Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, alipokuwa anamueleza
nia ya Kampuni hiyo kuwekeza mkoani Dodoma, alipomtembelea Dkt. Mpango
ofisini kwake mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akimsikiliza Kamishna Msaidizi-Sera,
Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Shogholo Msangi akifafanua jambo wakati
Waziri Mpango, alipokutana na kufaya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto Jarrin, uliofanyika katika
ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin, akifafanua jambo wakati wa
mkutano kati yake na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor
Mpango (Mb) (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo
mijini Dodoma.
Watumishi kutoka Wizara ya Fedha
na Mipango wakichukua kumbukumbu wakati wa mkutano kati ya Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw. Roberto Jarrin (hawapo
pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akizungumza wakati wa mkutano kati yake
na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Bw. Roberto
Jarrin (hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo mijini
Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Bia Tanzania-TBL, Bw. Roberto Jarrin, (katikati) akifafanua jambo
alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Mjini Dodoma.
Waziri
wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia),
akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Bw.
Roberto Jarrin, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika
ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Dodoma.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Fedha na Mipango
………..
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amekutana na kufanya
mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia-TBL, Bw. Roberto
Jarrin ambaye ameahidi kuwa kampuni yake itajenga kiwanda kikubwa cha
bia kitakachogharibu takriban dola milioni 100 za Marekani, mkoani
Dodoma.
Jarrin
ameeleza kuwa hatua hiyo inalengo la kuunga mkono juhudi za Serikali ya
Awamu ya Tano za kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa viwanda.
Amesema
kuwa mafanikio makubwa ambayo kampuni yake imeyapata hapa nchini hasa
baada ya kubadilisha ujazo wa kinywaji chake kimoja umeifanya Kampuni
yake ifikirie kuongeza uzalishaji kwa kuongeza kiwanda kingine mkoani
humo.
Bw.
Jarrin amebainisha kuwa upanuaji wa huduma zake nchini utakwenda
sambamba na kuendeleza kilimo cha mazao yanayotumika kutengenezea
vinywaji hususan shayiri ama ngano hatua ambayo itawanufaisha wakulima
nchini.
Akizungumza
katika kikao hicho, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
ameuelezea mpango huo wa TBL kwamba utachochea ukuaji wa uchumi na ajira
kwa wananchi.
“Tunataka
kujenga Tanzania ya viwanda, na TBL ni kiwanda ambacho kitanipa ajira
kwa Watanzania, kitanipa kipato zaidi, lakini pia nataka Dodoma iwe
kitovu kingine cha uchumi kwa kutupatia mapato kama ilivyo Dar es Salaam
inayochangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato ya Serikali” alisema Dkt.
Mpango.
Ameunda
timu ya wataalamu itakayopitia na kuchambua masuala mbalimbali ya
kikodi na kisera yaliyowasilishwa na kampuni hiyo ili yafanyiwekazi
haraka kwa manufaa ya pande hizo mbili.
“Ameahidi
kuwekeza kiwanda chenye thamani ya Dola milioni 100 na ili aweze
kufanya hivyo amehitaji ajue msimamo wa Serikali kuhusu kupunguza
gharama za uendeshaji ikiwemo kodi na mambo mengine ambayo
tutayafanyiakazi” Alisisitiza Dkt. Mpango
Dkt.
Mpango amesema kuwa ameweka utaratibu wa kukutana na wawekezaji wengine
wanaozalisha vinywaji baridi na vikali ili kufungua wigo zaidi wa
majadiliano ili kukuza uwekezaji hapa nchini kwa kuangalia na
kujadiliana kuhusu vikwazo na changamoto zinazoikabili sekta hiyo.