Na Tiganya Vincent
WANAVYUO
Mkoani Tabora wameagizwa kuhakikisha kuwa wanatumia elimu wanayopata
kuwa mabalozi watakaosaidia katika kuzuia uharibufu wa mazingira na
kuwahimiza jamii kujenga utamaduni wa kupanda miti mipya na kulinda
iliyopo kwa ajili ya manufaa yao ya sasa na baadae.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
wakati alipowaongoza wanavyuo kutoka Vyuo mbalimbali katika upandaji
miti ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kuhakikisha kila mtu anashiriki
katika zoezi hilo.
Alisema
kuwa wasomi kama wanavyuo wakiwa mstari wa mbele katika utoaji wa elimu
katika maeneo yao yanayowazunguka na sehemu za baadae watakazopangiwa
kazi ipo nafasi ya kuzuia uharibifu wa mazingira ikiwemo mistu kuendelea
kuharibiwa.
Mwanri
alisema kuwa jamii inawategemea sana wasomi katika kutoa elimu katika
hatua ya awali ya kuzuia uharibifu kabla ya masuala mengine kama
matumizi ya nguvu za dola hayafanyika katika kuzuia uharibifu
usiendelee.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa kitendo cha wanachuo hao kuomba kuweka
alama katika Mkoa wa Tabora kinapaswa kuwa mwanzo kwao katika katika
kupeleka elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ya jamii inayowazunguka ili
wananchi wengi waweze kutambua umuhimu wa kutoharibu mazingira na
vyanzo vya maji.
Naye
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa
Tabora Idd Moshi aliwataka Wanachuo kuunga mkono juhudi za Mkuu huyo wa
Mkoa wa kutaka kuigeuza sehemu ya kijana kwa kupanda miti miti na
kurudisha uoto wa asili.
Alisema
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora anafanyakazi nzuri ya kuhakikisha
anasimamia agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha mikoa yote hapa nchini inapanda miti
mingi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Moshi
alisema kuwa wanachuo na jamii kwa ujumla wanalojukumu la kuhakikisha
kuwa wanaunga mkono viongozi kwa kupanda miti sio katika maeneo ya umma
katika maeneo wanayoishi.
Alisema
kuwa wao wakiwa vijana wa CCM mkoa wa Tabora wameshapanda miti katika
Wilaya ya Igunga , Nzega, Sikonge na Urambo katika kuunga mkono juhudi
za viongozi wa Mkoa na Kitaifa.