Mgeni rasmi katika hafla ya ufunguzi wa Kiwanda cha kutengeneza mabati cha Kampuni ya ALAF Kanda ya Dodoma, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (mwenye tai), Waheshimiwa Wabunge ambao ni Wajumbe wa kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Viwanda pamoja na Viongozi wajuu wa Kampuni ya ALAF Tanzania wakishirikiana kukata utepe pamoja na kuashilia ufunguzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF kanda ya kati mjini Dodoma.
Kampuni ya ALAF (Tanzania) imefungua tawi lake jipya Mkoani Dodoma ikiwa ni kutekeleza maagizo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma kwa wananchi baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha. Tawi hili limezinduliwa tarehe Septemba 9, 2017 Kizota, Dodoma.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akifungua jiwe la msingi la kiwanda cha mabati cha ALAF Dodoma kwa ajili ya kuhudumia wananchi wa mikoa ya kanda ya kati (Dodoma, Singida na Tabora), Kushoto ni Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema "Napenda kuwahakikishia kwamba Serikali yetu inafanya kila linalowezekana kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa sehemu muhimu ya kuwekeza kwa kulinda mitaji yao kupitia kuondoa ushindani usiokuwa wa haki hasa unaotokana na baadhi ya wafanya biashara kudanganya thamani ya bidhaa za bati zinazoingizwa toka nje ya nchi na kulipa kodi pungufu, kudhibiti uingizaji wa bidhaa zisizokidhi viwango vya ubora na zaidi kulinda amani na maelewano yaliyopo baina ya Serikali na wadau mbalimbali ili kujenga ustawi wa nchi yetu.
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage (kulia) akimueleza jambo Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty.
Waziri Mwijage aliendelea kwa kusema “Napenda kuwashukuru Kampuni ya ALAF (Tanzania) Ltd kwa kutekeleza vizuri maelekezo ya Sera ya Viwanda kwa vitendo na kusogeza huduma zao kwa wananchi wa Dodoma baada ya kufanya hivyo katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Mbeya na Arusha.”
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni ya ALAF, Dipti Mohanty alisema "uwekezaji huu wa Dodoma ni wa thamani ya shilingi bilioni tatu ukiajiri watu 15 moja kwa moja na wengine zaidi ya 100 ajira zisizo za moja kwa moja kama kupakia na kushusha bati, kusafilisha bati, huduma za maji, stationary n.k."
Wageni waalikwa toka mikoa ya kanda ya kati Dodoma, Singida na Tabora.
Pia aliongeza kwa kusema "ALAF inakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo uagizaji wa bidhaa sizizokidhi viwango unaofanywa na makampuni mbalimbali na pia ukwepaji wa kodi, kupelekea serikali kukosa mapato stahiki na walaji kutumia bidhaa zilizo chini ya viwango na hii hupelekea kukatisha tama wawekezaji wa ndani ambao wanajitaidi kuzalisha bidhaa zenye ubora na kulipa kodi zote stahiki.
Meneja wa ALAF kanda ya kati, Grayson Francis Mwakasege akizungumza jambo katika hadhira iliyofika kwa ajiri ya uzinduzi wa kiwanda cha mabati cha ALAF tawi la Dodoma kwa ajiri ya kuhudumia mikoa ya kanda ya kati. [/caption]
ALAF imekuwa ikishiliki kwenye kama vile elimu, makazi, afya na mazingira.Mpaka sasa ALAF imetumia takriban shilingi milioni 200 kwenye mradi wa kuwaelimisha wafanyakazi na jamii kuhusu ukimwi, malaria na kifua kikuu kwa kushilikia na shirika la fedha duniani.
Alikadhalika kwa upande wake Meneja wa ALAF kanda ya kati, Grayson Francis Mwakasege nae aliongeza kwa kusema ufunguaji wa kiwanda hiki Dodoma umeleta ahuenei kwa wakazi wa kanda ya kati Dodoma, Singida na Tabora ambao hapo mwanzo walikuwa wakiagiza bati kutoka Dar es salaam kwa ghalama ya kati ya sh 3000 - 5000 kwa bati la rangi lenye urefu wa kuanzia mita 3 na kuendelea. Pia aliongelea uwezo wa machine zilizofungwa Dodoma kuwa zinaweza kuzalisha tani 50 sawa na nyumba 50 kwa siku.
Picha ya pamoja kati ya mgeni rasmi na wafanyakazi wa ALAF ,wakurugenzi wa wialya za Dodoma pamoja na wabunge wa mkoa wa Dodoma na Singida
Uzinduzi huo pia ulihudhuliwa na kamati ya bunge ya uwekezaji na viwanda pia wabunge kutoka Dodoma na Singida pamoja na mkuu wa wilaya ya Chamwino pia wakurugenzi wa wilaya za Dodoma.
Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.Wasilana nasi kwa namba hizi Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560, Dodoma - 0764 131442 na Mwanza 0682 808 080.
Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited
EmoticonEmoticon