TAIFA STARS KUCHEZA NA ALGERIA NA DR CONGO MWEZI HUU

March 02, 2018
TAIFA STARS KUCHEZA NA ALGERIA NA DR CONGO MWEZI HUU
Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki mwezi huu wa Machi kwenye tarehe za kalenda ya FIFA.
Taifa Stars itakuwa ugenini nchini Algeria Machi 22,2018 kucheza dhidi ya Algeria kabla ya kucheza na DR Congo Machi 27,2018 Uwanja wa Taifa Dar es Salaam,Tanzania.
Tayari mechi hizo zimethibitishwa na pande zote mbili kuchezwa katika tarehe hizo.

UPANGAJI RATIBA ROBO FAINALI NA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO LA AZAM WAFANYIKA
Upangaji wa ratiba kwa hatua ya robo fainali na nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Shirikisho la Azam umefanyika leo Ijumaa Machi 2, 2018 kwenye Makao Makuu ya Azam Tv.
Droo hiyo imehusisha timu saba za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na timu moja ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara.
Timu zilizochezeshwa kwenye droo hiyo ni Young Africans,Azam FC,Singida United,Tanzania Prisons,Njombe Mji,Stand United,JKT Tanzania na Mtibwa Sugar.
Mechi za hatua hiyo zitapangiwa tarehe ya kuchezwa baada ya tarehe za awali kuingiliana na mechi za timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 zilizotajwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa CAF.
Ratiba Nane bora
Singida United vs Young Africans          Uwanja wa Namfua
Tanzania Prisons vs JKT Tanzania          Uwanja wa Sokoine
Azam FC vs Mtibwa Sugar                      Azam Complex
Stand United vs Njombe Mji                 Uwanja wa Kambarage
Nusu Fainali
Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa
Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania
Fainali
Singida United/Young Africans vs Tanzania Prisons/JKT Tanzania vs Stand United/Njombe Mji vs Azam FC/Mtibwa

LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA MZUNGUKO WA 20 KUENDELEA KESHO
Mzunguko wa 20 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara unaendelea kesho Jumamosi Machi 3,2018 kwa kuchezwa mechi nne.
Njombe Mji watakuwa nyumbani Uwanja wa Sabasaba kucheza na Ruvu Shooting mchezo utakaochezwa saa 8 mchana wakati Kagare Sugar wao watakuwa nyumbani Uwanja wa Kaitaba kuwakaribisha Majimaji ya Songea mchezo utakaochezwa saa 10 jioni.
Mechi nyingine Tanzania Prisons ya Mbeya watakuwa nyumbani Uwanja wa Sokoine kucheza dhidi ya Mbao FC ya Mwanza saa 10 jioni,Azam FC watakuwa Azam Complex ikiwakaribisha Singida United saa 1 jioni.
LIGI KUU YA WANAWAKE YA SERENGETI PREMIUM LITE HATUA YA NANE BORA KUENDELEA KUTIMUA VUMBI KESHO
Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Premieum Lite hataua ya Nane bora inataraji kuendelea kesho Jumamosi Machi 3,2018 na Jumapili Machi 4,2018.
Jumamosi,Machi 3,2018  
Panama FC vs JKT Queens        Uwanja wa Samora
Jumapili Machi 4,2018
Simba Queens vs Evergreen       Uwanja wa Karume
Mlandizi vs Kigoma                    Uwanja wa Mabatini
Baobab vs Alliance                      Uwanja wa Jamhuri
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »