MARA, tarehe 20 Machi, 2018 – Mkoa wa Mara na Simiyu imezindua kuanza kwa mfumo wa kujitegemea wa usajili wa vizazi ambao unatarajiwa kunufaisha zaidi ya watoto 700,000 walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo.
Uzinduzi huo uliofanyika katika mji wa Musoma, ulihudhuriwa na Mheshimiwa Waziwa wa Katiba na Kisheria Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi, UNICEF na Mwakilishi wa Serikali ya Canada na wageni wengine mashuhuri. Mfumo huo wa usajili uliorahisishwa utasaidia usajili wa watoto wote wachanga na kupunguza idadi kubwa ya watoto ambao hawajasajiliwa walioko chini ya umri wa miaka mitano katika mikoa hiyo miwili.
Mfumo huu ambao unajitegemea usio ratibiwa kutoka serikali kuu unasogeza huduma ya usajili karibu na jamii. Inaanzisha vituo vya usajili katika vituo vya afya, ambavyo vinatoa huduma ya afya ya uzazi na watoto, na kwenye jamii katika ofisi za mtendaji wa kata kuendana na sera ya serikali ya ugawaji wa madaraka kwa serikali mitaa.
Zoezi hili limeziba pengo la mijini na vijijini, kwa kuzipa jamii za pembezoni nafasi ya kusajili watoto wao. Inatatua suala la msingi la upatikanaji na uwezo wa kumudu jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa katika usajili wa vizazi nchini Tanzania.
Kwa kuanza kwa mfumo huo katika mikoa miwili, wazazi wanaweza kufikia kwa urahisi zaidi ya vituo 790 vya usajili kulinganisha na vituo 11 vya usajili vilivyokuwepo awali. Zaidi ya Maafisa Usajili 1,700 wameshapewa mafunzo kwaajili ya kusaidia mchakato wa usajili.
Pamoja na mfumo mpya serikali pia imefuta ada ya usajili na nakala ya kwanza ya cheti cha usajili kinatolewa bure, jambo linalofanya ‘hatua fupi za mchakato wa usajili kwawazazi kupata cheti cha kuzaliwa. Kwa kutumia teknolojia ya simu za mikononi taarifa husafirishwa mara moja kwa njia ya ujumbe mfupi SMS, karahisisha ufuatiliaji wa maendeleo ya usajili hapo kwa hapo .
Mfumo huu wa kujitegemea unarahisisha kwa kiasi kikubwa usajili wa vizazi kwa eneo la Tanzania bara, baada ya kudorora kwa miaka mingi. “Tunabadilisha mfumo kurahisisha watoto na familia kuweza kupata haki yao ya kuwa na cheti cha kuzaliwa," alisema Emmy Hudson Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini(RITA), anayewajibika katika usajili wa matukio muhimu ikiwemo kuzaliwa. Aliongeza kwamba; “Sasa wazazi wanaweza kupokea vyeti vya kuzaliwa kutoka katika kituo husika cha kutolea huduma za afya au kupitia ofisi za mtendaji wa kata kwa wakati. Mfumo huu umewasaidia maelfu ya watoto katika mikoa hiyo ambako mfumo huu unafanyakazi na tunapanga kusambaza mfumo huu katika mikoa yote ya Tanzania bara ndani ya muda mfupi kadri iwezekanavyo.” Aliendelea kuongeza zaidi kwamba, “Serikali ya Tanzania inatambua mchango wa Serikali yaCanada, UNICEF na TIGO kwa mchango wao katika suala hili”.
Mwakilishi wa UNICEF nchini Tanzania Ms Maniza Zaman alisema kwamba "Kila mtoto ana haki ya kupata utambulisho. Mfumo huu mpya unarekebisha kiwango kidogo cha usajili wa uzazi na matokeo yake mamilioni ya watoto wa chini ya miaka mitano ambao walikuwa hawaonekani katika takwimu za taifa sasa watakuwa wanaonekana. Hii itasaidia watoto wengi wa kitanzania kudai haki yao na kulindwa, na serikali itakuwa na takwimu bora zaidi kwaajli ya sera na mipango."
Serikali inatekeleza mfumo mpya tangu 2012 kwa kushirikiana na UNICEF, TIGO na Serikali ya Canada, ambayo inatoa fedha. Kuanza kwa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, utaongeza mikoa 2 ambayo itakuwa ikiongezeka kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Geita, Shinyanga, Mbeya, Songwe, Mwanza, Iringa and Njombe ambayo tayari imeshaanza na kufikia watoto milioni 2 walioko chini ya umri wa miaka mitano.
Serikali ya Canada wanaamini katika haki za watoto, wakiwa wanashikilia kwamba kila mtoto anahitaji ushahidi wa kudumu wa kuzaliwa kwake kwani inatengeneza utambulisho wa mtoto kitaifa na haki zao.
"Usajili wa kuzaliwa unasaidia kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma za kiafya na za kijamii walizonazo kwa kisheria", alisema Ian Myles, Kamishina Mkuu wa Canada nchini Tanzania. “Canada wanajivunia kuunga mkono juhuduza tanzania katika kukuza usajili wa uzazi, kuwasaidia watoto na familia zao kujipatia haki zao za msingi kama wananchi wa Tanzania . Tunafuraha kuona uzinduzi wa mfumo huu mkoani Mara na Simiyu, ikiwa ni mwenyelezo wa mafanikio ya uzinduzi wa mfumo huu katika mikoa ya Iringa, Njombe, Geita na Shinyanga, Lindi, na Mtwara.” Mpaka sasa mfumo huu umezifikia Halmashauri za wilaya 58 katika mikoa 9 ya Tanzania bara.
Msaada wa kifedha kutoka serikali ya Canada umewezesha uanzishwaji wa mfumo endelevu wa usajili wa vizazi yenye lengo la kufikia mamilioni ya wasichana na wavulana walioko chini ya umri wa miaka mitano. Mfumo huu utachangia katika Usajili wa Raia wenye ufanisi na Mfumo wa Takwimu Muhimu katika nchi, ambao unaanzishwa.
TiGO inaunga mkono juhudu hizo kupitia teknolojia ya simu, ambayo inahakikisha kwamba taarifa za usajili ya vizazi unaingizwa na kutumwa kwenye database kuu iliyoko RITA wakati huo huo. TIGO pia inatumia vyombo vya habari kuongeza ufahamu kuhusu umuhimu wa usajili wa uzazi nchini Tanzania.
Akiongea katika sherehe za uzinduzi, Mkurugenza wa TIGOKanda ya Ziwa, Joseph Mutalemwa amesema “kwa pamoja tuna dhamana ya kuhakikisha ustawi wa nchi na wananchi wake. Maamuzi yaTIGO kuunga mkono juhudu hizi inasisitizia jitihada zetu za kujenga mfumo imara wa kijamii ambao uleta ahadi ya teknolojia katika jamii tunakofanyia kazi. Kwa uvumbuzi huu, TIGO inatoa mchango mzuri na mkubwa kwenye Malengo ya Maendeleo Endelevu na kulinda haki za watoto. Kwa kuongezea, ushirikiano huu unadhihirisha nafasi ya kampuni za simu katika kutatua mahitaji ya kijamii kupitia matumizi ya teknolojia yako na ujuzi wao.’