KENYA,SHELISHELI KUSHIRIKI BONANZA LA MCHEZO WA BAISKELI JIJINI TANGA

April 04, 2018



WAENDESHA Baiskeli kutoka nchini za Kenya na Visiwa vya Shelisheli wanatarajiwa kushiriki kwenye bonanza la mchezo huo ambalo litafanyika mkoani Tanga mwanzoni mwa mwezi wa sita mwaka huu.

Akizungumza na Tanga Raha Blog, Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli Mkoani Tanga (CHABATA) Dege Masoli alisema licha ya nchi hizo kushiriki lakini pia mikoa mbalimbali ya Tanzania bara nayo itashiriki.

Alisema lengo la bonanza hilo litakuwa ni kunua na kusaka vipaji vya wachezaji wachanga wa mchezo huo ili kuweza kuona namna ya kuwajengea uwezo waweze kuwa wachezaji wazuri siku zijazo.

“Kwa kweli kama unavyojua sisi kama chama tumeona tuanzisha bonanza hili na kuzialika nchi jirani na mikoa kwa lengo la kuweza kuinua mchezo huo mkoani hapa na hili tunadhani linaweza kutupa mafanikio siku zijazo”Alisema Dege Masoli.

Hata hivyo alisema kwenye bonanza hilo zaidi ya wachezaji 300 wanatazamiwa kushiriki ambao watapata fursa ya kuweza kuonyesha vipaji vyao huku akiyaomba makampuni mbalimbali kujitokeza kufadhili.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »