Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akihutubia wajumbe wa
Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda,
Biashara na Mazingira wakati akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa
na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa kuhusu mradi
wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza
umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Na Hamza Temba, Dodoma
.............................. ............................
..............................
Wizara
ya Maliasili na Utalii imeendesha warsha ya siku moja ya kuwajengea
uelewa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na
Utalii na Viwanda, Biashara na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao
unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia
sekta ya Utalii nchini.
Akifungua
warsha hiyo ya siku moja iliyofanyika mjini hapa jana, Waziri wa Wizara
hiyo, Dk. Hamisi Kigwangalla alisema lengo la warsha hiyo ni kuwajengea
uelewa wajumbe hao kuhusu utekelezaji na mafanikio ya mradi huo
unaofadhiliwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na nchi ya
Uswizi kupitia shirika la kiuchumi la State Secretariat for Economic
Affairs-SECO.
Alisema
mradi huo pia unalenga kuongeza ununuzi wa mazao na bidhaa za
mbogamboga na matunda zinazozalishwa Tanzania, kuongeza ajira kwa
Watanzania waliojifunza vema masuala ya utalii, na kuongeza nafasi ya
kujadili dhana ya Utalii Wenye Manufaa kwa jamii.
"Mradi
huu unaratibiwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na
kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Taasisi za Umoja wa
Mataifa zinazohusika na eneo la Maendeleo ya Biashara (UN Trade Cluster
Organizations) - UNIDO, UNCTAD, ITC na ILO, taasisi za Serikali na
zisizo za Serikali, na sekta binafsi" alisema Dk. Kigwangalla.
Alisema
awamu ya kwanza ya mradi huo ilitekelezwa kuanzia mwaka 2014 hadi 2016
ambapo jumla ya Dola za Kimarekani milioni 3.5 zilitumika.
"Awamu
ya pili ya mradi ilianza kutekelezwa mwaka 2017 na utarajiwa kukamilika
mwaka huu 2018. Jumla ya Dola za Kimarekani milioni 1.9 zimetumika
katika awamu hii ya mradi" alisema.
Alisema
mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa katika kuwawezesha wananchi
kiuchumi na kuhifadhi mazingira, na kufanya utafiti wa mazao mbalimbali
ya utalii ambao utawezesha kuandaa Sera na Mikakati mipya ya kukuza
Utalii hapa nchini.
Warsha
hiyo ya siku moja imehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula ambaye pia ni
mjumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimsikiliza Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Wiazara hiyo, Degracious Mdamu muda
mfupi kabla ya kufungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara
yake mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati za
Kudumu za Bunge za Ardhi, Maliasili na Utalii na Viwanda, Biashara na
Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya
wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini. Kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii, Ernest Mwamaja ambaye
aliwasilisha mada katika warsha hiyo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi
ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na
Viwanda, Biashara na Mazingira muda mfupi kabla ya kufungua warsha ya
siku moja iliyoandaliwa na Wizara yake mjini Dodoma kwa ajili ya
kuwajengea uelewa kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha
ya wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Baadhi
ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii na
Viwanda, Biashara na Mazingira wakifuatilia moja ya mada iliyowasilishwa
katika warsha ya siku moja iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii
mjini Dodoma kwa ajili ya kuwajengea uelewa wajumbe hao kuhusu mradi wa
SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya wananchi kwa kupunguza umasikini
kupitia sekta ya Utalii nchini.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula ambaye
pia ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Ardhi, Maliasili na Utalii
akichangia moja ya mada iliyowasilishwa katika warsha ya siku moja
iliyoandaliwa na Wizara Maliasili na Utalii mjini Dodoma kwa ajili ya
kuwajengea uelewa wajumbe wa kamati hiyo na kamati ya Viwanda, Biashara
na Mazingira kuhusu mradi wa SECO ambao unalenga kuboresha maisha ya
wananchi kwa kupunguza umasikini kupitia sekta ya Utalii nchini.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Wizara ya Maliasili na Utalii,
Deograsious Mdamu akitambulisha wajumbe wa meza kuu wakati wa warsha
hiyo.
Baadhi
ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa
ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii
Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Baadhi
ya wajumbe wa kamati hizo wakifuatia moja ya mada iliyokuwa
ikiwasilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Masoko kutoka Bodi ya Utalii
Tanzania, Ernest Mwamaja (hayuko pichani)
Baadhi ya washiriki na wawezeshaji wa warsha hiyo kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.