Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi (katikati) akisisitiza jambo
wakati akifungua Kikao cha Baraza la wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
lililofanyika tarehe 21Machi, 2018 mjini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akiimba wimbo wa Umoja na
Mshikamano pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo
mjini Dodoma kabla ya kufungua Kikao hicho.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakiimba wimbo wa Umoja na Mshikamano leo mjini
Dodoma kabla ya kufunguliwa kwa Kikao cha baraza hilo .
Katibu wa Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Waziri Mkuu Bi.Flora Bilauri akifafanua jambo wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akimsikiliza Mkurugenzi wa
Sera na Mipango wa Ofisi hiyo Bw.Packshard Mkongwa mara baada ya kufunga
kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa ofisi hiyo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu) Bi. Maimuna Tarishi akifurahia jambo na Katibu wa
TUGHE mkoa wa Dodoma Bw. John Mchenya mara baada ya kufungua kikao cha
Baraza hilo mjini Dodoma.
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi
Ofisi ya Waziri Mkuu Bi. Ernajoyce Hallo akiuliza swali wakati wa
mkutano wa baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo
Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Bunge na Waziri Mkuu)Bi. Maimuna Tarishi (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Ofisi hiyo leo mjini
Dodoma baada ya kufungua Kikao hicho
Mkurugenzi wa Sera na Mipango
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Packshard Mkongwa akiwasilisha mada ya Bajeti ya
Ofisi hiyo kwa Mwaka 2018/19 wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
wa ofisi hiyo
Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi
Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Alex Ndimbo akiuliza swali wakati wa mkutano wa
baraza hilo lililofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi hiyo Dodoma.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
…………………
Na.MWANDISHI WETU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu Bi. Maimuna Tarishi ameongoza
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi hiyo na kuwaasa wajumbe wa
baraza kutoa maoni yatakayosaidia kufanikisha mchakato wa maandalizi ya
Bajeti ya mwaka 2018/2019.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa
Kikao hicho Tarishi amesema kuwa Watumishi wote katika Ofisi hiyo wanao
wajibu wakushiriki kikamilifu katika mchakato wa maandalizi ya bajeti
ili kufanikisha azma ya Serikali kuendelea kutoa huduma bora kwa
wananchi.
“Bila kujali nafasi zenu ni lazima
mtambue kuwa mnao wajibu sawa katika kutoa maoni yatakayosaidia katika
mchakato wa maandalizi ya bajeti” alisisitiza Bi. Tarishi.
Akifafanua Tarishi amesema kuwa
Ofisi yake imekuwa ikizingatia maoni ya wajumbe wa baraza hilo katika
maandalizi ya bajeti hivyo ni wakati mwingine tena kwa watumishi hao
kuhakikisha kuwa wanashiriki kikamilifu katika kikao cha baraza hilo kwa
kutoa mchango utakaosaidia katika utendaji wa Ofisi hasa katika kipindi
hiki cha maandalizi ya bajeti.
Aliongeza kuwa Baraza hilo
linafanyika ikiwa ni utekelzaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yanayotaka Ofisi zote za Serikali kuwapa nafasi
watumishi wake kutoa maoni yao kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo bajeti
kupitia kwenye baraza la Wafanyakazi hali inayochochea maendeleo na tija
katika utoaji wa huduma.
Naye Katibu wa TUGHE mkoa wa
Dodoma Bw. John Mchenya alieleza kuwa Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
wanapaswa kuwa kielelezo katika uwajibikaji na utekelezaji wa majukumu
yao ili kuwa mfano wa kuigwa hususan katika kukilinda na kuhakikisha
uhai wa chama cha Wafanyakazi kwa kutenda haki kwa mujibu wa sheria
zilizopo.
“Ni vyema kila mmoja wenu akawa
wakili mzuri katika utendaji kuzingatia Ofisi hii ndiyo mtendaji Mkuu wa
Shughuli za Serikali bila kuacha kuzingazita uwepo wa TUGHE kwa kuwa
ipo kwa mujibu wa Sheria namba 6 inayoeleza masuala ya ajira na usajiri
wa vyama vya Wafanyakazi”.Alisema Bw.Mchenya
Kwa upande wake mmoja wa wajumbe
wa Baraza hilo Bw.Yona Mwakilembe amesema kuwa maoni ya watumishi
katika Ofisi hiyo yamekuwa yakizingatiwa kwa ukamilifu hali inayoongeza
morali kwa watumishi wa Ofisi hiyo.
“Tangu nimehamia hapa nimeshuhudia
kwa kiwango kikubwa kwamba maoni tunayotoa kupitia baraza la
wafanyakazi yanazingatiwa hivyo ni jambo la kujivunia na tunapongeza kwa
hatua hii” Alisisitiza
Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya
Waziri Mkuu linafanyika mjini Dodoma leo Machi 21, 2018 ikiwa ni sehemu
ya utaratibu wa uliowekwa na Serikali kupitia Wizara, Mikoa, Wilaya,
Idara, Wakala, Taasisi na Mashirika ya Umma kuwapa nafasi watumishi
kutoa maoni yao kupitia baraza la wafanyakazi ili kuongeza tija na
uwajibikaji katika Taasisi husika.