Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na maofisa ugani wakati akifungua mafunzo ya siku moja ya jinsi ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB). Kutoka kushoto ni Mtafiti, Bestina Daniel kutoka COSTECH na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Shakira Ahmadi, akimkaribisha mgeni rasmi mkuu wa wilaya kufungua mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Mji wa Newala, Calistus Komba, akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Mtafiti Besitina Daniel kutoka COSTECH, akiwatambulisha maofisa wenzake kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Muonekano wa Ukumbi wa Mikutano wa Halmshauri ya Wilaya ya Newala.
Maofisa ugani wakiwa katika mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Mafunzo yakiendelea.
usikivu katika mafunzo hayo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya hiyo, Ally Lilama, akijitambulisha katika mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya hiyo akisoma hutuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo. Wengine waliokaa nyuma ni wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo, akizungumza na watafiti. Kutoka kulia ni Dk.Emmarold Mneney, Benadetha Kimata, Dk.Nicholaus Nyange, Bestina Daniel na Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia katika Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi.
Maofisa ugani wa wilaya hiyo wakijadiliana wakati wa
mafunzo hayo.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney, akitoa mada kuhusu matumizi ya sayansi na teknolojia katika kilimo.
Ofisa Ugani wa Mji wa Newala, Lazaro Nchai, akiuliza swali kuhusu dhana potovu ya matumizi ya bioteknolojia katika kilimo.
Ofisa Ugani wa Kata ya Chikwedu-Chipamanda, Muharami Juma Salim, akiuliza swali katika mafunzo hayo kuhusu zao za mhogo.
Ofisa kutoka Costech, Rose Soloka akiwajibika katika mafunzo hayo.
Na Dotto Mwaibale, Newala
MKUU wa Wilaya ya Newala, Aziza Mangosongo amesema wilaya yake inahitaji teknojia ya kisasa ya kilimo ili kupata mazao mengi yenye tija.
Katika hatua nyingine amesema wilaya yake imejidhatiti katika kilimo kwa kuwa na chakula cha kutosha hivyo kutokuwepo na wasiwasi wa njaa.
Mangosongo ameyasema hayo wilayani hapa leo wakati akifungua mafunzo ya namna ya kutumia sayansi na teknolojia katika kuboresha kilimo kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo ambayo yameandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB).
Alisema wilaya yake inahitaji teknolojia ya kisasa ya kilimo ili kuongeza tija ya kilimo hivyo aliiomba COSTECH kufanya utaratibu wa kutoa mafunzo hayo.
Mangosongo alisema hali ya chakula katika wilaya hiyo ni nzuri na hiyo imetokana na wananchi kujituma na kushirikiana kwa karibu na maofisa ugani.
" Nawaombeni maofisa ugani kuzingatia mafunzo mtakayoyapata ili yaweze kuwasaidia wakulima wetu katika vijijini na kata mnazotoka" alisema Mangosongo.
Alisema wilaya hiyo imepata fursa kubwa ya kupata mafunzo hayo ya kilimo cha kisasa, na kuwataka elimu watakayoipata waipeleke kwa wakulima jambo litakalosaidia kuongeza mara dufu chakula katika wilaya hiyo.
Mwezeshaji kutoka OFAB, Dk. Emmarold Mneney aliwaambia maofisa ugani hao kuwa wameamua kutoa mafuzo hayo kwa kuwa wanaamini kwamba changamoto zinazokabili kilimo ni nyingi hasa magonjwa ya mazao, wadudu waharibifu pamoja na kukosekana
kwa mvua za kutosha.
Alisema mkulima ili aweze kuwa na kilimo chenye tija, lazima aongezee rutuba kwenye udongo wake, atibie mimea sawa na binadamu anavyotibiwa. Alisema sayansi ipo kwa ajili ya kumfanya mkulima apate mazao mengi na sio kuendelea kuwa maskini kama ilivyo sasa.
“Tuko hapa kuelezea namna teknolojia hizi ambazo zinasaidia kukabiliana na changamoto hizo, lengo ni kutaka wakulima wetu wazalishe kwa tija nchi ijitosheleze kwa chakula lakini pia mkulima auze mazao yake na kupata faida,” alisema Dk. Mneney.
Mshauri wa Jukwaa la matumizi ya Bioteknolojia katika kilimo, Dk.Nicholaus Nyange alisema kutokana na ongezeko la watu na ardhi kuwa ile ile matumizi ya sayansi na
teknolojia yanahitajika ili kukabiliana na ukosefu wa ardhi na ukame ambao ni changamoto kubwa kwa wakulima hasa katika kilimo cha mahindi.
"Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi hali ya kilimo imebadilika hivyo ni vizuri kilimo cha mazoea kikaachwa na kufanyika kilimo cha kitafiti chenye tija ambacho kitamwezesha mkulima kupata magunia ya mahindi 35 ya kilo 100 kwa ekari badala ya nane" alisema.
Mtafiti wa Mazao ya Mizizi na Jamii ya Viazi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele mkoani Mtwara, Benadetha Kimata, ametoa wito kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo kutoa ushauri kwa wakulima kutumia mbegu bora za mihogo zenye ukinzani.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB), Philbert Nyinondi aliwajulisha washiriki wa mafunzo hayo kuwa wakulima wa Tanzania hawajabahatika kulima zao lolote lililofanyiwa uhandisi jeni.
" Hadi sasa, hakuna mkulima wa Tanzania aliyewahi au anayelima mazao ya Uhandisi jeni (GMO)
, na sio kulima tu hata wale wanaofuga, hakuna mfugaji mwenye mnyama wa GMO Tanzania." alisema Nyinondi.
Akifafanua kauli yake Philbert Nyinondi alisema watu wengi kwa kutofahamu au kwa makusudi wanawachanganya wakulima hasa wale wanaotumia mbegu za chotara na kuwaambia ndo GMO.
"Tumefikia upotoshaji wa kiwango cha juu sana kwenye jamii. Mtu akiona kitu bora au kilichoboreshwa mfano maembe makubwa, mananasi makubwa, mimea inayokuwa kwa muda mfupi na hata kuku wa kisasa huitwa GMO. Ukweli ni kwamba labda Serikali yetu iamua wakulima wa Tanzania wafaidi teknolojia hii mapema zaidi. Vinginevo, kwa kasi ya watafiti wetu, tunaweza kuwa na zao la kwanza la GMO kwa mkulima kuanzia mwaka 2022" alisema Nyinondi.
Alitanabaisha kuwa upatikanaji wa mazao GMO hata hiyo mwaka 2022 utategemea matokeo ya utafiti unaendelea nchini, tathimini zitakazofanywa na Taasisi ya serikali kama kamati ya kusimamia matumizi salama ya bioteknolojia NBC,
Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Mamlaka wa Uthibiti wa Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na wepesi wa kampuni za mbegu zenye usajili Tanzani kuzalisha mbegu za kutosha kwa ajili ya kusambaza kwa wakulima.

EmoticonEmoticon