Wakazi Mwananyamala wavutiwa na huduma za 'One Stop Centre' za CRC

February 12, 2018
Mwanasheria wa Kituo cha Usuluhishi–CRC, Suzan Charles (kulia) akitoa huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jana jijini Dar es Salaam.

Afisa wa Polisi na Mratibu wa Kituo cha One Stop Center (OSC) Amana, Bi. Christina Onyango (kulia) akimsikiliza mmoja wa wateja waliofika kupata huduma leo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam.

Mmoja wa wahudumu wa afya kwenye kituo hicho akitoa huduma kwa mmoja wa wateja waliofika kupata huduma.


Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.

Shughuli za utoaji huduma kwa baadhi ya wateja waliojitokeza kwenye zoezi la utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwa waathiriwa wa matukio ya ukatili wa kijinsia pamoja na huduma zingine muhimu kwa kundi hilo Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam zikiendelea.


Na Mwandishi Wetu

BAADHI ya wananchi wanaoishi Mwananyamala 'A' jijini Dar es Salaam wamevutiwa na huzahuduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ namsaada wa ushauri kisheria zilizotolewa jana na Kituo cha Usuluhishi – CRC.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi waliopata huduma hizo kwenye Ofisi yaMtendaji Kata ya Mwananyamala 'A' walisema wamefurahishwa na kitendo cha CRC kusogezahuduma hizo eneo lao jambo ambalo limewavutia wakazi wengi.

"...Binafsi nimevutiwa na kitendo cha huduma kama hii kutolewa eneo letu, mimi nilikuwa nakesi kuna mtu anataka kunidhulumu kiwanja kesi yangu inaendelea lakini baada ya kuona
kuna huduma hizi nimekuja kupata msaada wa kisheria na nimeshauriwa cha kufanya...,"alisema Bi. Nzela Khamis akizungumza mara baada ya kuhudumiwa.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii wa Kituo cha Usuluhishi – CRC, Bi. Violeth Chonya akizungumza na mwandishi wa habari hizi eneo la tukio alisema Mwananyamala kumekuwa namuitikio mkubwa kwa wananchi kujitokeza kupata huduma za pamoja kwa waathirika kwavitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’.

Alisema jumla ya kesi 31 wamezisikiliza na kufikia hatua mbalimbali huku kesi mbili zamatuzo kwa watoto zikitatuliwa baada ya kukutanishwa pande zote mbili na wazazi kufikiamuafaka juu ya mvutano wao.

Bi. Chonya alisema kwa muitikio wa wananchi wa leo umeonesha kuna uhitaji mkubwa wa

huduma hizo hivyo kuwashauri wananchi wa Mwananyamala kujitokeza tena kesho ambapohuduma za pamoja kwa waathirika kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia ‘One Stop Center’ naushauri wa kisheria utatolewa.

"...Kimsingi bado uhitaji ni mkubwa hivyo tunawashauri kesho wananchi wanaohitaji hudumahizi wajitokeze tena kesho tunaendelea kutoa huduma zetu, na baadhi ambao watashindwa
uja kesho wanaweza kuja ofisi za TAMWA Sinza Mori kwenye ofisi zetu (CRC) watahudumiwapia," alisema Bi. Chonya.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »