Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi
wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akikata
utepe ishara ya uzinduzi wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato,
Leo Machi 2018
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Magufuli
akizungumza na wananchi mbalimbalia Chato waliohudhuria kwenye uzinduzi
wa jengo jipya la Benki ya CRDB tawi la Chato, Leo Machi 2018
Na Mathias Canal, Chato-Geita
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt John Pombe Maguguli Leo 9
Machi 2018 amezindua jengo jipya la Benki ya CRDB Tawi la Chato Mkoani
Geita.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mhe Dkt. Magufuli amesema kuwa uwepo wa Benki hiyo
utarahisisha huduma za uhifadhi fedha kwa wafanyabiashara wa samaki
Wilayani Chato sambamba na wananchi ambao kwa kiasi kikubwa katika msimu
wa Kilimo wamenilima Pamba kwa wingi.
Ameipongeza
Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuzifungia baadhi ya Benki nchini na
kuzipa onyo zingine ambazo zilikuwa zinafanya kazi kwa mazoea na kwenda
kinyume na utaratibu wa sheria za uendeshaji.
Alisema
ni bora kuwa na Benki chache nchini ambazo zinaweza kuwahudumia
wananchi wengi hususani masikini kama ilivyo CRDB ambayo imewafikia kwa
kiasi kikubwa wananchi vijijini hivyo kuendelea kuzifungia Benki zote
ambazo zimeshindwa kuendesha vyema shughuli zake na kusalia kufanya
huduma Jijini Dar es salaam pekee.
Rais
Magufuli ameiomba benki ya CRDB kupunguza riba ya mikopo kwani ni
asilimia 16 pekee ya watanzania ndio wanaohudumiwa kwenye Benki nchini
hivyo ili wananchi wote waweze kukopa na kuweka mitaji yao midogo kwa
ajili ya faida yao ya Sasa na badae ni lazima kuwa na riba rafiki kwa
wananchi.
JPM
ameipongeza Benki hiyo kwa kuajiri wafanyakazi wapatao 3200 tangu
ilipoanza rasmi nchini mwaka 1972 wakati wa utawala wa serikali ya awamu
ya kwanza chini ya hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyeielewa
dhana halisi ya kuwasaidia wananchi vijijini kutokana na usumbufu mkubwa
wanaoupata katika huduma za kifedha.
Alisema
kuwa anayo imani kubwa na Benki ya CRDB kwani naye ni mteja wa benki
hiyo hivyo ili kuendeleza mahusiano mema tayari seikali imelipa Deni
lote la shilingi Bilioni 16 ambalo ilikuwa inadaiwa na benki hiyo
kutokana na mikopo katika miaka ya nyuma.
Katika
hatua nyingine Rais Magufuli amewahamasisha wananchi kutunza fedha zao
benki na kuachana na dhana ya kuhifadhi fedha majumbani jambo ambalo ni
hatari kwa usalama wa fedha hizo na maisha yao wenyewe.
Mhe
Magufuli amesisitiza watanzania kuwa wazalendo huku akisema kuwa
anatambua kuwa wapo baadhi ya wananchi ambao wamesalia na jukumu la
kuandika katika mitandao na vyombo vya habari mambo ambayo ni kinyume na
utendaji wa serikali jambo ambalo ni uchonganishi dhidi ya wananchi na
serikali yao.
Aidha,
Mhe Rais Magufuli alikataa ombi la Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB
Tanzania Dkt Charles Kimei aliyetaka Benki hiyo kuitwa CRDB JOHN POMBE
MAGUFULI-CHATO huku akisema kuwa isalie kuitwa CRDB tawi ka CHATO.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Tanzania, Dkt Charles
Kimei ametoa pongezi kwa Rais Magufuli kwa kukubali kuwa mgeni rasmi
katika uzinduzi wa Benki hiyo huku akielezea namna ambavyo amekuwa na
dhamira ya dhati ya kuwainua watanzania kupitia rasilimali zao jambo
ambalo litawanufaisha na kuwainua kiuchumi.
Alisema
kuwa Benki hiyo itaendelea kubuni njia nzuri za mikopo huku akisisitiza
kuwa Benki hiyo kuendelea kuwasaidia wananchi kupitia SACCOS zao kupata
mikopo nafuu ili kujinufaisha kwa kuwa na uchumi imara utakaowawezesha
kukuza biashara zao.
Sambamba
na hayo pia amekubali ombi la Mbunge wa Jimbo la Chato Mhe Medard
Kalemani ambaye ni Waziri wa Nishati la kujenga uwanja wa kisasa wa
Mpira wa miguu ambapo kwa niaba ya Benki hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya
wadhamini Benki ya CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari amekabidhi Hundi la
Shilingi Milioni 50 kwa ajili ya hatua za mwanzo za kuanza ujenzi wa
uwanja huo huku akiahidi Benki hiyo kuwa wadhamini wa timu ya mpira wa
miguu ya wilaya ya Chato.
Dhifa
ya uzinduzi wa Benki hiyo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwemo Waziri Wa Nishati Mhe Medard M.Kalemani (Mb), Naibu Waziri wa
Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Mb), Mkuu Wa Mkoa Wa Geita Mhandisi
Robert Gabriel, Naibu Waziri Wa fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijazi (Mb),
Naibu Gavana Wa Benki Kuu Tanzania Dkt Bernard Yohana Kibese, Balozi
Wa Denmark nchini Tanzania Mhe Einar Hebogard Jensen, Mwenyekiti wa
Bodi ya wakurugenzi CRDB Tanzania Ndg Martin Mmari, Mkurugenzi Mtendaji
CRDB Tanzania Dkt Charles Kimei, na Wabunge wa majimbo mbalimbali
ikiwemo jimbo la Busanda na Mbogwe.