Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23 iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja
Mtumishi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga upande wa Idara ya Elimu Msingi
Waziri Ally akizungumza na waandishi wa habari wakati wakipongeza na
kumshuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara asilimia 23
iliyokwenda sambamba,ajira za watumishi na upandaji wa madaraja
Mtumushi wa Jiji la Tanaga Mwanaidi Mashaka
Na Oscar Assenga,Tanga.
WATUMISHI wa Serikali Mkoani
Tanga wamemshukuru Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara ya
asilimia 23 ambao umekwenda sambamba na upandishaji wa madaraja jambo
ambalo miaka ya nyuma halikufanyika na hivyo kuwawezesha kutekeleza
majukumu yao ipasavyo
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na
waandishi wa habari Jijini Tanga jambo ambalo amelifanya kwao ni kubwa
mno hivyo wanamshukuru na wataendelea kumuunga mkono.
Akizungumza
mmoja wa watumishi hao katika Jiji la Tanga Mwanaisha Shaka alisema
wanamshukuru pia kuwapandisha madaraja kwani wamekaa miaka mingi zaidi
ya sita hadi saba bila kupandishwa madaraja lakini kwa sasa jambo hilo
limefanyika.
“Tumekaa zaidi ya miaka 7 hatujawahi kupandishwa
madaraja lakini sasa Rais Samia Suluhu amepandisha madaraja kwa
watumishi wote sie tupo nyuma yake tutafanya kazi kwa bidii”Alisema
Naye
kwa upande wake mtumishi mwengine Waziri Ally ambaye ni mtumishi wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga Elimu ya Msingi alisema wana mpongeza Rais
kwa mengi aliyoyafanya kwa nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23
imewagusa moja kwa moja wao kama watumishi.
Alisema asilimia 23
sio ndogo wanaweza kufanya jambo kubwa kama watumishi na wana morali wa
kufanya kazi kwa bidii ili kuweza malengo yaliyotarajiwa yanafikiwa.
“Kwa
kweli ninampongeza Rais Samia Suluhu kwa nyongeza ya mshahara na
ongezeko la watumishi sasa tumekuwa wengi na tunafanya kazi bila kuwepo
kwa mzigo mkubwa”Alisema
Hata hivyo kwa upande wake Stella
Siang’a ambaye ni mtumishi wa Jiji Kada ya Elimu alisema kwamba Rais
Samia Suluhu amewafanyia mengi mno jambo la kwanza ni kuongeza
wafanyakazi miaka mingi watu walikuwa hawajaajiriwa walikuwa mitaani
iliyokwenda sambamba na ongezeko la mishahara ambalo litawawezesha
kufanikisha majukumu yao.
Halikadhalika mtumishi mwengine Kasim
Bashiru Lyimo kutoka Idara ya Elimu Sekondari alisema kwamba
wanampongeza Rais Samia ameupiga mwingi kwa mambo mazuri aliyoyafanya
kwa kuweza kuwaongezea asilimia 23 ya mshahara.
“Hili jambo sisi
tumelifurahia sana na tupo pamoja na Rais na tuna hari ya kufanya kazi
na atakapokuwepo mama na sisi tutakuwepo kuhakikisha tunamuunga
mkono”Alisema
Naye kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Mkwakwani Joshua Kiula alisema wana mpongeza Rais Samia
kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ikiwemo kuifungua nchi na
inakwenda na imetulia .
Alisema pia amefanikiwa kufungua
biashara zilikuwa zimefungwa na kurudisha na kuhuisha mahusiani na
mataifa mengine ikiwemo kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupandisha
madaraja.
“Kwa kweli Rais Samia ameupiga mwingi kubwa ni
kupandisha madaraja ambayo ni haki ya Msingi ya wafanyakazi na nyongeza
ya mishahara jambo hilo ni nzuri na limewapa faraja kubwa kwetu”Alisema
Hata hivyo alisema nyongeza hiyo hawakuitegemea kama wataipata
walidhani walipopandisha huo ndio ungekuwa mwisho lakini akaje na jambo
lingine kwao la kuwaongezea asilimia 23 wamelipokea kwa moyo mkunjufu.
EmoticonEmoticon