Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akiongea
jambo na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina, baada ya mkutano uliofanyika katika Ofisi ya Makamu wa
Rais Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaan Leo.
Mhe. Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza AshaRose Migiro, akizungumza
baada ya kikao na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia
Scotland alipofanya mazungumzo na Naibu Waziri Mpina na wataalaam kuhusu
masuala ya Mazingira, Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe.
Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe. Luhaga Mpina na wajumbe walioshiriki mkutano wa masuala
ya hifadhi ya mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli
jijini Dar es Salaam leo.
Picha ya Pamoja, ikimuonyesha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe.
Patricia Scotland, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na
Mazingira Mhe.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Mhe. Patricia Scotland akizungumza
na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.
Luhaga Mpina Nje ya Ofisi ya Makamu wa Rais Baada ya kumaliza mkutano
ulohusu suala zima la usimamizi na Utunzaji wa Mazingira.
Kushoto Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga Mpina akiongea na Balozi wa Tanzania Nchini Uingereza Mhe.
AshaRose Migiro baada ya kumaliza mazungumzo yaliyoohusu masuala ya
mazingira.
………………………………………………………………..
Katibu wa Jumuiya ya madola Mhe. Patricia Scotland amefanya
mazungumzo na Naibu Waziri Ofisi ya Mkamu wa Rais Muungano na Mazingira
Mhe. Luhaga kuhusu suala zima la Hifadhi na usimamizi wa Mazingira huku
eneo la mabadiliko ya Tabianchi likipewa kipaumbele.
Katika mazungumzo hayo Bi. Scotland alisema kuwa kuna kila sababu ya
nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola kuelewa zaidi suala zima la
mabadiliko ya tabianchi akieleza kuwa wanasayansi wanasema ifikapo mwaka
2050 dunia inaweza kabisa kuepukana na suala la athari kubwa za
mabadiliko ya tabianchi endapo itawezekana kulifanyia kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake Naibu Waziri Mpina alieleza kuwa Tanzania imeathiriwa
na mabadiliko ya tabianchi katika sekta mbalimbali na jitihada
zimefanyika katika kuwezesha jamii kuhimili na kukabiliana na athari za
mabadiliko ya tabianchi.
Alisema serikali inatekeleza Mkakati wa Mabadiliko ya Tabianchi
(2012) ambapo sekta za kilimo, mifugo, uvuvi, nishati zimeandaa na
zinatekeleza mpango kazi wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya
tabianchi katika maeneo yao.
Aidha, Mhe. Mpina alipokumbushwa kuhusu jitihada zake zinazoonekana
wazi katika suala zima la utunzaji wa mazingira hususan katika
oparasheni zake za viwandani, na Balozi Migiro; Mpina alisema kuwa
viwanda vingi nchini alivyovipitia havina mifumo ya kisasa ya kutibu
majitaka akitolea mfano wa jiji la Dar es Salaam Mpina lisema mfumo wa
majitaka katika jiji hilo kwa sasa ni asilimia 13% tuu ndiyo yenye mfumo
mzuri na kuongeza kuwa asilimia iliyobakia haijakaa vizuri, jambo
ambalo si salama kwa viumbe hai na mazingira.
Awali, akiongea katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini
Uingerea Mhe. Asharose Migiro akitolea mfano wa athari za mabadiliko ya
tabia nchi katika maeneo ya ufukwe ya ocean road ambayo imelika,
alisema wakati umefika sasa kwa Tanzania kuonyesha ushirikiano katika
suala hili na wananchi kuelewa shughuli za kibinadamu zinazochangia
kuongeza athari za mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Amefanya mazungumzo hayo leo na
Naibu waziri Mpina na Team ya wataalam baada ya kutembelea kisiwa cha
Zanzibar.
EmoticonEmoticon