Wateja 84 wajinyakulia simu janja za TECNO R6 na bonasi za data bure baada ya kununua bando za intaneti kupitia *147*00#
- Zaidi ya simu 840 pamoja na bonasi za uhakika za intaneti bado zinashindaniwa!
Dar es Salaam, Machi 9, 2018 – Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, leo imewazawadia washindi 84 wapya wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus simu aina ya Tecno R6 zenye uwezo wa 4G.
Akikabidhi zawadi hizo kwa baadhi ya washindi katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za Tigo jijini Dar es Salaam leo, Mtaalam wa usambazaji Bidhaa wa Tigo, Baraka Hamza alisema kuwa kufikia sasa promosheni hiyo imeibua washindi wa simu 240 kutoka sehemu mbalimbali za nchi.
‘Kila anayenunua bando la intaneti kuanzia TZS 1,000 kupita *147*00# anapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pia anaingizwa kwenye droo ya kushinda mojawapo ya simu zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 zinazoshindaniwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus.’
‘Nina furaha kubwa kupokea simu hii kutoka Tigo, itakayoniwezesha kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki kwa kasi ya juu ya 4G,’ Jasper Dethuel Kimei, mfanyabiashara na mkaazi wa Vingunguti Dar es Salaam alisema baada ya kupokea zawadi yake ya simu.
“Tunawakaribisha wateja wote wa Tigo kuchangamkia fursa hii kwani baio tuna simu 840 zinazozubiri kunyakuliwa katika promosheni hii ya Nyaka Nyaka Bonus,’ alisema balozi wa promosheni hiyo, Meena Ali.
Kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.