Na Beatrice Lyimo, MAELEZO-DODOMA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amehamia rasmi Makao Makuu ya Nchi Dodoma leo ikiwa ni utekelezaji wa
agizo la Rais Magufuli alililitoa tarehe 25, Ju.
Akizungumza
wakati wa halfa ya kumkaribisha, Makamu wa Rais amesema kuwa mpaka sasa
ni mwaka mmoja na nusu tangu tamko la kuhamia Dodoma litolewe hivyo
Serikali ipo na inatekeleza majukumu yake.
“Siku
ya leo ilikuwa mawazoni mwangu, ninafurahi imefika na pia ninamshukuru
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kwa maandalizi mazuri ya kunipokea ” Alisisitiza
Mhe. Samia.Aidha, Mhe. Samia amesema kuwa Ofisi yake imekuja na agenda
ya kuifanya Dodoma kuwa ya kijani hivyo wameandaa programu mbalimbali
ikiwemo ya upandaji miti .
“Tarehe
21, Disemba mwaka huu kutakuwa na shughuli ya upandaji miti hivyo
tunaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma kutuunga mkono ili kuweza kutimiza
azma hii” ameongeza Mhe. Samia.Kwa upande wake, Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa amesema kuwa Baba wa Taifa aliweka nia ya Serikali kuhamia
Dodoma tangu mwaka 1973 na leo Serikali ya Awamu ya Tano imetimiza ndoto
hiyo.
“Tunaendelea
kuamini kwamba tamko la Rais linatekelezeka ambapo mpaka sasa watumishi
2816 tayari wameshahamia Dodoma na wanaendelea kutoa huduma za Serikali
na kuanzia Februari mwaka 2018 tunaendelea kupokea watumishi wengine”
amefafanua Waziri Mkuu.
Naye
aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Pancras
Ndejembi ameishukuru Serikali ya Awamu ya Tano kwa kutimiza historia ya
Mwalimu Nyerere ya Dodoma kuwa Makao Makuu.
“Sikuwaza
kama kuna siku Makao Makuu yatakuwa Dodoma kwa sababu siku nyingi mambo
haya yanazungumzwa sasa yamekamilika kwa vitendo, leo nina furaha sana
kuona ndoto ya tangu mimi kijana imetimia” ameongeza Mzee Ndejembi.
Kwa
upande wake Balozi Job Lusinde amesema kuwa “leo Makamu wa Rais anahamia
Dodoma, kweli Mungu hupanga na Mungu huweka wakati wake, leo imekuwa”.
Mbali
na hayo Balozi Job Lusinde amesema kuwa Makamu wa Rai amekuja kipindi
ambacho Mkoa wa Dodoma unaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kulima,
hivyo kumpatia jina la kabila hilo “Mbeleje” likimaanisha kipindi cha
kuandaa mashamba.
Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwa na na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
pamoja na Waziri Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba
wakicheza ngoma ya Mwinamila wakati wa Makaribisho ya Makamu wa Rais
Mkoani Dodoma leo Desemba 15,2017.PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU