Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara
na Mazingira Mhe. Innocent Bashungwa akisisitiza jambo kwa watendaji
wa Ofisi ya Makamu wa Rais (hawapo pichani) mara baada ya kupokea taarifa
ya Ofisi ya Makamu wa Rais na kujadili utelekezaji wa Bajeti ya Ofisi
hiyo kwa mwaka fedha 2017/2018 na mapendekezo ya Mapato na Matumizi
kwa mwaka 2018/19. Taarifa iliyowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. Kulia ni
Katibu wa Kamati Bw. Wilfred Magova.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)Mhe.
January Makamba, Naibu Waziri Mhe. Kangi Lugola na Katibu Mkuu
Mhandisi Joseph Malongo wakifuatilia majadiliano ya wajumbe wa kamati
mara baada ya kuwasilisha taarifa yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Viwanda, Biashara na Mazingira, hii leo Mjini Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Kangi Lugola, Katibu Mkuu Mhandisi Joseph Malongo na Naibu Katibu
Mkuu Bi. Butamo Phillip wakifuatilia majadiliano ya wajumbe wa kamati
mara baada ya kuwasilisha taarifa yao kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Viwanda Biashara na Mazingira, hii leo Mjini Dodoma.
Pichani wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na
Mazingira Mhe. Hawa Subira Mwaifunga na Mhe. Omary Ahmed Badwel wakifuatilia
majadiliano katika Kamati yao hii leo Mjini Dodoma.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara
na Mazingira Mhe. Kanali (Mst) Masoud Ali Khamis na Mhe. Zainab Mdolwa
Amiri wakifuatilia majadiliano kikaoni hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba
#Kwa kiasi kikubwa kiwango cha uelewa kwa wananchi
na jamii kwa ujumla juu ya masuala ya mazingira kimeongezeka na Ofisi
ya Makamu wa Rais itaendelea kutoa elimu kwa Umma na suala hili litapewa
kipaumbele
#Ofisi ya Makamu wa Rais inashirikiana na wadau mbalimbali
katika kuhamasisha uwekezaji endelevu na rafiki kwa mazingira.
#Matumizi ya nishati mmbada wa mkaa yanaendea kuhimizwa
ikiwa ni pamoja na matumizi ya gesi na matumizi ya majiko banifu na
matumizi ya tungamotaka (Bio-Mass).
#Zaidi ya Maafisa Mazingira mia tano (500) wameteuliwa
kwa ajili ya kuwa ’wakaguzi wa Mazingira’ambao watafanya kazi kwa
mujibu wa sheria ya Mazingira ya Mwaka 2004 kifungu namba 182 (2)
#Serikali inaendelea kujenga uwezo wa Taasisi ikiwemo
NEMC ili iweze kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa mujibu wa Sheria.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa
Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Kangi Lugola
#Serikali imeanzisha Mfuko wa Mazingira ambao pamoja
na mambo mengine fedha yake itasaidia kampeni kubwa ya upandaji miti
hapa nchini
#Taasisi/Vikundi vinavyojihusisha na masuala ya hifadhi
na usimamizi wa mazingira nchini vinaweza kupewa tuzo ili kutoa chachu
kwa vikundi vingine pia
#Kila Wilaya na Halmashauri zinatakiwa kuanzisha
Sheria ndogo ndogo kwa ajili ya Hifadhi na usimamizi wa Mazingira katika
maeneo yao.
#Serikali imeanza mchakato wa kuandaa orodha ya wachimbaji
wadogo wadogo wote hapa nchini ili uandaliwe utaratibu maalumu wa kuwaratibu
kwa ujumla wao.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe.
Innocent Bashungwa
#Kampeni za kitaifa za Mazingira zinaonekana na vema
juhudi hizi ziendelee kwa kushirikisha wadau wote
#Serikali iangalie upya matumizi ya Mkaa wa kuja
na nishati mbadala ili kunusuru ukataji wa miti unaoendelea kwa kasi,
ikiwa ni pamoja na kushirikiana na SIDO katika kutengeneza majiko banifu
#Usimamizi wa Sheria ya Mazingira uzingatiwe ikiwa
ni pamoja na kuitaka Migodi mikubwa kufuata taka la kisheria la kurudhisha
hali ya mazingira ya awali mara baada ya kukamilika kwa uchimbaji.