Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya kusambaza vinywaji ya Victoria General Supply Jonathan Karaze, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi. |
Mkurugenzi wa kampuni ya usambazaji vinywaji Gramba Stanslaus Mmbaga, akiijaribu gari aliyopewa na kampuni ya bia ya Serengeti,wakati wa hafla ya makabidhiano jijini Mwanza jana. baada ya kuibuka mshindi.
|
Washindi wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa SBL |
Mwanza, Agosti 23 2017- Makampuni mawili ya usambazaji vinywaji jijini Mwanza kila moja yatunukiwa gari kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) kwa kuibuka wasambazaji wa juu wa bidhaa zake katika mikoa ya kanda ya ziwa. Makampuni hayo mawili - Gramba Limited kutoka wilaya ya Ilemela na Victoria General Supply Limited kutoka wilaya ya Nyamagana yote yakiwa yamejikita jijini Mwanza
Akikabidhi rasmi magari hayo kwenye sherehe iliyofanyika
kiwandani hapo jijini Mwanza, Meneja
wa kibiashara wa kikanda, Bwana Patrick Kisaka aliwapongeza washindi hao wawili
kwa kujitolea kwao na kujituma kulikowapelekea kushinda gari hizo aina ya
Eicher zenye thamani ya Shilingi 100m/=
Akitolea ufafanuzi, Kisaka alielezea kuwa Kampuni ya Gramba
iliibuka mshindi kwenye kipengele cha uuzwaji wa pombe kali huku Kampuni ya
Victoria General Supply ikiibuka mshindi kwenye kipengele cha msingi wa uuzwaji
bidhaa.
Baadhi ya bia zitolewazo na SBL ni pamoja na Serengeti
Premium Lager, Pilsner, Tusker Lager, Tusker Lite, Kibo Gold, Guinness stout,
Uhuru na Kick. Kampuni pia ni maarufu kwa utoaji wa bidhaa za pombe kali
duniani zikiwemo Johnnie Walker Whisky, Smirnoff Vodka, Gordon’s Gin, Captain
Morgan Rum pamoja na Baileys Irish Cream.
“Tunawapongeza washindi kwa jitihada zao zilizowapelekea
kuwapiku wasambazaji wengine kwa kanda ya ziwa. Huu ni ushahidi tosha wa
kujituma kwao na msukumo wa kufanikiwa kwenye biashara zao” alisema Kisaka
akisisitizia kuwa tuzo hizo, za pili kutolewa mwaka huu ni sehemu ya mpango wa
robo mwaka wa kutoa msukumo kwa wasambazaji wao.
Akiwatia moyo wasambazaji wengine ambao hawajashinda tuzo
hiyo, Kisaka aliwasihi wasambazaji wengine kuongeza juhudi katika kazi zao na
kuwasisitizia kuwa shindano hilo linatoa fursa sawa kwa wote kuweza kujizolea
ushindi huku akiwasihi waendelee kufanya kazi kwa moyo wa ushirikiano na
ushindani katika kufikia malengo waliyojiwekea.
Akitoa salamu zake, Mkurugenzi Mkuu wa Gramba Ltd, Bwana
Stanslaus Mbaga aliwashukuru SBL
kwa wazo lao la ubunifu lililopelekea kukuwa kwa kasi kwa
biashara yake huku akiwasihi
wasambazaji wenzake kutoa ushirikiano kwa SBL kwa ukarimu kwa kufanya kazi kwa bidii
ili kustahili tuzo.
Akiunga mkono maoni ya mshiriki mwenzake, Jonathan Karaze,
Mkurugenzi Mkuu wa Victoria General Supply Ltd, pia alishukuru uongozi wa
Kampuni ya bia SBL kwa kuanzisha shindano hilo huku akisema kuwa limewasaidia
wasambazaji kufanya kazi kwa bidii zaidi
Karaze aliwahakikishia SBL juu ya kujitolea kwake katika
kukuza zaidi mauzo ya bia ya kampuni hiyo kwakuwa kwa sasa tayari analo gari la
usambazaji ambalo litamsaidia kwenye biashara yake hiyo ya usambazaji wa bidhaa
zake.
Hii ni mara ya pili SBL inatoa tuzo hizi kwa wasambazaji
wake kwa kuchochea majukumu yao ya usambazaji wa bidhaa zao nchini. Mwezi Mei
mwaka huu, tuzo hizo zilitolewa kwa MMG Group, msambazaji mwenye biashara zake
wilayani Mpanda mkoani Katavi ambaye alishinda tuzo hizo katika hafla za nusu
ya kwanza ya mwaka huu.
EmoticonEmoticon