Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua mabweni mawili ya
Magufuli na Majaliwa katika Shule ya Sekondari ya Bumagi wilayani
Butiama Januari 20, 2018. Watatu kulia ni mkewe Mary.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiwasalimia wananchi baada ya kuzindua mabweni
mawili yaliyopewa majina ya Magufuli na Majaliwa katika shule ya
Secondari ya Bumagi wilayani Butiama Januari 20, 2018. Wapili kushoto
ni mkewe Mary.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Butiama, Nimrod Mkono
(katikati) na mkewe Marylouise Januari 202018,kabla ya kumkabidhi
mbunge huyo cheti cha shukurani kilichotolewa na wilaya ya Butiama ili
kuthami mchango wake mkubwa wa kujenga na kuchangia maendeleo ya elimu
wilayani humo. Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Chuo Kikuu cha
Julius Kambarage Nyerere ambacho kilichojengwa na mbunge huyo kikiwa ni
sekondari na kutokana na ubora wake kilibadilishwa kuwa Chuo Kikuu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mbuge wa Butiama, Nimrod Mkono cheti
cha shukurani kilichotolewa na wilaya ya Butiama ili kuthami mchango
wake mkubwa wa kujenga na kuchangia maendeleo ya elimu wilayani humo.
Makabidhiano hayo yalifanyika kwenye Chuo Kikuu cha Julius Kambarage
Nyerere kilichojengwa na mbunge huyo kikiwa na sekonda na kutokana na
ubora wake kilibadilishwa kuwa Chuo Kikuu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa
Sospeter Muhungo katika mkutano wa hadhara aliouhutubia kwenye kijiji
cha Muragi Januari 21, 2018.
Wananchi
wa Kijiji cha Muragi wilayani Musoma Vijijini wakimshangilia Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika
kijiji hicho Januari 21, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi na viongozi wa mkoa wa
Mara katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku saba mkoani humo
kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkoa wa Mara mjini Msoma Januari 21, 2018.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiaagana na viongozi wa mkoa wa Mara kwenye
uwanja wa ndege wa Musoma baada ya kukamilisha ziara ya siku saba mkoani
humo Januari 21, 2017. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza alikopitia akitoka Musoma
kwenda Dar es salaam Januari 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).