Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’,
Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi kipya kitakachocheza na Malawi
‘The Flame’ katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa chini ya utaratibu wa
kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu
Oktoba 2 hadi Jumatano ya Oktoba 11, mwaka huu ambako Tanzania
imekubaliana kucheza Malawi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Jumamosi ya Oktoba 7, 2017 katika mchezo utakaoanza saa 10.00 jioni.
Katika kikosi hicho cha wachezaji 22, Kocha Mayanga ambaye aliteuliwa
Januari 4, mwaka huu ameita nyota watano wanacheza soka nje ya mipaka
ya Tanzania akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajiwa kuingia kambini Ijumaa Oktoba mosi,
mwaka huu kwenye Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam
kina makipa Aishi Manula (Simba SC), Ramadhani Kabwili (Young Africans)
na Peter Manyika (Singida United).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao
FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Young
Africans), Salim Mbonde (Simba SC), Erasto Nyoni (Simba SC) na Adeyum
Ahmed (Kagera Sugar).
Viungo wa kati ni Himid Mao - Nahodha Msaidizi (Azam FC), Hamis
Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC) na Raphael Daud
(Young Africans).
Viungo wa pembeni ni Saimon Msuva (Difaa El Jadidah/Morocco), Shizza
Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya), Ibrahim Ajib (Young
Africans) na Morel Orgenes (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji) na Mbaraka Yussuph (Azam FC).
Benchi la Ufundi la Mayanga linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni
Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Ame Ninje (Kocha
Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja),
Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa
Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
EmoticonEmoticon