Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha akishiriki kwenye zoezi la kuteketeza nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa jina la operesheni Sangara zikiteketezwa kwa moto kulia mwenye suti ni Katibu Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana Budeba akishuhudia,Picha na John Mapepele
Katibu
Mkuu wa Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Sekta ya Uvuvi, Dkt. Yohana
Budeba ametaifisha na kuteketeza zaidi ya tani mia mbili za shehena
ya nyavu haramu za uvuvi zenye thamani ya shilingi bilioni 2.6 zilizokamatwa
katika maghala mbalimbali jijini Mwanza leo na kikosi kazi maalumu kilichoundwa
na Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Luhaga Mpina kutokomeza uvuvi haramu
kwenye operesheni maalum inayoendelea Kanda ya Ziwa Victoria iliyopewa
jina la operesheni Sangara .
Mbali
na kuteketeza zana hizo haramu, Serikali pia imekusanya zaidi ya shilingi
bilioni tano kama sehemu ya adhabu kwa wavuvi na wafanyabiashara
waliokutwa na zana haramu pamoja na makosa ya utoroshaji mwani, samaki
na mazao yake nje ya nchi.
Akizungumza
na mamia ya wavuvi wakati wa kuteketeza nyavu hizo leo, katika dampo
la Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza, Dkt. Budeba amesema hatua
hizo kali zinazochukuliwa na Serikali dhidi ya uvuvi haramu hazilengi
kuwaonea wafanyabiashara au wavuvi wanyonge bali zimelenga kuwatengenezea
maisha bora ya kizazi cha sasa na baadae ili kiweze kunufaika na rasilimali
zilizoko ziwani.
Aidha
Dkt. Budeba amesisitiza kuwa kikosi hicho kitaendelea na operesheni
hiyo bila kuchoka hadi hapo uvuvi haramu na utoroshaji wa mazao ya uvuvi
utakapokwisha ndani ya ziwa hilo.
Pia
aliwaonya wamiliki wa viwanda na wafanyabiashara wanaotengeneza
na kuuza nyavu hizo ambapo amesema Serikali ikiwabaini itawachukulia
hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafutia leseni zote
za biashara zao.
Alisema rasilimali zilizopo ndani ya ziwa hili ni mali ya wananchi
viongozi wamepewa dhamana ya kuongoza kazi ya ulinzi tu na endapo uvuvi
haramu utakomeshwa wananchi ndiyo watakaonufaika.
Pamoja
na kuteketeza nyavu hizo haramu, Dkt Budeba alieleza hali ya upatikanaji
wa samaki aina ya sangara katika Ziwa Victoria ambapo alisema kwa mujibu
wa utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) mwaka 2017 unaonesha kuwa samaki waliochini ya sentimita 50 ni asilimia
96.6 hivyo samaki hawa ni wachanga na hawarusiwi kuvuliwa ambapo
samaki walio zaidi ya sentimita 85 ni asilimia 0.4 tu ambao ni wazazi
na hawarusiwi kuvuliwa pia. Samaki wa sentimita 50 mpaka 85 ambao ndio
wanafaa kuvuliwa ni asilimia 3 tu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Uvuvi wa Wizara ya Mifugo
na Uvuvi, Fatma Sobo amesema Idara itaendelea kutumia Sheria ya Uvuvi
namba 22 ya mwaka 2003 na Kanuni zake za mwaka 2009 pamoja na Sheria
nyingine za Mazingira ili kudhibiti Uvuvi haramu nchini.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha alisema Serikali ya Wilaya
hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na uvuvi haramu na
kuwachukulia hatua stahiki kuwataka wananchi kuendelea kuwafichua wavuvi
haramu ili kulinda rasimali hiyo muhimu waliyopewa na Mungu.
Kwa upande wao baadhi ya
wavuvi walimuomba Dkt. Budeba kuwasiliana na Wizara ya Viwanda na Biashara,
ili kuona namna ya kudhibiti nyavu zisizoruhusiwa ambazo zinatengenezwa
viwandani na baadae kuuziwa wavuvi.
Hivi karibuni watendaji
wakuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na kikosi
kazi kilichoundwa na Mheshimiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi wameweza
kukamata nyavu haramu, meli za uvuvi kutoka nje ya nchi zinazovua
bia kufuata taratibu na mazao ya uvuvi yanayotoroshwa nje ya nchi ikiwemo
mwani na samaki yenye mabilioni ya fedha huku Waziri Mwenye dhamana
ya sekta hiyo Luhaga Mpina kuahidi kuwa operesheni hizo zitakuwa
za kudumu hadi uuvi haramu utakapokoma.