COASTAL UNION KUTUMIA MILIONI 200 KUSAJILI WACHEZAJI

April 04, 2018


MABINGWA wa Ligi kuu soka Tanzania bara mwaka 1988 Coastal Union wanatarajiwa kutumia milioni 200 kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji wa ndani na kigeni ili kuweza kukitumikia kikosi hicho.

Akizungumza na Tanga Raha Blog,Mkuu wa Idara ya habari na Mawasiliano wa timu hiyo,Hafidhi Kidoh alisema wanakusudia kutumia kiasi hicho cha fedha ili kuwea kukithi mahitaji ya kikosi chao msimu ujao.

Alisema fedha hizo ni nyingi hivyo wanakusudia kuangalia namna ya kusaka wadhamini ambao watawasaidia kwenye mchakato huo wa kupata wachezaji watakaowasajili kwa ajili ya kuichezea timu hiyo kongwe hapa nchini.

“Kama unavyojua hivi sasa tupo kwenye harakati za kusajili wachezaji lakini pia kusaka wadhamini ambao watatuwezesha kutimiza malengo hayo kwani kwa makadirio yetu tunatarajia kutumia milioni 200 kusajili Alisema.


Hata hivyo aliwataka wadau mbalimbali kujitokeza kuiunga mkono timu hiyo ili iweze kutimiza malengo yao waliojiwekea ya kushiriki vema michuano hiyo na hatimaye kuweza kuchukua Ubingwa.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »