SHIRIKA
la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi
vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya
shilingi.
Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini,Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.
Akizungumza
wakati wakukabidhiana vifaa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba UNESCO
inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia
wananchi wengi zaidi.
Aidha
alisema ni muhimu sana kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza
zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza stori
baada ya kukamilika kwake.
Alisema
ipo haja kwa vyombo vya habari kufanyakazi kwa mujibu wa taratibu zao
na kuhakikisha kwamba hawachapishi habari ambazo zinahatarisha uwapo wa
uandishi unaozingatia maadili.
Meneja
wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu aliishukuru UNESCO kwa
kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano.
Alishukuru
UNESCO kwa kuwawezesha kufika katika wilaya tano na kwamba kwa msaada
huo wataokoa shilingi laki saba kwa mwezi kuazima transmita.
“Radio
yetu inawafikia watu 500,000 lakini kwa kupatiwa hivi vifaa tutaweza
kufikia watu milioni 1 katika wilaya zaidi ya tano za Kahama, Shinyanga
Vijijini, Nyang’wale na Mbogwe mkoani Geita na pia Nzega na Uyui mkoani
Tabora ,” alisema meneja huyo .
Kwa mujibu wa Maduhu, kama wasingelipata transmita hiyo wangelikuwa wanatumia sh milioni 8.4 kwa mwaka.
Kwa
upande wake, Ayubu Kalufya wa radio ya jamii Uvinza alisema kwamba
kituo chake kilikuwa kinakodisha transmita kwash laki tano na kufanya
kwa mwaka mzima kutumia sh milioni 6.
Alisema kwa kupata vifaa hivyo walikuwa wanaachama na ukodishaji huo.
Kwa
mujibu wa Kalufya, transmita hiyo mpya itawafikisha mbali zaidi katika
pwani za Ziwa Tanganyika na hivyo kuleta mabadiliko yanayokusudiwa.
Kalufya
alisema wananchi wakisikia mambo mbalimbali ya kuwaelimisha na wao
wakapata nafasi ya kutoa maneno yao haki za binadamu zitakuwa
zimeheshimiwa sana nchini.
- Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya (kulia) akitoa neno la shukrani kwa hivyo Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues (kushoto) wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya radio hizo yaliyofanyika kwenye ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.
Aliishukuru
Unesco kwa kuendelea kuwasaidia na kusema kama si kwa msaada wa UNESCO
jamii zilizopo pembezoni zisingepata nafasi ya kutoa madukuduku yao.
Radio nyingine zilizonufaika na msaada huo ni Pangani FM. Radio hiyo sasa inaweza kusikika Tanga nzima badala ya Pangani pekee.
Katika orodha ya redio zilizopatiwa vifaa ipo pia Mkoani FM ya kutoka Zanzibar.
- Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.
- Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Ofisa Utawala na Rasilimali Watu wa Radio Jamii ya Pangani FM, Rehema Kilapilo wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano Unesco Dar es Salaam.
- Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO Dar es Salaam.
- Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Meneja wa radio ya Jamii ya Baloha FM ya Kahama, Samada Maduhu wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.
- Picha juu na chini ni Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues na Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa hivyo katika hafla fupi iliyofanyika kwenye ofisi za UNESCO jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Maofisa kutoka sekta ya mawasiliano UNESCO.
- Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akikabidhi hati ya makubaliano na moja kati ya vifaa hivyo kwa Mkurugenzi wa Radio Jamii Uvinza FM, Ayubu Kalufya wakati wa hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo jijini Dar es Salaam.
- Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues akigonga 'cheers' na wawakilishi wa redio jamii zilizopokea vifaa hivyo kwenye hafla fupi iliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Unesco jijini Dar es Salaam.
EmoticonEmoticon