WANANCHI JIJINI TANGA WATAKIWA KUSAIDIA WATOTO YATIMA

April 17, 2018


WANANCHI Jijini Tanga wametakiwa kuwasaidia watoto yatima wanaolelewa kwenye vituo mbalimbali mkoani Tanga ili kuwaepusha na vishawishi vinavyoweza kuwakuta na kukwamisha ndoto zao za kupata elimu bora ambayo inaweza kuwakomboa kimaisha.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga (CCM) Mustapha Selebosi wakati akifungua bweni Jipya la wasichana katika Taasisi ya Goodwill&Humanity Foundation ambayo imejikita kuwasaidia jamii inayoishi kwenye mazingira magumu na hali duni mjini Tanga.

Alisema lazima jamii itambue kuwa ukiwanusuru watoto wa kike utakuwa umeisaidia familia nzima hivyo umuhimu wa kuwajali kwa kuwaangalia kwa jicho la huruma unahitajika kwa kiasi kikubwa kwao kwa ajili ya kuwawezesha kufikia malengo yao.

“Ndugu zangu lazima tuwaangalie watoto yatima kwa jicho pana kwa lengo la kuwasaidia ili waweze kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo kwani ukimnusuru mtoto wa kike umeinusuru familia na ukiamuacha utakuwa umeiangamizi dunia “Alisema

Hata hivyo aliitaka jamii inayoishi karibu na kituo hicho kuacha kutoa maneno ya kejeli ikiwemo kuwabuguzi watoto hao badala yake washirikiane nao kuweza kutimiza malengo yao ya kuhakikisha wanaishi kwa upendo na amani.

Aliwataka pia wakazi wa Jiji hilo kuwasaidie watoto hao kuwalea kwenye ,misingi ya kiimanio tusiwabuguhudhi kwa maneno ya kejeli kuwa wanasaidiwa,wale ambao hawawatakii mem watoto hao wazibitiwe ambao wanaweza kuiwafanya watoto hao kama wake zao.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Goodwill and Humanity Foundation Shekhe Sayyed Muhdhari alisema taasisi hiyo ilianzishwa kwa lengo la kusaidia makundi ya wasiojiweza ndani ya jamii ikiwemo kuleta usawa baina ya watu wa kaya tofauti.

“Pamoja na hayo ni kusimamia watoto wasiokuwa na wazazi wakulea katika maadili mema pia tulianzisha taasisi hii baada ya kufanya utafiti pamoja na sense ulibaini idadi kubwa ya yatima,wazee,walemavu na wagonjwa waishio kwenye hali duni wakiwa hawana uwezo wa kumudu gharama za matibabu “Alisema.

Kwa upande wake Mlezi wa kulea kituo cha kulea watoto yatima cha Casa Della Gioia Sista Consolata Mgumba aliitaka jamii kuwapenda watoto hao kwa kuwasaidia mahitaji mbalimbali ili waweze kufikia malengo yao.

“Ndugu zangu yoyote anayependa kuwajali watoto yatima anapata Baraka kutoka kwa mwenyezi mungu hivyo nawaasa jamii kubadilika na kuona namna ya kuwaunga mkono waweze kupata malezi bora na elimu “Alisema.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »