Na Lawrence Raphaely - Bunge.
Balozi
wa China nchini LU Youqing amefika Ofisini kwa Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai Jijini Dar es
Salaam mapema leo kumuaga baada ya muda wake wa kukaa Tanzania kwisha.
Akizungumza
na Spika Ndugai, Balozi huyo alisema kuwa muda wake wa kutumikia kama
Balozi wa China hapa nchini umekwisha hivyo hana budi kuondoka ingawa
angetamani kuendelea kubaki.Balozi
huyo aliongeza kuwa amefurahi kuona kuwa katika kipindi chake chote
akiwa hapa nchini uhusiano baina ya Tanzania na China umezidi kukua.
“Ninafuraha
kubwa wakati ninaporejea China kuona kuwa uhusiano wetu wa kihistoria
umezidi kukua na kwamba kuna ongezeko kubwa la uwekezaji wa China hapa
Tanzania na pia tumesaidia katika utekelezaji wa miradi mingi,” alieleza
Balozi huyo.
Balozi
huyo ambaye amesema kuwa Tanzania ni nchi yake ya mwisho kuhudumu kama
Balozi aliongeza kuwa kwa sasa anarejea nchini China na akiwa huko
ataendelea kujitikita katika shughuli za kudumisha uhusiano baina ya
Tanzania na China.
“Tanzania
ndiyo nchi yangu ya mwisho kuhudumu kama Balozi na nitakaporejea
nyumbani (China) nitaendelea kufanya shughuli nyingine ambazo zinalenga
kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na China,” alisema Balozi
Youqing.
Kutokana
na hilo Balozi Youqing alisema kuwa ingawa anarejea nchini China
lakini yupo tayari kwa Tanzania kuendelea kumtumia kama Balozi wake
katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali zitakozosaidia katika
kudumisha ushirikiano baina wa nchi zote mbili.
“Nipo
tayari kwa Tanzania kuendelea kunitumia kama Balozi wake aliyepo Nchini
China, ninawakaribisha kwa mikono yote miwili tuendelee kufanya kazi
kwa pamoja,” alisema Balozi huyo.
Kwa
upande wake Spika Ndugai alimshukuru Balozi huyo kwa kazi kubwa ambayo
ameifanya akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa daima Watanzania
wataendelea kumkumbuka kwa kazi nzuri aliyoifanya.
“Mimi
binafsi katika kipindi chako ukiwa kama Balozi nimeshuhudia ongezeko
kubwa la watanzania wengi tena wa hali ya chini wakisaifiri kwenda China
kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kibiashara,” alisema Spika Ndugai
na kuonegeza kuwa; kupitia fursa hiyo Watanzania wengi wameweza
kujiajiri kupitia biashara ya kununua bidhaa toka China na kuja kuuza
hapa nchini.
Mhe
Spika pia alimshukuru Balozi Youqing kwa uchakapakazi wake katika
kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia
wataalamu kutoka nchini China.
“Unaondoka
lakini utakapojisikia kurudi, sisi kama Bunge na Serikali kwa ujumla
tupo tayari kukupokea kwa mikono miwili na kuendelea kufanya kazi na
wewe,” alisema Spika Ndugai.
Mbali
na hayo Spika Ndugai pia alimuomba Balozi Youqing kuendelea kuwa Balozi
wa Tanzania atakaporejea nchini China kwa kuendelea kufanya shughuli
ambazo zitasaidia katika kuimarisha ushirikiano baina ya pande zote
mbili.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
(kulia) akizungumza na Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza
muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo
ya Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimueleza jambo
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia na Vyombo ya
Habari- Ubalozi wa China Bi. Wang Fang.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
(kulia) akimkabidhi zawadi Balozi wa China nchini LU Youqing
anayemaliza muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake
Jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake akimkabidhi zawadi
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Katibu wa Spika Bw. Said Yakubu
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
(kulia) katika picha ya pamoja na Balozi wa China nchini LU Youqing
anayemaliza muda wake alipofika kumuaga mapema leo Ofisini kwake
Jijini Dar es Salaam.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Job Ndugai
akiagana na Balozi wa China nchini LU Youqing anayemaliza muda wake
mara baada ya kuzungumza nae mapema leo Ofisini kwake Jijini Dar es
Salaam. Picha na Ofisi ya Bunge
EmoticonEmoticon