Mkurugenzi wa Mkuu wa TIB Corporate Bank,Frank Nyabundege akizungumza wakati wa Jukwaa la Biashara lililofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mahusiano ya Benki ya TIB Corporate ,Theresia Soka akizungumza wakati wa Jukwaa hilo |
TIB Corporate Bank (TIB CBL) wameshiriki katika Jukwaa la Biashara
,Jukwaa hili linakutanisha wadau mbalimbali wa maendeleo ili kujadili na
kuona namna gani Kila mmoja anawezesha mkoa wa Tanga Katika kuleta
maendeleo.
TIB Corporate Bank ni benki ya Biashara na inatoa Huduma zote
za kibenki. Kwa kutambua fursa mbalimbali KTK Mkoa wa tanga, benki
inajiweka sawa ili kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia wana
Tanga.tunambua Kuwa maendeleo yoyote Yale ya kibiashara na viwanda
yanahitaji uwezeshwaji wa kifedha (bank facilities).
TIB Corporate Bank inatoa Huduma mbalimbali kutokana na mahitaji
ya Mteja.Baadhi ya Huduma hizo ni pamoja na akaunti mbalimbali za kwa
makampuni na Watu binafsi,mikopo ya aina mbalimbali ya muda mfupi na
muda wa kati,dhamana za kibenki( bank guarantee),ununuaji na uuzaji wa
fedha za kigeni,uwekezaji katika hati fungani,( treasury bills &
Bonds), ukusanyaji wa fedha na kuwezesha malipo ya jumla kwa makampuni
(cash management ) pamoja na ulipaji wa mishahara kwa Njia rahisi na
haraka
Huduma zetu hutolewa kwa umahiri na ufanisi mkubwa ili kuhakikisha
Mteja anafurahia mahusiano yake na benki.
Pia Huduma ya Premier Banking kwa wateja wanaopenda kujitofautisha zaidi.
EmoticonEmoticon