Katibu
Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE), mkoa wa Dar es
Salaam, Bw. Gaudence Kadyango aliyekuwa msimamizi wa uchaguzi wa Chama cha
Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE)
tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), akitoa
maelezo kwa wapigaji kura kwenye uchaguzi mdogo wa tawi hilo uliofanyika leo
kwenye ukumbi wa Transit uliopo Jengo la Kwanza la abiria(TBI).
Bw.
Filbert Lyimo akijinadi katika nafasi ya Uenyekiti katika uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNIA) uliofanyika leo katika ukumbi wa Transit uliopo jengo la kwanza
la abiria (TBI)
Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Johannes Munanka (wa kwanza kulia), akifuatilia kwa makini zoezi la uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la kiwanja hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa Transit uliopo jengo la kwanza la abiria (TBI).
Msimamizi wa uchaguzi mdogo wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bi. Honesta Ngowi kutoka Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana (kulia) akishughudia wanaohesabu kura za nafasi ya ujumbe wa TUGHE katika uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Jengo la Pili la abiria (TBII).
Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali
na Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
wakihesabu kura za nafasi ya Uenyekiti Kamati ya Wanawake, katika uchaguzi
uliofanyika kwenye ukumbi wa Transit wa Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Na
Mwandishi Wetu
WENYEVITI
Bw. Filbert Lyimo na Bi. Anna Myovela wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na
Afya (TUGHE) tawi la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA),
wameahidi makubwa katika kutetea haki za wanachama wao mara baada ya
kuchaguliwa leo kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katika ukumbi wa Transit
uliopo Jengo la Kwanza la abiria (TBI).
Bw. Lyimo aliyechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa TUGHE
tawi la JNIA alisema atahakikisha anawawakilisha vyema wanachama kwa mwajiri,
ikiwemo kutetea haki na maslahi yao ya kazi.
“Nashukuru
kwa kunionesha ushirikiano nyie ndio mlionichagua mimi na sio mimi
niliowachagua nyie, hivyo ninaahidi sintawaangusha nitakwenda kifua mbele
kutetea haki zenu kwa mwajiri, na jambo la msingi tushirikiane ili kufanikisha
haya ninayoyatarajia,” alisema Bw. Lyimo.
Pia
amewakumbusha wafanyakazi wote ambao bado kujiunga kwenye chama cha Wafanyakazi
sehemu ya Kazi, wafanye hima na wajiunge ili nao wapate haki za kutetewa endapo
watapata matatizo mbalimbali.
Naye
Bi. Myovela aliyechaguliwa katika nafasi ya Uenyekiti Kamati ya Wanawake alisema
atahakikisha anawatumikia wanachama wote bila kujali umri, dini wala kabila,
ambapo amesisitiza hatakuwa na urafiki kwa yeyote atayekwamisha jitihada zake hizo.
“Naomba
ushirikiano wenu mkubwa ili tujenge TUGHE mpya ninayoamini itafanya vizuri
kutetea wanachama wote,” alisema Bi. Myovela.
Hata
hivyo katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani
Bw. Lyimo alishinda kwa kishindo kwa kura 39 na kuwashinda Simon Mbogo
(32) na Victor Mabote (3).
Naye
Bi. Myovela alipata kura 24 na kuwashinda Rehema Ambari aliyepata kura 17,
Mwanahawa Mdee kura moja na Yusta Swebe hakupata kitu.
Kwa
upande wa ujumbe Bw. Steven Ntambi alishinda kwa kura tisa, huku mpinzani wake
Bi. Ambari akiambulia kura tano.
Uchaguzi
huo umefanyika wa kuziba mapengo baada ya aliyekuwa Wenyeviti Bw. Abbas
Rweyumamu, na Bi. Simai Ngasani kuhamishwa kituo cha kazi cha JNIA na kupelekwa
Makao Makuu, huku Bw. Ntambi akijaza nafasi ya ujumbe iliyoachwa na Lyimo.
Hata
hivyo kwa nyakazi tofauti wasimamizi wa uchaguzi huo, Katibu Mkuu wa TUGHE Mkoa
wa Dar es Salaam, Bw. Gaudence Kadyango na Bi. Honest Ngowi kutoka Wizara ya
Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana waliwataka viongozi waliochaguliwa kuhakikisha
wanaongeza idadi ya wanachama ili kuzidisha mshikamano sehemu ya kazi.
Uongozi
mzima wa TUGHE-JNIA ni Lyimo (Mwenyekiti), Thawabu Njeni (Katibu), Anna
(Mwenyekiti wanawake), Mastidia Ndyomulwango (Katibu Kamati ya Wanawake),
Mwanaisha Athuman (Kamati ya Vijana), Kidiga Baltazar (Kamati ya Walemavu),
huku wajumbe ni Sadic Milulu, Theobald Beng’inus, Mwanaheri Omar, Adventina
Rugimbila, Hussein Msuya, Ntambi na Mbogo.