Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujengajamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku yaKimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambaloufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya MaendeleoEndelevu.Ufikivu habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewana kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchangokikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike.Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasakwa wasichana na wanawake.Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza nakutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwakwa haki hii ya kibinadamu. Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji nautamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. Wananchi wanahitaji pia kuwa nafikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao unahitajika kufikia,kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. Hii ndiyomaana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote.Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea ahadi yetu yauhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari. Vyombo vya habarihuchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa habari kwa wananchi nakatika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na wakati huo huo vikiwaelimishawafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi. Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wahabari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru.Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katikautekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo nimuhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke namwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.
EmoticonEmoticon