TAASISI
ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Shirika la
Utafiti lisilo la kiserikali (GRADE) lililopo nchi ya Lima, Peru
zimetengeneza program ya simu ya mkononi inayoitwa LOTIZER inayoweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Teknolojia
hiyo mpya ya kupanga makazi ilioneshwa kwa viongozi, wananchi na
watendaji wa mkoa wa Dar es salaam katika semina iliyofanyika katika
ukumbi wa ESRF.
Programu
hiyo iliyotengenezwa baada ya kufanywa kwa utafiti unaohusu "Upangaji
wa Hiari wa Makazi katika Jamii" katika Mkoa wa Dar es Salaam, imefunzwa
pia kwa madalali.
- Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho ESRF, Profesa Fortunata Makene akitoa neno la ukaribisho kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dr. Tausi Kida kwenye warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mradi
huo wenye lengo la kuimarisha michakato bora zaidi ya kupanga miji
katika nchi zinazoendelea, hususani kwenye makazi yasiyo rasmi inaweza
kupakuliwa kutoka kwenye tovuti ya “www.grade.edu.pe/lotizer” na kuwekwa kwenye simu ya mkononi.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho Profesa Fortunata
Makene ambaye ni mmoja wa watafiti waliozungumza na wananchi wa maeneo
ya holela ya jijini Dar es salaam kama Kivule, Tandika, Tandale na Keko
maghurumbasi, Program hii inaweza kutumiwa na wamiliki ardhi katika
maeneo mapya ya mijini ili kupanga viwanja kabla ya kuuza.
Profesa
Makene alisema kwamba walifanya utafiti kuelewa sababu za kijamii,
kiuchumi na kitamaduni zinazosababisha ukaaji wa watu katika makazi
yasiyo rasmi maeneo ya mijini.
- Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole akiitambulisha na kuelekeza jinsi ya kupakua LOTIZER programu ya simu bure kabisa ambayo ni teknolojia mpya ya kupanga makazi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Aidha
katika utafiti huo pia waliibua changamoto zinazowakabili wakazi
waishio katika makazi yasiyo rasmi, yaani makazi holela na kutafuta
suluhisho la kiteknolojia ya kuwasaidia wanajamii, hususani wenye maeneo
ya kuuza, kuweza kupangilia viwanja kabla ya kuuza.
Imeelezwa
kuwa mara tu inapowekwa kwenye simu, program hiyo inaweza kutumika
kutengeneza mpango wa viwanja wenye ukubwa tofauti kutokana na upendeleo
wa mmiliki ardhi.
Katika
mahojiano na baadhi ya wananchi na watendaji waliofika katika semina
hiyo ya maelekezo, walisifia uwapo wa teknolojia na kusema itasaidia
sana kupanga miji.
- Mtafiti kutoka ESRF, Jires Tunguhole akitoa maelekezo ya namna ya kupakua LOTIZER kupitia simu za Android bure ambayo unaweza kutayarisha mpango wa makazi wa viwanja kwa muda wa dakika moja tu wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano ESRF jijini Dar es Salaam.
Mjumbe
wa mtaa wa Msigani kata ya Msigani Elibariki Mollel alisema kwamba
program hiyo ndio suluhu ya mipango holela kwani inaonekana kuwa na
manufaa makubwa.
Alisema kwamba mafunzo hayo yamewafungua macho na kuwaweka katika hali ya kutambua umuhimu wa mipango miji na mpangilio.
Alisema program hiyo itaondoa matata yaliyopo sasa katika kuwekeza kwenye ardhi.
Naye
dalali wa viwanja Hassan Poronmo wa Mambwepande alisema kwamba mafunzo
waliyopata kuhusiana na mipango miji na uwapo wa program utawasaidia
kushawishi wenye ardhi umuhimu wa mipangilio kwa kutumia program hiyo.
Alisema
wao awali walikuwa wanahaja ya fedha tu lakini kwa sasa baada ya
mafunzo anaona kwamba watakuwa na ushawishi mkubwa zaidi kwa wenye
maeneo wanayotaka kuyauza.
Mmiliki
wa ardhi aliyejitambulisha kwa jina la Mwajuma Hemed wa Mivumoni
maarufu kama Difenda alisema kwamba mafunzo hayo yamemwezesha kutambua
umuhimu wa mipango miji.
Aidha alisema kwamba programu iliyooneshwa inahakikisha usalama wa maisha ya wananchi kutokana na kuwapo kwa mpangilio murua.
- Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Yvonne Matinyi (kulia) akizungumza kuhusu mtrandao wa www.grade.edu.pe/lotizer am
bapo mbali na kupakua program hiyo kuna video na miongozo ambayo itasaidia kujenga makazi mazuri katika maeneo tunayoishi wakati wa warsha ya uenezaji wa programu ya kupanga makazi kwa wamiliki ardhi, madalali, viongozi wa mitaa na wataalamu iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Awali
Prof. Fortunata Songora Makene, Mkuu wa Kitengo the Utafiti na
Machapisho akisoma hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo kwa niaba ya Dk
Tausi Kida – Mkurugenzi Mtendaji, Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF) aliwashukuru washiriki wa semina hiyo na kusema kuwa
utafiti walioufanya uliweza kutoa mchango katika juhudi za serikali
kuweka mipango miji salama.
“Kwa
hiyo utafiti huu ni muhimu katika kuchangia mipango ya serikali na pia
kutoa ushauri wa kisera unaohusiana na upangaji wa makazi bora kwa
maendeleo ya Tanzania.” alisema.
- Mkuu
wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Profesa Fortunata Makene
akielezea kuhusu kijarida cha mwongozo wa mipango miji kinachopatikana
bure katika tovuti ya www.grade.edu.pe/lotizer
wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kulia ni Mtafiti Mwandamizi wa ESRF, Prof. Haidari na kushoto ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Yvonne Matinyi.
EmoticonEmoticon