Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari
wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka
kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam ,Paul Makonda akikagua kwa kujaribu
kuziendesha Pikipiki hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama
Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya
utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.
.Muonekano wa pikipiki hizo.
Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii
MKUU
wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa
10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi
Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya
China.
Hatua
hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha
ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya
Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo
kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki
hizo.
Makonda
amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la
Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi
sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer
100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo
yaliyokuwa yameharibika.
Aidha
Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya
Dar es salaam kuwakamata Askari wote waliobainika kushirikiana na
wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi
kukamatwa ndani ya masaa Masaa matano.
Agizo
hilo limekuja baada ya hivi juzi msamariamwema kutoa taarifa za uwepo
wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika kwenye Hotel
wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa akaachiliwa na
kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada
ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabainu Askari hao.
Pamoja
na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake
kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi
cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume
Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo hivyo votendeke kwenye Mkoa
wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki vitendeke.
Makonda
kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa
China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi
wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.
Amesema
hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa
Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi
kushindwa kutoa ushirikiano.
EmoticonEmoticon