Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa
Mazao cha TARAKEA kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Kituo cha Ukaguzi wa
Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisikiliza maelezo ya utendaji kazi katika Kituo cha Ukaguzi wa
Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha Ukaguzi wa
Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akifungua bomba ili kuona kama maji
yanatoka wakati akikagua maabara ya upimaji wa mazao katika Kituo cha
Ukaguzi wa
Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya.
Picha ya pamoja kati ya wafanyakazi wa Kituo cha Ukaguzi wa
Mazao cha HOLILI kilichopo Katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro
Mpakani Mwa Tanzania na Kenya na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni Ofisi za
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mara baada ya kuwasili katika Kituo cha
Ukaguzi wa
Mazao cha TARAKEA.
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mathew John Mtigumwe Leo Novemba 11, 2017 ametembelea Vituo vya
ukaguzi wa mazao vilivyopo Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro ili kujionea
ufanisi wa utendaji kazi sambamba na kubaini Changamoto zinazowakabili ili
kuongeza tija katika ukusanyaji wa ushuru.
Katika ziara hiyo ya kikazi Mhandisi
Mtigumwe ametembelea Kituo cha HOLILI na TARAKEA ambavyo vipo upande wa
Tanzania ikiwa ni mpakani mwa Tanzania na Kenya.
HOLILI ni moja ya mpaka kati ya
Tanzania na Kenya ambalo upo umbali wa takribani Kilomita 25 Kutokea Himo
Njiapanda huku Mpaka wa TARAKEA ukiwa umbali wa Takribani Kilomita 58 kutokea
Himo Njiapanda.
Miongoni mwa Changamoto alizozibaini
katika ziara hiyo kwenye Vituo vya ukaguzi wa Kilimo kwenye hivyo mipaka miwili
ni pamoja na uduni wa vifaa vya kufanya kazi za Kiofisi, Kutokuwa na vifaa vya
kufanya kazi ya kupimia Sampuli ya mazao katika Maabara ya Holili.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Mtigumwe amewataka watumishi wanaosimamia ukaguzi wa mazao
kutojihusisha na vitendo vya upokeaji Rushwa kwani kwa mtumishi atakayebainika
kufanya hivyo sheria zitachukuliwa haraka dhidi yake ikiwemo kufukuzwa kazi na
kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mpaka huo wa TARAKEA una jumla ya
Njia za panya 250 kutokea Mpaka wa Hororiri mpaka kufikia mpaka wa Namanga.
Aidha, Alisema serikali inaendelea
na juhudi mbalimbali za kuzikabili Njia za panya zote ili kubaini kila aina ya
uhalifu unaofanywa ikiwemo magendo yanayopitishwa kinyemela.
EmoticonEmoticon