WAZIRI UMMY AIBEBA AFRICAN SPORTS YA JIJINI TANGA

October 06, 2017


 WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati akiteta jambo na wachezaji wa timu ya African Sports kabla ya kuwakabidhi hundi milioni 2.1 leo


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi nahodha wa timu ya African Sports hundi ya milioni 2.1 leo wanaoshuhudia ni viongozi wa timu hyo na wachezaji


WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya African Sports mapema leo mara baada ya makabidhiano hayo

 Mmoja kati ya viongozi wa timu ya African Sports wakimshukuru Waziri Ummy kwa msaada huo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo leo

WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewakabidhi timu ya African Sports “Wana kimanu manu”fedha milioni 2.1 kwa ajili ya posho za wachezaji wa timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la pili Tanzania.

Licha ya kukabidhi fedha hizo lakini pia aliwalipia kwenye shirikisho la soka Tanzania (TFF)Laki tano (500,000) kwa ajili ya leseni za wachezaji na ada ya ushiriki wa timu hizo.

Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo,Waziri Ummy alisema ameamua kutoa msaada huo ili kuiwezesha tmu hiyo kuweza kutimiza malengo yake ikiwemo kupanda daraja na kufikia hatua ya kucheza Ligi kuu soka Tanzania Bara.
“Kwani iwapo timu hiyo itarejea Ligi kuu soka Tanzania Bara itasaidia kukua kwa fursa mbalimbali za kiuchumi  katika Jiji la Tanga.
“Sambamba na hilo lakini pia tumepokea mchango wa milioni 3 kutoka Kampuni ya GBP Oil ya Tanga ambao umeweza kuipa hamasa timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano wanayowakabili “Alisema.
Aidha pia Waziri Ummy aliitaka timu hiyo wahakikishe wanafanya vizuri katika michuano hiyo ili kuweza kurejesha hadhi yake ya miaka ya nyuma ilipoweza kuwika katika medani ya soka hapa nchini.
“Ndugu zangu wana African Sports msituangushe hakikisheni mnatumia misaada hii mnayoipata iweza kuwa chachu ya kufikia malengo yenu ya kufanya vizuri “Alisema.
Hata hivyo pia Waziri Ummy aliwafungulia akaunti ya fedha wachezaji wote wa timu hiyo katika benki ya NMB ili iwe rahisi posho zao kulipwa moja kwa moja kupitia benki ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »