Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika Jengo la Sukari
House lenye Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma kwa
ajili ya kuwasilisha Fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa
Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna wa
Maadili, Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold
Nsekela mara baada ya kuwasili katika Makao Makuu ya Ofisi za
Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio
Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha wageni mara
baada ya kuwasili katika Makao makuu ya Ofisi za Sekretarieti ya Maadili
ya Viongozi wa Umma zilizopo katika Mtaa wa Ohio Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasilisha fomu zake za Tamko
la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa Umma kwa Kamishna wa Maadili,
Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela
katika Makao makuu ya ofisi hizo yaliyopo katika Mtaa wa Ohio jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kamishna wa Maadili,
Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela
mara baada ya kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa
Viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya
kuwasilisha fomu zake za Tamko la Rasilimali na Madeni kwa Viongozi wa
Umma katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini
Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwepo
katika jengo la Sukari House wakati akitoka katika katika Ofisi za
Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Kamishna wa Maadili,
Sekretarieti ya Maadili wa Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela
wakati akitoka katika Jengo la Sukari House lenye Ofisi za Sekretarieti
ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiondoka katika jengo la Sukari
House jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi walio
simama kando ya barabara inayopita mtaa wa Ohio wakati akitoka katika
Ofisi za za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma jijini Dar es
Salaam. PICHA NA IKULU