Na Grace Michael, Geita
MKUU
wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel ameupongeza Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) kwa namna ulivyojipanga na unavyoshirikiana na
Uongozi wa Mikoa mbalimbali kwa lengo la kuimarisha na kuboresha huduma
za matibabu nchini.
Pongezi
hizo amezitoa leo wakati akipokea msaada wa vifaa mbalimbali
vilivyotolewa na Mfuko katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Simiyu.
“NHIF
nawapongeza sana kwa namna ambavyo mmekuwa tayari wakati wote
kuhakikisha huduma za matibabu zinakuwa bora zaidi na niwahakikishie tu
kwamba Mkoa umejipanga kutoa huduma kwa wananchi ambazo ni za kiwango
cha juu kwani kama viongozi tuna deni la kuwatumikia Watanzania,”
anasema.
Injinia Gabriel aliutaka Mfuko kutochoka kutoa misaada kama hiyo ambayo inalenga kuwanufaisha wananchi moja kwa moja.
Alisema
kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Pombe John
Magufuli imedhamiria kusogeza huduma kwa wananchi hivyo Mkoa unatekeleza
miradi mbalimbali ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za matibabu ili
kuondokana na changamoto za huduma za afya.
Akikabidhi
msaada huo, Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti, Bi. Anjela Mziray
alisema jukumu kubwa la Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ni kurahisisha
upatikanaji wa huduma za matibabu kwa Watanzania kupitia mfumo wa bima
ya afya.
“NHIF
inayo mipango mbalimbali ya kuhakikisha huduma za matibabu zinawafikia
wanachama na wananchi kwa ujumla katika mazingira ambayo ni bora zaidi,
mipango hiyo ni pamoja na mpango wa Mikopo ya vifaa tiba na ukarabati wa
majengo ya vituo vya kutolea huduma ambayo ni mikopo nafuu inayosaidia
kwa kiwango kikubwa kuboresha huduma za matibabu,” anasema.
Alisema
kuwa NHIF pia imekuwa na mipango mingine ikiwemo ya kupeleka Madaktari
Bingwa katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa
huduma za kitalaam katika maeneo yote ambapo Mkoa wa Geita ni moja ya
Mikoa ambayo imeshanufaika na mpango huo.
Alitumia
fursa hiyo kuuomba uongozi wa Mkoa hususani wa Hospitali kuhakikisha
unaunga juhudi za Mfuko kwa kuhakikisha unatoa huduma bora kwa wanachama
wake na kutatua kero ambazo wamekuwa wakizipata wakati wa kupata huduma
hizo.
Bi.
Mziray kwa niaba ya Uongozi wa Mfuko alikabidhi Vitanda 20, Magodoro 20
pamoja na mashuka 80 kwa hospitali hiyo ambayo ilikuwa na uhitaji wa
vifaa hivyo.
Wakizungumza
kwa nyati tofauti wanachama wa Mfuko waliokuwa hospitalini hapo
walisema kuwa, huduma wanazopata kupitia kadi za matibabu za NHIF ni
nzuri ambazo zimewaondolea usumbufu wa kutafuta fedha wakati wanapopatwa
na magojwa.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi.
Anjela Mziray akionesha vifaa vya msaada vilivyotolewa na Mfuko huo
katika Hospitali Teule ya Mkoa wa Geita kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita
Injinia Robert Gabriel.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akipokea vitanda 20, magodoro 20 na mashuka 80 msada ambao umetolewa na NHIF.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akikalia kitanda kwa lengo la kukagua ubora wake.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel akichunguza kitanda hicho na kuangalia ubora wa mashuka yaliyokabidhiwa.
Baadhi ya Watumishi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa katika hafla ya kukabidhiwa kwa vifaa hivyo.
Meneja wa Mkoa wa Geita wa NHIF, Dk. Mathias Sweya akielezea shughuli zinazofanywa na Mfuko mkoani humo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bi.
Anjela Mziray akizungumza na Mama ambaye ni mmoja wa wanachama wa Mfuko.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Injinia Robert Gabriel wakiwa na Maofisa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.