo ni nzuri na limewapa faraja kubwa kwetu”Alisema

Hata hivyo alisema nyongeza hiyo hawakuitegemea kama wataipata walidhani walipopandisha huo ndio ungekuwa mwisho lakini akaje na jambo lingine kwao la kuwaongezea asilimia 23 wamelipokea kwa moyo mkunjufu.

WAZIRI AWESO AMALIZA MZIZI WA FITNA KARATU,AAGIZA BEI YA MAJI IWE 1,300 UNITI MOJA.

August 02, 2022

 



Mwandishi wetu,

Waziri wa Maji,Jumaa Aweso ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu wilayani Karatu baada ya kuamuru kuwepo kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma ya maji katika Mji huo huku akiagiza bei ya maji inayostahili kutozwa kwa sasa ni sh1,300 kwa uniti1  badala ya sh,2,000 hadi sh 3,000.

Aweso ameagiza kuungana kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) na Mamlaka ya Utoaji wa  Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU) na kutengeneza chombo kimoja ambacho kitatoa huduma kwa wananchi kwa maslahi ya wananchi wa Karatu.


Hatahivyo waziri Aweso alitamka kwamba Rais Samia Hassan Suluhu ameridhia kutoa sh,bilioni 4.5 kwaajili ya mradi mkubwa wa maji wilaya hiyo na kuagiza mamlaka husika zianze kutangaza zabuni ya mkandarasi atakayetekeleza mradi wa kusambaza maji wilayani humo.

Awesso amesema hayo leo baada ya kusikiliza maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa maji wilayani humo ambapo awali kulikuwa na mgawanyiko wa maslahi ikiwemo Kaviwasu kutoza sh, uniti moja kwa sh,2000 hadi 3000 huku Karuwasa ikitoza sh,1,750 kwa bei za majumbani.

Alisema uwepo huo wa chombo kimoja kutawezesha maslahi ya wananchi ikiwemo utoaji wa huduma bora za utoaji maji pamoja na kuhakikisha miundombinu ya maji haiharibiki.

 Alisema hakuna mtumishi yoyote atakayefukuzwa baada ya kuungana Karuwasa na Kaviwasa kwa kuwa watakapoungana lita zaidi ya milioni 6 zitakuwepo ndani ya mamlaka moja ambazo zitakidhi mahitaji ya wakazi wa wilaya hiyo.

"Wekeni utaratibu mkandarasi atangazwe aanze kazi ya kusambaza miundombinu ya maji na nyie wenyewe mtaunda bodi itakayopanga mipango yake kwani maji si biashara bali ni huduma,tuunganishe mamlaka hizi na utaratibu wa bei uwe ni sh,1300 kwa uniti 1 kwa kila mwananchi "alisema Aweso 

Aliagiza bei atakayotozwa mwananchi wa kawaida kwa hivi sasa iwe ni sh,1,300 kwa uniti 1 wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za  Nishati na Maji( Ewura) ikiendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi juu ya ulipaji wa ankara za maji.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba,alimshukuru Waziri Aweso kwa kutoa maagizo hayo kwani wananchi watanufaika na bei moja badala ya awali kuwa na mkanganyiko wa bei kati ya Karuwasa na Kaviwasu

Alisema baada ya Rais Samia kutangaza filamu ya Royal Tour watalii wamefurika wilayani Karatu na hivi sasa hoteli zaidi ya 60 zilizopo hapo zinahitaji maji hivyo aliomba wilaya hiyo kupewa zaidi vipaumbele vya maji ili kuwezesha kila mtu kunufaika na huduma za maji.

Awali,Ofisa Tawala  Mkuu kutoka Wizara ya Maji,Jacob Kingazi akisoma mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Waziri Aweso kwaajili ya kufanya tathimini ya hali ya upatikanaj wa huduma ya maji mji wa Karatu,alisema lazima kuwepo Kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma katika mji wa karatu ili kuondoa migogoro.

Kingazi alisema awali walibaini bodi kuendelea kutekeleza baadhi ya majukumu ya kiutendaji ilhali ilifikia ukomo mwaka 2019 ikiwemo ukusanyaji wa ukusanyaji mapato.

Naye  mbunge la jimbo la Karatu, Daniel Awackii alimshukuru  Waziri,Aweso kwa kuunganisha bodi hizo mbili na kuwa moja kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa hivi sasa watafanya vikao kwa wanachi kwaajili ya kuwaeleza wananchi kulipa ya bei hiyo ya unit 1,300 kwa kila mmoja badala ya sh,2000 hadi 3000 zinazotozwa na Kaviwasu

Mwisho.