Mwandishi wetu,
Waziri
wa Maji,Jumaa Aweso ametatua mgogoro uliodumu kwa muda mrefu wilayani
Karatu baada ya kuamuru kuwepo kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji
wa huduma ya maji katika Mji huo huku akiagiza bei ya maji inayostahili
kutozwa kwa sasa ni sh1,300 kwa uniti1 badala ya sh,2,000 hadi sh
3,000.
Aweso ameagiza
kuungana kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu
(KARUWASA) na Mamlaka ya Utoaji wa Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU)
na kutengeneza chombo kimoja ambacho kitatoa huduma kwa wananchi kwa
maslahi ya wananchi wa Karatu.
Hatahivyo
waziri Aweso alitamka kwamba Rais Samia Hassan Suluhu ameridhia kutoa
sh,bilioni 4.5 kwaajili ya mradi mkubwa wa maji wilaya hiyo na kuagiza
mamlaka husika zianze kutangaza zabuni ya mkandarasi atakayetekeleza
mradi wa kusambaza maji wilayani humo.
Awesso
amesema hayo leo baada ya kusikiliza maoni ya wananchi na wadau
mbalimbali wa maji wilayani humo ambapo awali kulikuwa na mgawanyiko wa
maslahi ikiwemo Kaviwasu kutoza sh, uniti moja kwa sh,2000 hadi 3000
huku Karuwasa ikitoza sh,1,750 kwa bei za majumbani.
Alisema
uwepo huo wa chombo kimoja kutawezesha maslahi ya wananchi ikiwemo
utoaji wa huduma bora za utoaji maji pamoja na kuhakikisha miundombinu
ya maji haiharibiki.
Alisema
hakuna mtumishi yoyote atakayefukuzwa baada ya kuungana Karuwasa na
Kaviwasa kwa kuwa watakapoungana lita zaidi ya milioni 6 zitakuwepo
ndani ya mamlaka moja ambazo zitakidhi mahitaji ya wakazi wa wilaya
hiyo.
"Wekeni utaratibu
mkandarasi atangazwe aanze kazi ya kusambaza miundombinu ya maji na nyie
wenyewe mtaunda bodi itakayopanga mipango yake kwani maji si biashara
bali ni huduma,tuunganishe mamlaka hizi na utaratibu wa bei uwe ni
sh,1300 kwa uniti 1 kwa kila mwananchi "alisema Aweso
Aliagiza
bei atakayotozwa mwananchi wa kawaida kwa hivi sasa iwe ni sh,1,300 kwa
uniti 1 wakati Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(
Ewura) ikiendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi juu ya
ulipaji wa ankara za maji.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba,alimshukuru Waziri Aweso kwa
kutoa maagizo hayo kwani wananchi watanufaika na bei moja badala ya
awali kuwa na mkanganyiko wa bei kati ya Karuwasa na Kaviwasu
Alisema
baada ya Rais Samia kutangaza filamu ya Royal Tour watalii wamefurika
wilayani Karatu na hivi sasa hoteli zaidi ya 60 zilizopo hapo zinahitaji
maji hivyo aliomba wilaya hiyo kupewa zaidi vipaumbele vya maji ili
kuwezesha kila mtu kunufaika na huduma za maji.
Awali,Ofisa
Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Maji,Jacob Kingazi akisoma mapendekezo ya
kamati iliyoundwa na Waziri Aweso kwaajili ya kufanya tathimini ya hali
ya upatikanaj wa huduma ya maji mji wa Karatu,alisema lazima kuwepo Kwa
chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma katika mji wa karatu
ili kuondoa migogoro.
Kingazi
alisema awali walibaini bodi kuendelea kutekeleza baadhi ya majukumu ya
kiutendaji ilhali ilifikia ukomo mwaka 2019 ikiwemo ukusanyaji wa
ukusanyaji mapato.
Naye
mbunge la jimbo la Karatu, Daniel Awackii alimshukuru Waziri,Aweso kwa
kuunganisha bodi hizo mbili na kuwa moja kwaajili ya kuleta maendeleo
kwa wananchi na kuongeza kuwa hivi sasa watafanya vikao kwa wanachi
kwaajili ya kuwaeleza wananchi kulipa ya bei hiyo ya unit 1,300 kwa kila
mmoja badala ya sh,2000 hadi 3000 zinazotozwa na Kaviwasu
Mwisho.
EmoticonEmoticon